Maisha ya nabii



Yüklə 0,69 Mb.
səhifə13/15
tarix10.12.2017
ölçüsü0,69 Mb.
#34382
1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   15

(Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliyowapa mahari yao, na (wanawake) uliyowamiliki kwa mkono wako wa kulia katika wale aliokupa Allah, na tumekuhalalishia mabinti wa ami zako, na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa mama zako wadogo…)
Kwa hivyo, ni wazi kwa mujibu wa Aya hii kwamba Bibi Amina alikuwa na ndugu wa kike na wa kiume ambao ni wajomba na mama wadogo wa Mtume (s.a.w.). Lakini Sheikh aliposema kuwa Mtume (s.a.w.) hana wajomba wala mama wadogo labda kakusudia kwamba Mtume (s.a.w.) alipozaliwa hao wajomba zake na mama zake wadogo walikuwa wameshafariki dunia.

1 -Bwana wenyewe alikuwa ni Abu Umayya bin Al- Mughira Al-Makhzumi.

1 - Kusema kwake Sheikh "Dini ya Kimasihi" haimaanishi kwamba Nabii Issa alikuja na dini isiyo ya Kiislamu; laa! Bali alikuja na Uislamu kama walivyokuja nao Mitume wengine kwani hii ndio dini pekee ya mbinguni, na lile linalofanywa na baadhi ya watu wengi hii leo hasa wa nchi za Kiarabu la kumwita mkristo kuwa ni Masihi ni kosa kubwa, kwa sababu Masihi ni sifa iliyotoka kwa Allah kwa kumsifu Mtume wake Nabii Issa, kwa hivyo hii si sifa ya mwenye kulielekea sanamu wakati wa Ibada na kumgawa Mungu sehemu tatu: Baba, mwana na roho mtakatifu. Kwani wale wamesifiwa na hali hawa wamelaaniwa.


1 - Jibril alikuwa akenda kwa njia mbili, ya kwanza ni kwa sura ya binaadamu na ndio njia ambayo kwayo Masahaba waliweza kumuona baadhi ya wakati. Njia ya pili ni kwa sura yake ya Kimalaika. Hili limemtokea Mtume (s.a.w.) mara mbili tu: ya kwanza ni hapa hapa ardhini. Anasema Allah Mtukufu katika Sura ya 81 Aya ya 23: وَلَقَدْ رَآهُ بِالأُفُقِ الْمُبِين (Na hakika yeye alimwona (Jibril) katika upeo wa macho ulio safi kabisa). Na mara ya pili alipokwenda mbinguni, kama alivyosema Allah katika Suratu An-Najm Aya ya 13: وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَى (Na akamwona (Jibril) kwa mara nyengine - katika sura yake ya Kimalaika – ).

1 - Aya zenyewe ni hizi, anasema Allah Mtukufu: يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ (1) قُمْ فَأَنذِرْ (2) وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ (3) وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ (4) وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ (5) وَلا تَمْنُنْ تَسْتَكْثِرُ (6) وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ (7) (Ewe uliyejifunika maguo (1) Simama uonye (2) Na Mola wako umtukuze (3) Na nguo zako uzisafishe (4) Na mabaya yapuuze (5) Wala usiwafanyie ihsani (viumbe) ili upate kujikithirishia (hapa duniani) (6) Na kwa ajili ya Mola wako fanya subira (7).

1 - Hakuwa ndiye wa mwanzo na wa mwisho. Yaani hakuwa ndiye huyo huyo tu.

2 - Takwimu za sasa zinaashiria kuwa ni kiasi cha Bilioni moja na nusu na zaidi.

1 - Na wa mwanzo katika aliowafikishia ujumbe huu kwa njia za siri walikuwa ni watu wake wa karibu kama Allah alivyomwamrisha kwa kusema:
وَأنْذِرْ عَشِيْرَتَكَ الأقْرَبِيْنَ

(Na waonye jamaa zako waliokaribu ((nawe))
Hapo Mtume (s.a.w.) akawakusanya jamaa zake akawaambia:

