Maisha ya nabii


(Amekupeni sheria ya dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tuliyokufunulia wewe na tuliyowausia Ibrahim na Mussa na Issa, kwamba simamisheni dini wala msifarikiane kwayo…)



Yüklə 0,69 Mb.
səhifə14/15
tarix10.12.2017
ölçüsü0,69 Mb.
#34382
1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   15

(Amekupeni sheria ya dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tuliyokufunulia wewe na tuliyowausia Ibrahim na Mussa na Issa, kwamba simamisheni dini wala msifarikiane kwayo…). Na ndio maana Allah akasema kwa mfano: كَذَّبَتْ عَادٌ الْمُرْسَلِينَ (Kina 'Ad wamewakadhibisha Mitume), na hali kina 'Ad waliomkadhibisha ni Nabii Hud. Na akasema: كَذَّبَتْ ثَمُودُ الْمُرْسَلِينَ (Kina Thamud wamewakadhibisha Mitume), na hali waliomkadhibisha kina Thamud ni Nabii Saleh na Aya nyingi mfano wa hizi ambazo zimekuja katika mfumo huo. Kuambiwa kwao huko kwamba wamewakadhibisha Mitume, ni kwa sababu, kumkadhibisha Mtume mmoja ni kuwakadhibisha wote. Na hii ni kwa sababu ulinganio wa Mitume wote ni wa dini moja ya Uislamu na itikadi zake na misingi yake. Ama sheria ya baadhi ya matendo inaweza ikabadilika kwa kutafautika umma kama Allah anavyosema: لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنْكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجاً (Kila (Uma) katika nyinyi tumeujaalia sheria yake na njia zake). (Al-Maida 48). Natija ni kuwa Nabii Isa (Masihi bin Maryam) ni Muislamu na sisi ndio tuliomkubali kikweli: si Wakiristo. Kwa hivyo musiwaite wao Masihi kwani Masihi hawatambui wao kamwe kwa uzushi wao huo waliozuwa, bali waiteni Manasara kama Qur-ani inavyowaita.

1 - وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلا تَعْتَدُوا إِنَّ اللَّهَ لا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ


2 - وَلا تُقَاتِلُوهُمْ عِنْدَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّى يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ فَإِنْ قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ كَذَلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ


3- وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّهِ فَإِنِ انتَهَوْا فَلا عُدْوَانَ إِلاَّ عَلَى الظَّالِمِينَ


4- لا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ


5 - -فَإِنْ اعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَاتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا إِلَيْكُمْ السَّلَمَ فَمَا جَعَلَ اللَّهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلاً


6 - وَإِنْ جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ


2 -  أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّهَ عَلَى نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ



3 -  الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِنْ دِيَارِهِمْ بِغَيْرِ حَقٍّ إِلاَّ أَنْ يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّهُ...


4 - لا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ


1 - ادْعُ إِلَى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ وَجَادِلْهُمْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

2 - وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ



1 - Wasimbakishe.

1 - فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ قَتَلَهُمْ

2 - Baadhi ya watu huitumia Hadithi hii kwa kumpa mawaidha maiti wakati wa kuzikwa, na kwa hivyo utawaona wanamwambia maiti kuwa: “Ukiulizwa Mola wako nani, sema Allah; Mtume wako nani, sema Muhammad; Kitabu chako gani, sema Qur-an…” na mfano wa hayo. Lakini watu hawa hawakujikalifisha na kuitupia macho Qurani, kwani kama anavyosema Allah katika Surat Yasin Aya ya 70 kuwa Qur-an unaweza kumuonya kwayo yule aliyehai na akaonyeka: sio mfu. Basi ndipo akasema vile vile kumsikilizisha maiti mawaidha hakumfai kitu, pale aliposema katika Suratl Naml Aya ya 80 na Surat Rum Aya ya 52 kuwa: إِنَّكَ لا تُسْمِعُ الْمَوْتَى...(Kwa hakika huwezi kuwasikilizisha wafu (mwito wako)…). Na Aya 22 Surat Fatir isemayo:  وَمَا أَنْتَ بِمُسْمِعٍ مَنْ فِي الْقُبُورِ (…Na wewe huwezi kuwasikilizisha waliomo makaburini). Ingawa Aya hizi si maandiko ya wazi katika maudhui hii, lakini ndani yake kuna dalili kwamba maiti hafaliwi tena na wito wowote ule, inayomfaa ni: amali yake ndio msingi, kisha dua za Waislamu, au sadakat jariya kama kaiwacha ikiwemo elimu inayowafaa watu. Na hivi ndivyo Mtume (s.a.w.) alivyofundisha.



