“Your name is?” (Jina lako ni nani?)
“I’m Marione!” (Naitwa Marione)
“You are beautiful Marione, can we talk privately?”
“No I’m busy! Thanks for your complements” (Hapana nina kazi nyingi sana! Ila nashukuru sana kwa sifa zako)
“What about tomorrow?” (Vipi kesho?)
“I’m not sure either?” (Sina uhakika pia).
Walishamtilia mashaka tayari, ni jina tu ndilo lilikuwa tofauti lakini sura ilikuwa ili ile! Kama ni yeye walikuwa na uhakika wa kupata zawadi kubwa sana kutoka kwa Dk. Ian! Hicho ndicho walichonong’onezana vijana hao kabla ya kumwita Caroline! Walipanga kujaribu kumtaka urafiki ili tu wapate picha yake nakuituma Canada, kama angethibitishwa kuwa ndiye yeye basi wamkamate na kumsafirisha.
“Ningependa sana kupiga picha na wewe?”
“Mimi?”
“Hapana, sipendi kupiga picha!” Caroline alikataa lakini kwa mama mwenye mgahawa hilo halikuwa na kizuizi sababu mteja alikuwa mfalme! Caroline alilazimishwa kufanya hivyo, ingawa hakutaka ilibidi akubali na picha ikapigwa.
Walipotoka hotelini hapo vijana hao bila kuchelewa walikwenda kwenye kompyuta na kuzituma picha hizo kwa Dk. Ian huko huko Canada kwa nje ya barua pepe, jibu lilifuata dakika chache baadae lilikuwa:
“ She is the one, once you bring her here, you are rich!” (Ni yeye mara mkimfikisha hapa nyie matajiri!) Alisoma barua pepe hiyo, vijana hao walichanganyakiwa walichanganyikwa kupita kiasi, ilikuwa ni lazima wamfikishe Caroline, Canada haraka iwezekanavyo hawakutaka kutumia nguvu!
“Njia pekee ni kujifanya unamtaka kimapenzi, ipo siku atakubali na siku tutakayotoka nae kwenda popote kustarehe ndiyo siku tutakayomlewesha kwa madawa na kumsafirisha hadi Canada au?”
“Sawa kabisa, hiyo ndiyo njia sahihi!” Wote waliitikia.
Je, nini kitampata Caroline? Je, kweli atafika Tanzania? Wiki ijayo.
“Lakini lazima tufahamu ni kiasi gani Dk. Ian atatulipa, tusijejikuta tukifanya kazi halafu malipo yakawa kidogo, kumbukeni kumsafirisha kutoka hapa hadi Canada ni lazima tutumie ndege ya kukodi hivyo ni vyema tufahamu ni kiasi gani tutalipwa ili tupange bajeti yetu vizuri!”
“Kwa hiyo?” Aliuliza mmoja wao.
“Inabidi tumpigie simu Dk. Ian kuuliza juu ya jambo hili!”
“Tufanye lini?”
“Leo hii hii, hakuna sababu ya kuchelewa!”
Baada ya maongezi yao wote walitoka haraka na kwenda moja kwa moja hadi mjini kwenye kituo cha kupigia simu ambako walitafuta namba ya Dk. Ian katika vitabu vya simu na kufanikiwa kuipata! Hawakutaka kupoteza muda, waliipiga moja kwa moja bila kusita.
“Hallow, Dr. Ian’s office can I help you? (Hallo hapa ni ofisi ya Dk. Ian, naweza kukusaidia?)
“Can I speak to Dr. Ian himself?” ( Je, naweza kuongea na Dk. Ian mwenyewe?)
“Can I know your name and the place you are calling from sir?” (Naweza kujua jina lako na unapiga simu kutoka wapi bwana?)
“My name is O’brien, calling from Cambodia!” ( Ninaitwa O’brien napiga kutoka Cambodia)
“Hold on.. (Subiri), ilisema sauti hiyo na baadae sauti nzito ilisikika.
“Hallow, Dr. Ian speaking!” (Dk. Ian anaongea!)
“Naitwa O’brien mmoja wa watu uliowasiliana nao kwa barua pepe juu ya Caroline! Unakumbuka?”
“Ndiyo nakumbuka sasa kwanini hamjafika naye hapa?”
“Ni kwa sababu hatujafahamu ni kiasi gani utatulipa kwa kazi hiyo hatari!”
“Unataka ulipwe kiasi gani?”
“Chochote lakini kiwe kiasi kikubwa!”
“ Sawa, nitawalipa dola millioni mbili”
“Hakika?”
“Huwa sidanganyi”
“Tumemaliza, tupe wiki mbili au tatu Calorine atakuwa mikononi mwako”
“Kupitia akaunti gani ya benki niwalipe tangulizo la dola laki tano?”
“Namba 01J200601293, benki ya Uingereza tawi la Trivial”
Baada ya maongezi hayo simu ikakatwa, Kennedy aliruka juu na kushangilia, wenzake wote walimfuata kutaka kujua alichoongea na Dk. Ian, aliwasimulia kila kitu na alipofika mwisho wa maelezo yake wote walikumbatiana kwa pamoja na kujikuta wakitamka neno “Kwa heri unga na kwa heri madawa!” Kwa pesa waliokuwa wameahidiwa walikuwa na uhakika wa kuacha biashara ya unga na bado wakaendelea kuishi.