((يَا بَنِيْ عَبْد الْمُطَّلِب، إنَّ اللهَ أمَرَنِيْ أنْ أنْذِرَكُمْ إشْتَرُوْا أنْفُسَكُمْ مِنَ اللهِ ، فَإنِّيْ لاَ أُغْنِيْ عَنْكُمْ مِنَ اللهِ شَيْئًا، ألاَ وَإنَّ أوْلِيَائِيْ مِنْكُمُ الْمُتَّقِوْنَ ، ألاَ لأَعْرِفَنََّ مَا جَاءَ النَّاس غدًا باِلدِّيْنِ وَجِئْتُمْ بِالدُّنْيَا تَحْمِلُوْنَهَا عَلَى رِقَابِكُمْ ، يَا فَاطِمَةُ بِنْت مُحَمَّدٍ وَيَا صَفِيَّةُ عَمََّة مُحَمَّدٍ إشْتَرِيَا أنْفُسَكُمَا مِنَ اللهِ ، فَإِنِّيْ لاَ أُغْنِيْ عَنْكُمَا مِنَ اللهِ شَيْئًا))
((Enyi kizazi cha Abdul Muttalib! Hakika Allah kaniamrisha nikuonyeni, basi zinunuweni (zikomboeni) nafsi zenu kwa Allah, kwani mimi sikufaeni chochote mbele ya Allah. Jueni kwamba hakika ya vipenzi vyangu miongoni mwenu ni wale wacha Mungu. Jueni kwamba watu nitakaowajua ni wale watakaonijia kesho na hali wameshika dini, na hali mtanijia nyinyi na huku mumeibeba dunia shingoni mwenu. Ewe Fatma mtoto wa Muhammad na ewe Safiyya shangazi wa Muhammad , zinunuweni nafsi zenu kwa Allah hakika mimi sikufaeni chochote mbele ya Allah)).
Hadithi hii inaashiria mambo mawili muhimu:

  1. Nasaba haifai kitu huko akhera. Kama Aya na Hadithi nyengine zinavyoeleza.

  2. Ucha Mungu tu ndio utaomfaa mtu huko.




1 - Aya yenyewe inasema kuwa: فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنْ الْمُشْرِكِينَ (Basi pasua (yatangaze kwa uwazi) ulioamrishwa (wala usijali upinzani wao) na wapuuzilie mbali hao washirikina). Sura 15, Aya 94.

2 - Mwaminifu.

1 - Yaani “Mbebaji wa kuni” (za fitina, mwenye kuwafitini watu kwa kutia maneno baina yao). Na kuna tafsiri nyengine pia iliofasiriwa Aya hii.

2 - Yaani baba la ujinga.

1 - Vile vile baada ya kumaliza Utba kuyasema hayo Mtume (s.a.w) alimwambia: Je umeshamaliza Ewe Aba Al-Walid? Akasema: “Ndio.” Mtume (s.a.w) akasema basi nisikilize! Hapo akasoma Surat Fussilat mpaka Aya ya 38 ambayo ni sehemu ya sijida akasujudu kisha akamwambia: “Umesikia Ewe Aba Al-Walid uliyoyasikia kwa hivyo wewe na uliyoyasikia”. Na riwaya nyengine inasema kwamba Mtume (s.a.w) alisoma Sura hiyo mpaka Aya ya 13 isemayo: (Basi kama wakipuuza sema nakuhadharisheni na adhabu mfano wa adhabu ya Adi na Thamud) alipofika hapo Utba akamwambia Mtume (s.a.w) basi inatosha.

1 - Na wengine wanasema kuwa walikuwa idadi yao ni 16. wanaume 12 na wanawake 4. Tazama Mbarakfuri Al-Rahiqul Makhtuum uk. 73.

2 - Na hiyo ndiyo iliyokuwa Hijra ya pili ya Waislamu kwenda Uhabeshi.

3 - Bwana Jaafar bin Abi Talib vile vile ndiye aliyekuwa msemaji wa Waislamu katika majadiliano yaliofanyika mbele ya Najashi Mfalme wa Uhabeshi pale walipokwenda Makureshi kuwatilia fitna.

4 - Watu wenyewe waliopelekwa kwa Mfalme huyo kwa ajili ya kuwafitini Waislamu ni Amru bin Al-‘Aas na Abdallah bin Abi Rabiia na wakati huo walikuwa hawajasilimu.

1 - Na kauli nyengine inasema kuwa ilikuwa ni mwaka wa sita baada ya kuja Utume. Mbarakfuriy Al-Rahiqul Makhtuum uk. 81.



1 - Na vile vile inasemwa kwamba kuvunjika kwa mkataba huo wa Makureshi ilikuwa ni katika mwezi wa mfunguo nne mwaka wa kumi wa kuja Utume. Tazama Mubarakfuri Al-Rahiqu Al-Mahtum uk. 88.

1 - Na inasemwa kwamba Abu Talib alifariki miezi sita baada kuvunjika mkataba wa Makureshi yaani katika mwezi wa Rajab. Tazama Mubarakfuri Al-Rahiqu Al-Mahtum uk. 92. Na hii ni kwa kuizingatia kauli ya waliosema kwamba mkataba wa Makureshi ulivunjika kwenye mwaka wa kumi katika mwezi wa Mfunguo nne. Ama tukichukua kauli ya waliosema kuwa alifariki Ramadhani itamaanisha kwamba alifariki miezi minane baada ya kuvunjika mkataba wa Makureshi. Lakini kwa mujibu wa riwaya aliyotunakilia Sheikh Abdallah Saleh Al-Farisi ni kuwa yeye alifariki katikati ya mfunguo mosi kwenye mwaka wa kumi wa kuja Utume, na hii inamaanisha kuwa alifariki siku chache tu baada ya kuvunjika mkataba wa Makureshi, kwani – kwa mujibu wa Sheikh – ni kuwa mkataba huo ulivunjika awali ya mwezi wa mfunguo mosi mwaka huo wa kumi.