1 - Akauliwa na Hamza bin Abdul Muttalib kwa dharuba ya upanga iliyoanzia begani mpaka kitovuni.

2 - Akauliwa na Saad bin Abi Waqqas kwa mshare uliozama kwenye koo yake na akafa ulimi nje, na inasemekana pia aliuliwa na Ali bin Abi Talib kwa upanga.

1 - Akauliwa na Aasim bin Thabit kwa mshare.

2 - Akauliwa na Zubayr bin ‘Awaam.

3 -Akauliwa kwa kuchomwa upanga na Talha bin Abdillah, na inasemekana aliuliwa kwa mshare na Aasim bin Thabit.

1 - Pakawa kimya.

1 - وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُمْ بِهِ وَلَئِنْ صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِلصَّابِرِينَ (126)

2- وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلاَّ بِاللَّهِ وَلا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلا تَكُ فِي ضَيْقٍ مِمَّا يَمْكُرُونَ (127)

1 - Wanauzunguka kwa kuuzingira.

1 - Kutuhadaa.

2 - Kila anayetii amri yangu.

1 - يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَاءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحاً وَجُنُوداً لَمْ تَرَوْهَا وَكَانَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيراً (9) إِذْ جَاءُوكُمْ مِنْ فَوْقِكُمْ وَمِنْ أَسْفَلَ مِنْكُمْ وَإِذْ زَاغَتِ الأَبْصَارُ وَبَلَغَتِ الْقُلُوبُ الْحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِاللَّهِ الظُّنُونَ (10) هُنَالِكَ ابْتُلِيَ الْمُؤْمِنُونَ وَزُلْزِلُوا زِلْزَالاً شَدِيداً (11)

1 - Lafdhi ya Aya inafasirika: "Kwa hakika Allah amekunusuruni ….." badala ya maneno tumekunusuruni. Inaonesha Sheikh kafasiri kimaana tu badala ya kufasiri kwa mujibu wa lafdhi, vivyo hivyo kafanya katika baadhi ya Aya nyengine.

1 - لَقَدْ نَصَرَكُمْ اللَّهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنْكُمْ شَيْئاً وَضَاقَتْ عَلَيْكُمْ الأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُمْ مُدْبِرِينَ (25) ثُمَّ أَنزَلَ اللَّهُ سَكِينَتَهُ عَلَى رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُوداً لَمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَذَلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ (26) ثُمَّ يَتُوبُ اللَّهُ مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ عَلَى مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (27)

1 - Yaani kabla ya hapo Mtume (s.a.w.) na Waislamu walikuwa wakisali lakini si Sala tano. Na mwaka wa 12 wa Kiislamu anaoukusudia Sheikh hapa si mwaka wa 12 wa Hijria, bali kakusudia mwaka wa 12 wa Utume.

