(Katika hii ardhi tumekuumbeni na humo tutakurudisheni na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine??!!) (Taha - 55).
Au hajui kuwa Allah kasema: (Je hatukuifanya ardhi kuwa ni yenye kukushanya (viumbe) * Vilivyohai na wafu) (Al-Mursalat 25-26). Je hajui kuwa kauli ya Allah isemayo :
(Allah akamletea kunguru anayefukua ardhini ili amwonyeshe jinsi ya kuificha (kuizika) maiti ya nduguye) (Maida – 31); hajui yeye kuwa Aya hizi ni dalili ya mafundisho ya kuzikwa baada ya kufa? Je yeye hajui kuwa haya ni mafundisho aliyokuja nayo Mtume (s.a.w.)?!” Na unaweza kusema mengi kuliko haya ya kumfanya yeye kuwa hana analolijua na hali ya kuwa mambo hayakuwa hivyo, bali ni kule kufazaika kwake kwa kifo cha Baba yake Mpenzi, Rasulu Allah (s.a.w.). Na ndio maana baada ya Sayyidna Abu Bakr kuwasomea watu kauli ya Allah isemayo:
(Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume tu. Wamepita kabla yake Mitume (mingi) akifa au akiuawa ndio mtarudi nyuma kwa visigino vyenu (muwe makafiri) na atakayerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru Allah chochote. Na Allah atawalipa wanaoshukuru), kasema Ibnu Abbas kuwa:
وَاللهِ لَكَأنَّ النَاسَ لَمْ يَعْلَمُوْا أنَّ اللهَ أنْزَلَ هَذِهِ الآيَةَ حَتَّى تَلاَهَا أبُوْ بَكر
(Wallah kana kwamba watu walikuwa hawajui kuwa Allah kateremsha Aya hii ila baada ya kuisoma Abu Bakr).