1 - Tumeona katika maelezo ya Sheikh Abdallah Saleh Al-Farisi kwamba Bw. Abu Talib kafa katikati ya mwezi wa mfunguo mosi, kwa hivyo kusema kuwa Bibi Khadija kafa siku tatu baada ya kifo cha Abu Talib, kunamaanisha kwamba Bibi Khadija naye kafa katika mwezi wa mfunguo mosi. Ama tukichukuwa kauli isemayo kwamba Abu Talib alikufa katika mwezi wa Rajab na kwamba Bibi Khadija alikufa mwezi wa Ramadhani kama ilivyo mashuhuri, basi hii itamaanisha kuwa Bibi Khadija alikufa miezi miwili baada ya kifo cha Abu Talib.



1 - Mbingu hazijulikani hakika yake ni nini. (Sheikh: Abadallah Saleh Al Farisi).

2 - Moja katika madhehebu yaliyokuwa na nguvu na wanavyuoni wakubwa zamani. (Sheikh: Abdallah Saleh Al Farisi).

3 - Aya yenyewe ni hii:
سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّه هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
(Utukufu ni Wake Yeye Ambaye alimpeleka mja Wake usiku ( mmoja tu) kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa Al-Baytu Al-Muqaddas) ambao (tumeubariki na) tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake, ili tumwonyeshe baadhi ya Alama zetu. Hakika Yeye (Allah) ni mwenye kusikia (na) mwenye kuona).


1 - Hii ndio kauli ya Jumhur. Lakini kuna kauli nyengine kuwa ilikuwa ni mwaka ambao Mtume (s.a.w) kapewa Utume. Na ikasemwa kuwa ilikuwa baada ya kupewa Utume kwa miaka mitano. Na ikasemwa kuwa ilikuwa ni usiku wa mwezi ishirini na saba Rajab mwaka wa kumi wa kupewa Utume. Lakini kauli hizi tatu zimerudishwa kwani inajulikana wazi kuwa sala tano zimefaradhishwa katika tokeo hilo la Mi'iraj, na kwamba Bibi Khadija hakuziwahi sala tano kwani yeye alikufa Ramadhani mwaka wa kumi. Sasa tukidai kuwa safari hiyo ilikuwa katika mwaka wa mwanzo au wa tano au wa kumi katika mwezi wa Rajab hii itakuwa na maana kuwa Bibi Khadija alikufa baada ya kufaradhishwa sala tano, na hili ni kinyume na uhakika. Kwa hivyo kauli tunazoweza kuzizingatia ni zile zisemazo kuwa tokeo hili lilikuwa kabla ya Hijra kwa miezi kumi na sita yaani Ramadhani mwaka wa kumi na mbili wa Utume, au kabla ya Hijra kwa mwaka na miezi miwili yaani mfunguo nne mwaka wa kumi na tatu wa Utume, au kabla ya Hijra kwa mwaka mmoja yaani katika mwezi wa mfunguo sita mwaka wa kumi na tatu wa Utume. Kauli hizi pamoja na ya Sheikh Abdallah Saleh Farsiy ndizo zinazoweza kuchukuliwa kwa kuzingatia kwamba tokeo hili tukufu ndani yake zimefaradhishwa sala tano wakati ambapo Bibi Khadija alikuwa hayupo tena duniani. Rejea Mubarakfuri Al-Rahiqu Al-Mahtum uk. 111.

2 - الْحَمْدُ لِلَّهِ فَاطِرِ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلائِكَةِ رُسُلاً أُولِي أَجْنِحَةٍ مَثْنَى وَثُلاثَ وَرُبَاعَ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

(Sifa zote njema ni za Allah Muumba wa mbingu na ardhi aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili mbili na tatu tatu na nne nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo, bila shaka Allah ni mwenye uwezo juu ya kila kitu). Surat Fatir: Aya ya 1.

1 - Kilichopunguzwa hapa ni idadi ya sala, ama ujira inasemwa kuwa haukupunguzwa bali mtu hulipwa malipo ya zile zile sala khamsini kwa kusali sala tano hizi. Na hizi ni miongoni mwa rehma za Allah kwa waja wake.

1 - Yaani Aya isemayo kuhusu hali ya Fir'auna na wafuasi wake kwamba: النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوّاً وَعَشِيّاً Adhabu za motoni wanadhihirishiwa (makaburini mwao) asubuhi na jioni …. Anasema Sheikh Muhammad 'Ali Al-Sabuni kwamba maana ya Aya ni: "Wanaunguzwa kwa moto asubuhi na jioni. Wamesema wafasiri: 'Makusudio ya moto hapa ni moto wa kaburini". Saf-watu Al-Tafasir j. 3, uk. 74.