2- Hii ni kauli moja ya wanavyuoni kwamba Zaka imefaradhishwa katika mwaka wa pili wa Hijra; nao wenye kauli hii wanakusudia kusema kuwa Zaka imefaradhishwa Madina yaani baada ya Mtume (s.a.w) kuhama Makka. Na wanavyuoni wengine wanaona kinyume na hivyo. Alipoulizwa ni wakati gani imefaradhishwa Zaka, Sheikh Ahmad bin Hamad Al-Khalili, Mufti Mkuu wa Oman, alisema: "Kilichosahihi ni kuwa Zaka imefaradhishwa kiujumla tangu Makka, na dalili ya haya ni Aya zenye kuonyesha hivyo ambazo zimeshuka Makka, kama kauli ya Allah katika Surat Al-Muzzammil Aya 20: (Na simamisheni sala na toeni zaka…) Nayo ni miongoni mwa Sura za mwanzo kushushwa. Ama yanayosemwa kuwa Aya hii imeshuka Madina si sahihi, kwa sababu ingelikua imeshuka Madina basi isingelikuwa sehemu hii tu ni ya Madina bali ingelikuwa Aya nzima, kwani inafahamika kuwa sehemu ya mwazo ya Aya hii ni Nasikh (yaani hii kauli ya Simamisheni sala ni yenye kufuta hukumu) ya yale yaliokuwa yamefaradhishwa hapo kabla katika mwanzo wa Sura hii ambayo ni kusimama usiku kwa muda mrefu, na haya yote yalikuwa Makka, kwa hivyo hii ni dalili ya wazi kuwa Aya hii ni ya Makka. Na miongoni mwa dalili ni kauli ya Allah katika Surat Al-Ma'aarij Aya 24: (Na ambao katika mali zao kuna sehemu maalum) na hii ni dalili vile vile kwani imeterermka Makka. Na kauli ya Allah katika Suratul Muminun ambayo imeteremka Makka vile vile Alla anasema katika Aya ya 4: (Na ambao wanaitekeleza zaka). Na kauli ya Allah katika Surat Fussilat ambayo imeteremka Makka anasema Allah katika Aya 7: (Amabo hawatoi zaka na wanaikanusha Akhera). Ama katika Surat An-Nisaa kauli ya Allah Aya 77 isemayo: (Je huwaoni wale walioambiwa: Izuieni mikono yenu (msipigane na makafiri mpaka muamrishwe). Na (sasa) simamisheni Sala na toeni zaka…) ingawa Aya hii ni ya Madina lakini inaeleza hali ya Makka ilivyokuwa, kwani Waumini waliambiwa waizuie mikono yao huko Makka (wasipigane) na hapo ndipo wakaambiwa simamisheni Sala na toeni zaka, na wakafaradhishiwa Jihadi baada ya kuhamia Madina na wala hawakuamrishwa tena hapo kuizuia mikono yao, na hii inaonesha kuwa zaka ilikuwa imefaradhishwa lakini waliachiwa matajiri wenyewe ikawa kila mmoja hutekeleza wajibu huo wa mali yake kwa kadiri ya kukidhi haja ya mafakiri kwa kadiri ya uwezo wake. Na mambo yalipotulia Madina Allah akateremsha hukumu za zaka kwa urefu na zikaendelea kama zilivyo. Ama kufaradhishwa kiujumla ilikuwa tokea Makka.. (Fatawa Az-zakaa uk 235) Mwisho wa kunukuu.
Tunasema: Wenye kauli hio ya pili wanakusudia kusema kuwa Zaka ilifaradhishwa Makka kiujumla tu (yaani bila kufafanuliwa kiwango gani na kwa muda gani) kama Aya tulizozinukuu zinavyoonesha. Ama huko Madina katika mwaka wa 2 wa Hijra, kilichofanyika ni kufafanuliwa kwa Zaka kwa kuwekewa kiwango chake na kwa kuwekewa muda wake. Hii ina maana kuwa Zaka iliofaradhishwa mwanzo huko Makka ilikuwa ni bila kiwango maalumu na bila ya kupitiwa na wakati maalum – ukipata unawajibika kutoa chochote. Na hii ndio asili ya kuchanganyisha baina ya kufaradhishwa kwake na kufafanuliwa kwake – kufaradhishwa ilikuwa Makka na kufafanuliwa ilikuwa Madina.

3- Makusudio ya kuutaja Mfunguo mosi na Mfunguo pili kuwa ni miezi ya Hija , si kwamba watu wanakwenda kuhiji katika miezi hii bali imekusudiwa kuwa ni miezi ya kuhirimia Hija. Ama mwezi wa kuhiji hija kubwa ni Mfunguo tatu tu. Ama Umra hutekelezwa katika mwezi wowote, isipokuwa mwezi wenyewe wa Hija ndio kuna khilafu kwa Wanavyuoni: je inafaa kufanya Umra isio tamatu'u wala qiran au vipi au je inamjuzia kwa asiyefanya Hija kufanya Umra katika miezi ya Hija? Halkadhalika kuna khilafu juu ya Ayami Ttashriq inajuzu kufanya Umra kwa asiyefanya Hija? Rejea Yahya Muhammad Bakush Fiq-hi Al-Imami Jabir bin Zaid uk. 322-323.