2 - Inawezekana ikawa labda wako baadhi ya wanavyuoni wenye kauli hii na ikawa labda Sheikh anakusudia kusimulia tu kauli hio. Kwani ukitazama maneno yake yaliotangulia utaona kwamba kanukuu kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo kuhusu kaburi kuwa: “Ima ni bustani katika mabustani ya Peponi au ni shimo katika mashimo ya Motoni.” Ni matarajio yetu kwamba Hadithi hii ndio hasa tegemeo la Sheikh katika maudhui hii, nayo kama unavyoona inaonesha kuwa kaburi ima kuna mateso au starehe. Cha kujua hapa ni kuwa dhambi ziko za namna mbili: kubwa na ndogo. Anayejiepusha na kubwa basi ndogo hufutiwa. Ushahidi ni Aya isemayo: "Ikiwa mutajiepusha na madhambi makubwa munayokatazwa, basi madogo madogo tutakufutieni." (Al-Nisaai 31). Ama mwenye madhambi makubwa yeye ni lazima atubie, na hili ndilo linalomaanishwa na Aya zote nyengine zenye kuhimiza toba kama Aya isemayo: "Na hakika mimi ni mwenye kusamehe sana kwa aliyetubia na akaamini na akafanya mema kisha akashika uongofu." (Taha 82). Utaona hapa kwamba msamaha wa Allah kwa waja wake umefungamanishwa na kutubia kwao waja hao.

1 - Inaonekana kwamba neno hili hapa ni kosa la chapa, kwani neno hili maana yake ni “Kumkosesha” yaani kusema kuwa fulani kakosea, au “kumkadhibisha” au kudhoofika mawazo kutokana na uzee, na bila shaka haya si makusudio ya Sheikh hapa bali dhahiri inaonekana kwamba neno lililokusudiwa hapa ni “Alimfananishia”.

1 - سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الآفَاقِ وَفِي أَنْفُسِهِمْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ... (53)

1 - Taif iko umbali wa kiasi cha meli sitini kutoka Makka.

1 - Ndugu yake Utba alikuwa akiitwa Shaybah bin Rabia, na shamba hilo lilikuwa kiasi cha meli tatu kutoka Taif.

2 - Mtumwa huyo aliyekuwa akiitwa Addaas baada ya kumwona Mtume (s.a.w.) anapiga Bismillahi kabla ya kula, alistaajabu sana na akamwambia kuwa watu wa miji hii hawasemi maneno haya?! Mtume (s.a.w) alimuuliza kijana huyo 'Je wewe unatoka mji gani?' Akamjibu: 'Mimi ni Nasara kutoka Naynawa, (mji katika miji ya Iraq).' Mtume (s.a.w.) akamwambia: 'Unatoka katika kijiji cha mtu mwema Yunus bin Matta?' Kijana yule akashangaa sana kuona kwamba Mtume (s.a.w.) kamtaja Yunus bin Matta (Nabii Yunus) kwani hakufikiria kwamba yeye anamjua. Kwa hivyo kijana huyo akamuuliza Mtume (s.a.w.) vipi anamjua Yunus bin Matta? Mtume (s.a.w.) akamwambia: “Huyo ni ndugu yangu alikuwa Nabii nami ni Nabii”. Kwa hivyo, kijana huyo baada ya kupata habari za Nabii Yunus kutoka kwa Mtume (s.a.w) akamkubali kuwa huyu ni Mtume wa kweli na akasilimu papo hapo. Na aliporudi kwa Bwana wake akamwambia: “E bwana wangu hakuna katika ardhi kilichobora zaidi kuliko mtu huyu kwa hakika kaniambia mambo hakuna ayajuaye isipokua Mtume”. Tazama Mbarakfuri Al-Rahiq Al-Mahtum uk. 102.

3 - Awaangamize kwa kuwababatiza (kuwabataniza) baina ya majabali mawili ya Makka, moja linaitwa Abu Qubays na la pili lililokabiliana nalo linaitwa Qu’ayqi’an. Mbarakfuri Al-Rahiq Al-Mahtum uk. 102.

1 - Yaani katika Aya isemayo: وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلاَّ رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ (Hatukukutuma ila uwe rehma kwa walimwengu wote) Suratul Anbiyaa: Aya 107.

1 - Kusema kwake Sheikh kwamba Mtume (s.a.w) alimuamrisha Bwana Hassan bin Thabit amsifu Mut’im kwa nyimbo hakusudii kwamba Mtume (s.a.w) alikuwa akiamrisha kuimba, la hasha! Na ndio maana utaona kuwa Mtume (s.a.w) alipojiwa na wageni 12 kutoka Madina kutaka kufundishwa mambo ya dini yao, Mtume (s.a.w.) aliwapa Bwana Mus’ab bin Umeyr na Bwana Abdalla bin Umm Maktum ili wakawafundishe dini; na miongoni mwa aliyowataka Mtume (s.a.w) watu hao ni kuwa: Wasiabudu chochote kingine ila Allah na wala wasikwimbe. Kwa hivyo, alichokiamrisha Mtume (s.a.w) kule ni mashairi.


2 - Na imekuja vile vile habari hii katika Sura ya 46 ya Suratul Ahqaaf kuanzia Aya ya 29.

1 - Na zimekuja Riwaya kuonesha kwamba Makureshi walipomtaka Walid atowe rai yake baada ya kuzikataa rai zao, alisema: “Nipeni muda nifikiri” baada ya kuvuta fikra akatoa rai yake hiyo. Na Allah akaiteresha Qur-ani kuhusu Walid na kufikiri kwake katika Surat Al-Muddath-thir kuanzia Aya ya 11 – 26.

1 - Baadhi ya Waarabu walikuwa wakiwaua watoto wao wanawake kwa kuchelea aibu, na wanaume wanapochelea ufakiri. (Sheikh Abdallah Saleh Al-Farisi).


1 - Huenda ikawa kusema kwake Sheikh kwamba Waarabu wanaanza mwaka wao mpya kila Mfunguo nne, imetokana na kule kuwa yeye anazungumzia katika Kitabu hiki yale yaliojiri katika ulimwengu au jamii ya Kiarabu, lakini bila shaka alilolikusudia yeye ni kusema kuwa: “Waislamu huanza mwaka wao mpya kila Mfunguo nne”.

1 - Alitoka Sayyidna Umar (r.a.) na huku anawambia Makureshi kuwa: “Mwenye kutaka kumwacha mkewe kizuka na watoto wake mayatima basi anifuate” lakini hakuna hata mmoja aliyemsogelea. Ama hili la kuonesha ushujaa wa Sayyidna Umar (r.a), wale ambao hawamkubali yeye wanalipinga kama wanavyoipinga kauli ya kusema kwamba Waislamu walidhihirisha ibada zao baada ya kusilimu Sayyidna Umar. Siku moja nilizungumza na kijana mmoja katika hao wasiomkubali 'Umar akaniambia: “Ikiwa kweli Umar huyu kadhihirisha ushujaa wake kwa Makureshi wote wa Makka mbele ya macho yao. Je ni kitu gani kilichomwogopesha hata akashindwa kwenda kupeleka ujumbe kwa Makureshi hao hao pale Mtume (s.a.w.) alipowataka Masahaba wake ajitokeze mmoja wao kwenda kupeleka ujumbe kwamba makusudio ya kutua kwao hapo Hudaybiya si mengine ila wanataka waingie Makka wakafanye Umra muda wa siku 1 tu, halafu waondoke wende zao, na wote wakaogopa kwenda Makka hata huyo Umar mwenyewe na badala yake akajitokeza Sayyidna Uthman. Je inayumkinika kuwa Umar huyu kawambia Makureshi wa Makka nzima hayo aliyowambia na hali tunaona hapa kuwa kaogopa kwenda kwa Makureshi hao hao na ujumbe wa Mtume (s.a.w.)?!”
Kisha akaendelea na kusema: “Kisha katika vita vya Khandaq, Mtume (s.a.w.) alipowataka Masahaba wake ajitokeze mmoja wao vile vile kwenda kupigana na kafiri aitwaye Amr bin Abd-Wud wote waliogopa hata huyo Umar mwenyewe, na badala yake akajitokeza Al-Imam Ali akakabiliana naye na akamuua. Kwa hivyo, si kweli kwamba aliwaambia Makureshi wote wa Makka maneno hayo na hali hapa tunamwona anaogopa kukabiliana na kafiri mmoja tu, na kwa hivyo, hayakuwa madai yenu hayo ila ni kutaka kumpandisha cheo Umar tu: si chengine”.
Mimi sikuwa na haja ya kujadili njia alizotumia katika kusimulia visa hivyo, bali nilikuwa na haya machache tu ya kumwambia. Nilimuuliza: Je inayumkinika kuwa Sayyidna Uthman alijitokeza kwenda kuwakabili Makureshi wote wa Makka kwa kupeleka ujumbe wa Mtume (s.a.w.) ?! Akasema: “Ndiyo”. Nami sikumkatalia juu ya hili kwani hoja yangu haikuwepo hapo. Nikamwambia: Ikiwa ni hivyo, je inayumkinika kuwa Sayyidna Uthman huyo aliyeweza kujitokeza kwenda kuwakabili Makureshi wote wa Makka amwogope kafiri mmoja ambaye ni Amr bin Abd Wud katika vita vya Khandaq?! Unaonaje nikikwambia kuwa hayakuwa madai yako haya ila ni kutaka kumpa cheo Sayyidna Ali tu?! Hapa sikuweza kupate jawabu kutoka kwake!
Na kawa kuongezea ni kuwa: Sayyidna Ali alipotaka kwenda zake Makka alipanda juu ya jabali akasema: “Yoyote mwenye kuweka amana kwa Nabii Muhammad (s.a.w.) naaje achukue, kabla sijaondoka Makka”. Sasa tumuulize yule ndugu yetu aliyempinzani wa 'Umar. Je tusiamini kuwa Ali alionyesha ushujaa wake kwa kutangaza Hijira yake mbele ya Makureshi? Ikiwa tuamini ushujaa huu wa Ali, swali ni kuwa. Je kule Sayyidna Othman kwenda kwake kufikisha ujumbe wa Mtume (s.a.w) kwa Makureshi, ilhali Ali alikuwepo, kulimaanisha kuwa Ali hakuyasema haya? Au tujenge hoja kuwa ikiwa Ali kayasema hayo kwanini kashindwa kwenda kwa Makureshi!?