1 - لَقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةًِ (18)

1 - Kuhusu kadhia hii, wale wanaompinga Sayyidna 'Umar bin Al-Khattab (r.a.) wanalichukulia suala hili la Umar kukataa baadhi ya masharti hayo yaliomo katika mkataba huo kuwa ni kupinga amri ya Mtume (s.a.w.), na kuna ziada nyingi zinazosimuliwa na wao ili kuonesha kuwa Umar ni mbaya, na masimulizi ya aina hii yanayosimuliwa na wao dhidi ya Umar na Abu Bakr ni mengi sana kwao, na wameacha ukweli kuwa haya yalikuwa ni mashauriano tu juu ya kadhia hiyo baina ya Mtume (s.a.w.) na Mashaba wake, na wala hilo halikuwa geni kwao, kwani Mtume (s.a.w.) alikuwa akiwashauri mambo mengi na kutaka rai zao, ambapo huwasikiliza kisha hufuata lenye maslahi kwao. Na vipi Mtume (s.a.w.) asiwashauri Masahaba wake ilhali Allah anamuongoza kwa kumwambia: "Na shauriana nao katika mambo." Al-Imran Aya 159. Na kushauriana nao kwenyewe ni katika mambo ya kidunia: si yale anayopewa wahyi. Katika vita vya Khandaq, Mtume (s.a.w.) alizungumza na wakuu wa kabila la Bani Ghatafan waliokuwa wameuzingira mji wa Madina, na Mtume (s.a.w.) akawataka warejee makwao na atawapa 1/3 ya mavuno ya tende za Madina ya mwaka huo. Baada ya mjadala mrefu, wale wakubwa wa Bani Ghatafan walikubali rai ile ya kwenda zao na jeshi lao la watu 6,000. Lakini kabla hawajaondoka wakuu hawa na shauri hii kuwapelekea wenziwao, Mtume (s.a.w.) aliwaita wakuu wa Kiansar kusikiliza nini rai yao katika sulhu hiyo, lakini jawabu ya Ansar ilikuwa kinyume na matakwa ya Mtume (s.a.w.), kwani walisema: “Ikiwa hii si amri ya Allah wala si amri yako, bali ni jambo unalolifanya kwa ajili yetu sisi Ansar tu, basi sisi hatupendi hata kidogo…. – Hawa jirani zetu Bani Ghatafan – hawajapata kutushinda wakala tende zetu ngawira siku za ujahili, watatushinda wale tende zetu ngawira leo, na hali wewe upamoja nasi? Wape habari, Ya Rasula Llah! Kuwa hapana baina yetu na wao ila upanga tu – huo ndio utakaobainisha haki”. Lakini ukitaka kupotoa maudhui hii na kuwafanya Ansari wamepinga amri ya Mtume (s.a.w.) unaweza ukatunga maneno mazuri ya kuwashawishi watu, na kuwafanya Ansar kuwa ni wabaya juu ya hili, na hali si hivyo bali mambo yalikuwa ni kushauriana si chengine. Na mifano juu ya maudhui kama hizi ni mingi mno. Bali Allah aliposema kuwa anataka kuumba Khalifa katika ardhi, Malaika walijadili juu ya hili (Suratul Baqara Aya ya 30 – 33). Lakini ukitaka kuipotoa maudhi hii unaweza kuwalingania watu na ukasema: "E jamani nyi! Watizameni Malaika hawa jinsi wanavyoijadili amari ya Mola wao! Allah anasema kuwa anataka kuleta Msimamizi katika ardhi wao wanajadili, Aah! Watamwaga damu, watafanya ufisadi sijui hivi na hivi. Je Allah hajui hilo hata wakajifanya wao wanajua kuliko Allah" na maneno zaidi ya hayo unaweza kuyaleta na kuonesha kwamba hawa Malaika wamekosea. Na hali mambo hayako hivyo. Pia Nabii Mussa alipotumwa kwa Firauna alisema anaogopa watamua na kwamba hana ufasaha kuliko ndugu yake Haruna "Basi nipeleke pamoja naye." Ukitaka kuipotoa Maudhui utasema: "Basi Mussa anamfundisha Allah kwani Yeye hajui kwamba Haruna ni mfasaha zaidi." Na yako mengi. Kwa hivyo, ndugu zetu hawa wasipotoshe ukweli kwa kutaka kumfanya Umar kapinga amri ya Mtume (s.a.w.), kwani kadhia ilikuwa ni mashauriano baina yao na kila mmoja alikuwa na rai tofauti na mwenziwe. Na ilipokatwa shauri juu ya jambo hilo, hapakuwpo na aliyekuwa na haki ya kukataa hata huyo Umar mwenyewe. Au tuseme – ikiwa tutachukua mantiki yao hio – kuwa Ali naye kamuasi Mtume (s.a.w.) pale alipomuamuru kuwa alifute jina la Utume katika Sulhu ya Hudaibiya naye akakataa: je na Ali ni asi anampinga Mtume (s.a.w.)?!