1 - Watatu katika Bani Umayya ni Abu Sufyan bin Harb na ndugu wawili Shaybah bin Rabi’a na Utbah bin Rabi’a. Na mmoja katika Bani Makhzum ni Abu Jahal bin Hisham. Na watatu katika Bani Naufal ni Jubeyr bin Mut’im na Tu’ayma bin Uday na Al-Harith bin 'Amir. Na wawili katika Bani Sahm ni ndugu wawili Nubayh bin Al-Hajjaj na Munabbih bin Al-Hajjaj. Na mmoja katika Bani Abdid Dar ni An-Nadhr bin Al-Harith. Na mmoja katika Bani Jumah ni Umayya bin Khalif. Na watatu katika Bani Asad ni Abu Al-Bakhtari bin Hisham na Zam’a bin Al–Aswad na Hakiim bin Huzam.


2 - Hii ilikuwa ni rai ya Abu Al-Bakhtari.

3 - Ama rai hii ya kutolewa Mtume (s.a.w) katika nchi ilikuwa ni rai ya Abu Al-Aswad.

1 - Rai hii ya nne ilikuwa ni rai ya Abu Jahal bin Hisham.

2 - Diya ni mali wanayopewa jamaa za aliyeuliwa, ikiwa wamesamehe kumwua yule aliyewauliya jamaa yao. (Sheikh Abdallah Saleh Al Farsi) .

1 - Yaani mwanawe Sayyidna Abubakar, Bibi Asmaa.

2 - Na imesemwa kuwa Bwana 'Amr bin Fuhayra alikuwa akiwapitisha wanyama hao zile sehemu alizopita Abdallah mtoto wa Sayyidna Abu Bakr ili kuficha alama za nyayo zitakazowawezesha Makureshi kujua kwamba kumepita mtu kwenda katika pango hilo.

1 - Aya yenyewe ni hii:
قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ فَإِنَّهُمْ لا يُكَذِّبُونَكَ وَلَكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّهِ يَجْحَدُونَ
(Tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema (katika kukutukana na kukukadhibisha). Basi wao hawakukadhibishi wewe laikini madhalimu hao wanakanusha hoja za Mwenyezi Mungu).
Imepokewa kwamba Mtume (s.a.w.) alipita kwa Abu Jahl na masahibu zake wakamwambia: “E’ Muhammad! Wallahi sisi hatukukadhibishi wewe, kwani wewe kwetu ni mkweli, lakini tunayakadhibisha haya uliyokuja nayo” kwa hivyo, Allah akaiteremsha Aya hii.