1 - Aya yenyewe ni hii: إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحاً مُبِيناً (Bila shaka tumekwisha kupa ushindi uliodhahiri ) .

1 - Historia.


1 - Maneno kishindo kikubwa” hapa hayakukusudii kwamba walitumia nguvu, bali anakusudia kusema kuwa walisilimu kwa shangwe kubwa.

2 - Miongoni mwa waliofatana naye ni Ja'afar bin Khutham Al-'Itki, Abu Sufra Sarif bin Dhalim na kundi la Azdi. Al-Salimi Tuhfatu Al-A'ayaan j. 1, uk. 12.

3 - Kumkirimu mgeni ni sifa ambayo ndugu zetu wa Omani wamepambika nayo zaidi kuliko watu wengi, na kwa ajili hiyo Waomani wakasifiwa sana na Sayyidna Abu Bakr kwa ukarimu wao. Kapokea Al-Imam Ahmad bin Hanbal na Al-Imamu Muslim kuwa Mtume (s.a.w) alimwambia Sahaba wake baada ya kumtuma kwenda kulingania kwa watu na wakamkadhibisha na wakampiga, basi alimwambia:"لَوْ أَهْلَ عُمَانَ أتَيْتَ، مَا ضَرَبُوْكَ وَمَا سَبُّوْكَ" (Lau ungaliwaendea watu wa Omani, basi wasingalikupiga wala wasingalikutukana). Na haya yote ni kuonesha ukarimu wao na upole wao. Bali Waomani walipokwenda kwa Abu Bakr na kumpelekea Zaka baada ya kufa Mtume (s.a.w.), walimwambia: "Ewe Khalifa wa Mtume (s.a.w.), na Enyi Makuraish! Hii amana iliokuwa mikononi mwetu na katika dhimma yetu: amana ya Mtume (s.a.w.)". Abu Bakr akawasifu sana, na siku ya pili akahutubia na kuendelea kuwasifu na kuwaombea dua na akawambia: "Enyi watu wa Oman! Mumesilimu kwa khiari yenu, Mtume (s.a.w.) hakuigusa ardhi yenu kwa kwato (za jeshi la ngamia) wala kwato (za jeshi la farasi). Wala hamukumpa tabu kama walivyompa tabu Warabu wengine…kisha akamtuma kwenu Amru bin Al-'Aas bila jeshi nanyi mukamkubali..na kumtii..basi kuna fadhila gani ilio bora kuliko hii na kuna kitendo gani kilichokitukufu kuliko kitendo chenu?! Inakutosheni kauli ya Mtume (s.a.w.) kuwa utukufu kwenu hadi siku ya kiama". Al-Salimi Tuhfatu Al-A'ayaan j. 1, uk. 12-13.


1 - Allah anasema: قُلْ لِلَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُمْ مَا قَدْ سَلَفَ(Wambie wale waliokufuru kama wataacha (yale mabaya waliokuwa nayo) watasamehewa yaliopita). Anfal Aya ya 38. Na Mtume (s.a.w.) anasema: "الإسلام جب لما سبق" (Uislamu unakata yote yaliopita).

1 - Na upasue ndani yake mito yenye kububujika (maji)

2 - وَقَالُوا لَنْ نُؤْمِنَ لَكَ حَتَّى تَفْجُرَ لَنَا مِنْ الأَرْضِ يَنْبُوعاً (90) أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِنْ نَخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ الأَنهَارَ خِلالَهَا تَفْجِيراً (91) أَوْ تُسْقِطَ السَّمَاءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفاً أَوْ تَأْتِيَ بِاللَّهِ وَالْمَلائِكَةِ قَبِيلاً (92) أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِنْ زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَى فِي السَّمَاءِ وَلَنْ نُؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّى تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَاباً نَقْرَؤُه قُلْ سُبْحَانَ رَبِّي هَلْ كُنتُ إِلاَّ بَشَراً رَسُولاً (93)

1 - Mataifa.

2 - يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوباً وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ

3 - قَالَ لا تَثْرِيبَ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ يَغْفِرُ اللَّهُ لَكُمْ ........... . (92) Surat Yusuf Aya

1- Wamepokea Imam Bukhari na Muslim Riwaya isemayo:

"عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَتْ هِنْدُ امْرَأَةُ أبِيْ سُفْيَانَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: إنَّ أبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ شَحِيْحٌ وَلَيْسَ يُعْطِيْنِيْ مَا يَكْفِيْنِيْ وَوَلَدِيْ إلاَّ مَا أَخَذْتُ مِنْهُ وَهُوَ لاَ يَعْلَمُ، قَالَ: خُذِيْ مَا يَكْفِيْكِ وَوَلَدكِ بِالْمَعْرُوْفِ"

"Kutoka kwa Aysha (r.a) kasema: kasema Hind mke wa Abu Sufyan kumwambia Mtume (s.a.w): Hakika Abu Sufyan ni mwanamme bakhili, na wala hanipi chenye kunitosha mimi na mwanangu, isipokuwa kile ninachochukua kwake pasina yeye kujua, akasema (Mtume s.a.w): 'Chukua chenye kukutosha wewe na mwanao kwa wema (kadiri ya haja)".



2 - Bali yote alioyakataza Mtume (s.a.w.) hapa yalikuwa yakitendeka kama Qur-ani, Hadithi na historia zinavyonena kwa uwazi.

1 - Tazama jinsi tabia njema zinavyozaa matunda mazuri!

2 - Bila shaka hisabu hii ni kwa mujibu wa reti katika zama za Sheikh Abdallah Saleh Al–Farisi, ama kwa sasa ni tofauti na hivyo. Lakini Sheikh alipokuwa akizungumzia kuhusu "Kuja Madina watu wa Mtume (s.a.w.) na wa Sayyidna Abubakr" alisema kuwa "Dirham 500 ni kiasi cha shilingi 250". Kwa hivyo utakapotazama hesabu hii ya dirham 500 ambazo ni kiasi cha shilingi 250 utona kuwa dirham moja ni sawa na senti 50 (nusu shilingi), ambapo hapa katika hesabu hii ya dirham 354 kasema kuwa kila dirham ni sawa na senti 60. Kwa hivyo, kama hili si kosa la chapa, basi dhahir ni kuwa Sheikh kafanya makadirio tu (rough figure).


1 - Nayo ni kusema: ( لبّيك اللهم لبّيك ، لبّيك لا شريك لك لبّيك ، إن الحمد والنعمة لك والملك لا شريك لك ) (Labbayka llahumma labbayka, labbayka laa shariika laka labbayka, inna lhamda wa nni’imata laka wal mulk laa shariika laka).

1 - Kusai ni kwenda baina ya majabali mawili la Safa na Marwa, mara saba.

2 - Madhehebu ya Kishia hawakuipa uzito Hadithi hii kwani wanaona kuwa inapingana na Riwaya walioikubali wao iliyokinyume na hiyo. Riwaya yao wanayoitegemea inasema: “Nimekuachieni vizito viwili mkishikamana navyo hamtapotea milele. Kitabu cha Allah na watu wa nyumba yangu (Ahlu Bayti)”. Bila shaka kushikamana na wacha Mungu ni jambo lisilokatalika, ama kuwafanya wao kuwani marejeo ya pili baada Qur-ani hili ndilo lenye mushkila, kwani Allah anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُوْلِي الأَمْرِ مِنْكُمْ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِنْ كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً


(Enyi mlioamini! Mtiini Allah na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu katika nyinyi. Na kama mukikhitilafiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Allah na Mtume, ikiwa mnamwamini Allah na siku ya mwisho, hiyo ndiyo kheri na matokeo bora kabisa). Surat Al-Nisaa Aya 59. Na hakuna shaka kwamba maana ya kurudi kwa Allah ni kuitazama Qur-ani inavyosema, na kurudi kwa Mtume (s.a.w.) ni kutazama Hadithi zake zinasema nini: si Ahlu Bayti wanasema nini. Maelezo kwa urefu juu ya maudhui hii ni katika Mezani Ya Haki cha Al-Akh Juma Mazrui.