1 - Anasema Allah katika Surat Attaubah Aya 40:
إِلاَّ تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّهَ مَعَنَا
(Kama hamtamnusuru (Mtume s.a.w) basi Allah alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru, alipokuwa (mmoja tu na mwenziwe) wa pili (Yeye na Abubakar) walipokuwa pangoni ambapo alimwambia sahibu yake usihuzunike kwani Allah yuko pamoja nasi…).
Tunajua kuwa kuna baadhi ya ndugu zetu wana msimamo tofauti na Jamuhuri ya Umma kuhusu Sayyidna Abu Bakr na Sayyidna Umar. Siku moja kijana mmoja alinihadithia kuwa miongoni mwa hoja walizozitegemea baadhi ya wanavyuoni katika kuonesha ubora wa Abu Bakr ni Aya hii ambayo ndani yake Allah kamwita Abu Bakr kuwa ni Sahibu wa Mjumbe wake na ambapo Mtume (s.a.w) anamwambia sahibu yake huyo kwamba usihuzunike kwani Allah yuko pamoja nasi. Anasema kijana hoyo kwamba, lakini wako wengine ambao hawakuona ubora wowote wa Abu Bakr ulioainishwa na Aya hiyo, kwani wao wanasema kuwa Allah hata Makafiri kawaita kuwa ni Sahibu za Mtume (s.a.w) pale aliposema katika Surat Kuwwirat Aya 22, وَمَا صَاحِبُكُمْ بِمَجْنُونٍ (Na wala Sahibu yenu (huyu Muhammad) si mwendawazimu). Na katika Surat Al A’araf Aya 184 anasema: أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا مَا بِصَاحِبِهِمْ مِنْ جِنَّةٍ... (Je basi hawatafakari kwamba Sahibu yao (huyu) hana wazimu). Na katika Surat Saba-a Aya 46 ... مَا بِصَاحِبِكُمْ مِنْ جِنَّةٍ (Sahibu yenu huyu hana wazimu). Suala linaloulizwa ni: je kutakuwa na ubora gani na utukufu gani kwa makafiri kwa sababu ya kuambiwa kuwa Mtume (s.a.w) ni sahibu yao? Tunasema: Neno moja linaweza likawa na maana tofauti kwa kuzingatia Qarina (context). Kwa mfano: Neno “Aya” “آية” katika kauli ya Allah isemayo: وَقَوْمَ نُوحٍ لَمَّا كَذَّبُوا الرُّسُلَ أَغْرَقْنَاهُمْ وَجَعَلْنَاهُمْ لِلنَّاسِ آيَةً ... (Na watu wa Nuh, walipowakadhibisha Mitume tuliwaangamiza kisha tukawafanya kuwa ni “Aya” kwa watu) - Furqan 37. Kufanywa makafiri hapa kuwa ni Aya kwa watu ni tofauti na kufanywa kwa Nabii Issa kuwa Aya pale Allah aliposema: وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِنَّا.... (Na ili tumfanye “Aya” kwa watu na rehema itokayo kwetu) – Maryam 21. "Aya" katika Aya inayosimulia habari za Nabii Nuh na makafiri wa Umma wake maana yake ni "Mazingatio", wakati "Aya" katika Aya hii inayosimulia habari za Nabii Issa ni "Muujiza". Kwa hivyo, kinachozingatiwa sio neno tu, bali ni neno pamoja na Qarina ambayo ndiyo yenye kutoa makusudio ya neno. Ukiniuliza je ni Qarina gani hio iliompa Abu Bakr sifa njema kule? Nitakwambia ni kauli yake Allah aliposema: "Usihuzunike kwani Allah yuko pamoja nasi". Maneno haya Mtume (s.a.w.) hawezi kumwambia mtu muovu. Hivyo basi, neno “Sahibu” inawezekana likatumika kumaanisha usuhuba wa kiuadui au wa kimapenzi, na hakuna chenye kutafautisha makusudio ya usuhuba uliopo baina ya pande mbili hizi kuwa ni wa kimapenzi au wa kiuadui ila kwa kutazamwa Qarina (context) – Sibaq au Siyaq ya Aya.

1 - Katika sehemu zote Sheikh alikuwa anasema “Vijana wa Kikureshi” sio “Vijana vya Kikureshi,” kwa hivyo huenda ikawa hili hapa ni kosa la chapa au huenda ikawa kakusudia kuwadogosha (Tasghiir) vijana hao, kwamba ni vijana wadogo.

1 - Vile vile Bibi huyu alikuwa akijulikana kwa jina la Ummu Ma’abad na mumewe ikijulikana kwa jina la Abu Ma’abad.

2 - Suraqa bin Malik bin Ju’ushum.

3 - Kwa Kipemba, punda anapokwenda mbio za wastani huku akiruka kwa miguu yote mine, huambiwa anapiga shoti. Huenda ikawa neno hili katika lahaja nyengine za Kiswahili, lina maana sawa na maana yake katika lahaja ya Kipemba.

4 - Kupiga ramli au kutizamia.

1 - Katika maelezo yaliotangulia ya Sheikh, alisema: “Nabii Muhammad na Sayyidna Abubakr walisalia katika pango muda wa siku 3: Ijumaa, Jumaamosi na Jumaapili.” Pia tumeona katika maelezo ya Sheikh kwamba vijana wa Kikureshi walikwenda kutaka kumuua Mtume (s.a.w) siku ya Ijumaa ya mwezi mosi au pili. Kwa hivyo, ikiwa imethibiti kuwa Ijumaa ilikuwa ni mwezi mosi basi Jumaatatu ya pili itakuwa ni mwezi 11 na kama ilikuwa Ijumaa ni mwezi 2, basi Jumaatatu ya pili itakuwa ni mwezi 12.

1 - Na inasemwa kuwa alifikia kwa Bwana Sa’ad bin Khaythamah, lakini kauli isemayo kuwa alifikia kwa Bwana Kulthum bin Al-Hadm ndiyo iliyothibiti zaidi Tazama Mbarakfuri Al-Rahiiqu Al-Makhtuum uk. 139.

2 - Mji wa Madina kabla ya hapo ulikuwa ukijuilikana kwa jina la Yathrib, lakini baada ya kuja Mtume (s.a.w) hapo ukaitwa Madiinatun Nabii yaani mji wa Mtume (s.a.w).