1 - الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلامَ دِيناً فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لإِثْمٍ فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (3)


2 - Baadhi ya maneno tumeweza kudiriki kuwa ni makosa ya chapa kwa hivyo tumeweza kuyarekebisha, lakini kwa vile neno hili hatukuweza kujua makusudio yake ni nini: je ni kosa la chapa au ni neno katika lugha ya Kiswahili, kwa hivyo tumeamua kuliwacha kama lilivyo. Hususan tukizingatia ukweli kwamba Mtunzi wa kitabu hiki ni katika watu waliosifika sana kwa ufasaha wa Kiswahili.

1 - Dhahir ni kuwa neno "Anajida" ni kosa la spelingi la neno "Anajidai? Lakini ni dhahir pia kwamba Sheikh hawezi kutumia lugha hii dhidi ya Bibi Aysha kwamba alikuwa anajidai kuwa anaumwa na kichwa. Bali ni wazi kuwa neno "Anajida" Sheikh kalichukua katika riwaya yenyewe inayozungumzia kisa hiki ambapo ndani yake Bibi Aysha kasema: "وَأنا أجِدُ صُدَاعًا فِي ْرَأسِيْ" Wa Ana Ajidu Suda'an Fii Ra-asi (Nami nina maumivu ya kichwa). Tazama Ibn Majah Al-Sunan Hadithi na. 1465. Kwa hivyo, baada ya Sheikh kutumia maneno "Nina maumivu" katumia maneno "Anajida kuwa kashikwa na kichwa". Inaonesha neno "Anajida" ndio lile Ajidu lililo katika Hadithi. Wallahu A'alam.


1 - Bwana mmoja wa huko kwetu Afrika Mashariki siku moja aliielezea sehemu hii ya kufa kwa Mtume (s.a.w.). Aliponukuu maneno hayo ya Sayyidna Umar, Bwana huyo alisema: “Umar anakusudia kwamba Ali na Abbas ni wanafiki”. Lakini kila mwenye akili anadiriki kwamba huku ni kutaka kukuzisha mambo tu: si jengine, kwani ukweli ni kuwa kifo cha Mtume (s.a.w.) kiliwafadhaisha wengi, nyoyo na nafsi zilibabaika, watu wasijue nini wanafanya; wasijue nini wanakisema: mtafaruku mkubwa ulikuwa katika nafsi za Masahaba kila mmoja kapigwa na bumbuwazi, kaduwaa, wakaanguka walioanguka, miili ikawapooza na wengine wakaiaga dunia papo hapo. Kwa hivyo, ikiwa imethibiti kuwa Sayyidna Umar alitamka neno hilo basi haikuwa kamwe akiitakidi kuwa Ali na Abbas ni wanafiki. Haashahu! Vipi aitakidi hivyo, halafu:

1) Papo hapo – baadae – akubali kuwa Mtume (s.a.w.) kafa? Hili linaonesha wazi kuwa hakuyasema hayo ila kwa kufadhaika: si kwa kuyaitakidi.

2) Vipi Umar amuone Ali kuwa ni mnafiki halafu amfanye mmoja wa watu sita wa kuchaguliwa kwa ukhalifa baada yake?!

Bali tunaona kwamba mfazaiko wa aina hii pia tunaona kwamba ulimkumba hata Bibi Fatma, kama alivyosimulia Imam Bukhari kwamba alipozikwa Mtume (s.a.w) alisema Fatma: “Vipi zimekupelekeeni nafsi zenu hata mukaufukia mwili wa Mjumbe wa Allah katika dongo?” Lakini ukiwa unamchukia Bibi Fatma na ukataka kupotoa ukweli na kukuzisha jambo hili unaweza kusema kuwa: “Mtizameni huyu Fatuma! Hivyo yeye hajui kuwa hivi ndivyo Uislamu ulivyofundisha?! Hivyo hajui huyu Fatuma kwamba Allah kasema:


Yüklə 0,69 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   15




Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2024
rəhbərliyinə müraciət

gir | qeydiyyatdan keç
    Ana səhifə


yükləyin