1 - Kisha unafatia Msikiti wa Baitul Muqaddas uliopo Palestina ambao ndio ulikuwa kibla cha mwanzo cha Waislamu, na huo ndio msikiti wa tatu kwa daraja kubwa. Kisha inafatia misikiti myengine ambayo kidaraja zote ni sawa, hata kama myengine imetandikwa zulia la dola milioni 15 na myengine imetandikwa magunia na vipande vya mikeka.

1 - Bila shaka hisabu hii ni kwa mujibu wa (reti katika) zama za Sheikh Abdallah Saleh Al – Farisi.

1 - Aya yenyewe inasema: (وَالَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَانُكُمْ فَآتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ). Sheikh Abdallah katika maelezo ya tafsiri yake aliiletea Aya hio isemayo:وَالَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَانُكُمْWalladhiina ‘Aqadat Aymaanukumْ” tafsiri mbili kisha akasema: "Au muradi wa tamko hili “Walladhiina ‘Aqadat Aymaanukumْ” ni mke na mume. Na bora kufasiri kwa hivi". Yaani mke anamrithi mume na mume anamritni mke. Cha kufahamu ni kuwa tafsiri zote hizo zipo. Na hii alioitaja hapa ipo pia imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas na Ibn Zaid. Tazama Al-Baghawi Ma'alimu Al-Tanzil j. 1, uk. 610, na Imamu Al-Mufassirin Ibn Jarir Al-Tabari Jami'u Al-Bayan j. 5, uk. 66. Wallahu A’alam.

1 - ...وَأُوْلُوا الأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَى بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ


2 - لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِنْ دِيارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلاً مِنْ اللَّهِ وَرِضْوَاناً وَيَنْصُرُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَئِكَ هُمْ الصَّادِقُونَ

1- وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالإِيمَانَ مِنْ قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْمُفْلِحُونَ

2 - Yaani ni ndugu yangu kwa dini na nasaba.

3 - Yaani atakuwa katika amani sio atasadikika.

1 - وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّهِ فَإِنِ انتَهَوْا فَلا عُدْوَانَ إِلاَّ عَلَى الظَّالِمِينَ

1 - Wanavyuoni wengine wanahisi kuwa tutumie neno Manasara kumaanisha Wakiristo badala ya kutumia neno Masihi kumaanisha watu hao. Na hii ni kwa sababu Masihi ni Nabii Issa naye alikuwa ni Muislamu, wakati hawa ni Makafiri: si Waislamu. Kwa hivyo, hakuna uhusiano wowote ule baina yao na Nabii Issa: wasijinasibishe na yeye bure. Mitume wote (a.s.) wamekuja na dini moja tu ambayo ni Uislamu hata kama kuna baadhi ya tafauti za kimatendo katika Sharia. Ama itikadi na mambo ya misingi yote ni sawa. Anasema Allah akisimulia wasia wa Nabii Ibrahim na Nabii Ya'aqub kwa watoto wao: "Hakika Allah kakuchagulieni dini basi musife ila nanyi ni Waislamu." (Al-Baqarah: 132). Na akasimulia kauli ya Nabii Musa kwa watu wake: akasema: "Na akasema Musa kuwambia watu wake: mukiwa mumemuamini Allah basi mtegemeeni Yeye ikiwa nyinyi ni Waislamu (kweli)." (Yunus: 84). Na akasimulia Habari za Nabii Nuh, akasema: "Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu." Na Nabii Sulaiman naye alipompelekea barua Bilqis alimuandikia: "Msinifanyie kibri na munijie hali ya kuwa ni Waislamu." (Al-Nnaml: 31). Na Aya nyengine tafauti zinaonesha wazi kuwa Mitume wote (a.s.) walikuja na dini moja tu nayo ni ya Uislamu. Bali na adui wa Uislamu, Fir-awn (Laanatu Allahi alaihi) naye pia alipokuwa akizama akadai kuwa naye sasa ni Muislamu: "Mpaka alipofikwa na gharka akasema nimeamini kuwa hakuna mola isipokuwa yule ambaye Wana wa Israili wamemuamini, nami ni katika Waislamu (sasa)." (Yunus: 90).Lakini wakati ulikuwa umekwisha, akaambiwa: "Sasa hivi (ndio unaamini) na umeasi hapo mwanzo na ukawa miongoni mwa waharibifu (katika ardhi)." (Yunus: 91). Kwa hivyo, dini ni moja tangu enzi na enzel (azal), nayo ni Uislamu tu. Na kwa hivyo, ndio Mtume (s.a.w.) akaambiwa na Allah:
شَرَعَ لَكُمْ مِنْ الدِّينِ مَا وَصَّى بِهِ نُوحاً وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ
Yüklə 0,69 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   15




Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2024
rəhbərliyinə müraciət

gir | qeydiyyatdan keç
    Ana səhifə


yükləyin