Saa moja na nusu baadae walipiga simu ofisi za benki ya Uingereza na kuuliza kama kweli pesa iliingia. Hawakuamini masikio yao walipopewa jibu kuwa dola 500,000 tayari zilishaingia katika akaunti yao, kazi pekee iliyokuwa mbele yao ni kumteka Caroline na kumfikisha Canada ndipo wangemaliziwa sehemu ya pesa iliyobaki.
“Kazi hii ni rahisi mno kama tulivyopanga jana, tunachotakiwa kufanya ni kucheza karata yetu vizuri bila kugundulika, hatakiwi kabisa kuelewa kuwa sisi tumeshafahamu! Cha kufanya hapa wewe Kennedy kwa sura yako ilivyo nzuri tunakupa kazi ya kumfuatilia huyu mtoto, hakikisha unajenga nae urafiki wa ghafla na awe mpenzi wako! Akikubali tu kuwa na wewe na kuwa anatoka naye kwenda sehemu mbalimbali usiku au hata mchana itakuwa rahisi sana sisi kumteka na kumpeleka hadi Canada kwa ndege ya kukodi!”
“Lakini jambo hili haliwezi kuwa la haraka kiasi hicho, linahitaji muda zaidi!”
“Ndiyo maana tumempa Dk. Ian wiki mbili, wewe fanya usanii wote uuwezao hakikisha mtoto anakubali!”
“Ok, nitajaribu lakini itabidi mnikabidhi fungu la kutosha kutanua naye ili iwe rahisi kumuingiza kingi”
“Hiyo haina shida, kwa kuanzia kamata kwanza dola mia tano!” Nicky kiongozi wa kundi hilo alimkabidhi Kennedy pesa, kwa kitendo hicho operesheni ya kumteka Caroline ilikuwa imeanzishwa rasmi!
“Hatuhitaji kumsafirisha kwa ndege, ya nini gharama yote hiyo? Huyu ni wa kumlewesha madawa tu kisha tunatafuta cheti cha daktari kuwa ni mgonjwa wetu tunamsafirisha kumrudisha nyumbani Canada kutoka hapa Cambodia, basi! Hiyo itapunguza gharama kidogo, ndege ya kukodi itatugharimu pesa nyingi tutapunguza pesa zetu bure!” alisema O’brien kijana mdogo kuliko katika kundi lao lililoitwa Three some squad”
Lilikuwa ni kundi la vijana wenye vipaji vya kuimba na kupiga muziki walisafiri sehemu mbalimbali duniani wakifanya maonyesho lakini mara nyingi walisafiri sana kati ya Pakstan na Cambodia! Kwa kofia ya uanamuziki walifanya biashara ya madawa ya kulevya bila kugundulika. Kennedy ndiye kijana pekee aliyekuwa na damu mchanganyiko wa Mwafrika na Mzungu katika kundi hilo, O’brien na Nicky walikuwa Wazungu! Mchanganyiko wa rangi ulimfanya Kennedy kumvutia karibu kila msichana aliyemwona kwa kumtumia yeye walijua ni lazima tu Caroline angenasa!
*************
Jioni ya siku hiyo walikuwa ndani ya mgahawa wa mama Suzane ambao Caroline alifanya kazi, walikaa kwenye meza ya pembeni kabisa na muda mfupi msichana mfupi aliwafuata ili awahudumie walimkataa na kuomba waitiwe Marione, jina ambalo Caroline alilitumia.
“Sorry, don’t lake it badly and accept our demand! (Samahani, usituelewe vibaya na tafadhali kubali takwa letu!)
“Worry not, let me call her for you, a customer is always a king!” (Msiwe na wasiwasi acheni niwaitie, mteja siku zote ni mfalme) Mhudumu alisema huku akiondoka na dakika mbili tu baadae Caroline alionekana akitembea kuelekea mezani, alipofika aliwasalimia watu wote kwa kuwashika mikono, wote walimwangalia kwa macho ya tamaa! Kwao tayari Caroline alikuwa pesa! Uhai wake ulikuwa mali lakini yeye hakulifahamu hilo.
“Why are you looking at me like that?” (Kwanini mnaniangalia namna hiyo?) Macho yao yalimtisha Caroline ilibidi aulize.
“Uzuri wako! Wewe ni mzuri sana! Ni mwanamke wa kiafrika haswa! Tena hakuna mwingine kama wewe katika Cambodia!
Badala ya kusema kitu chochote Caroline alitabasamu aliyachukulia maneno hayo kama utani, ilikuwa ni miaka mingi sana tangu aambiwe ni mzuri kwa mara ya mwisho! Mtu pekee aliyemwambia hivyo hakuwa mwingine bali Dk. Ian! Kipindi hicho alikuwa msichana mrembo kweli kweli, kwa hali aliyokuwa nayo mahali pale aliamini aliyoambiwa yalikuwa utani.
“What can I serve you?” (Niwahudumie nini?)
“What do you have for dinner?” (Una chakula gani cha usiku?)
Hapo Caroline hakujibu kitu chochote kwa sababu hakuwa na uzoefu wa vyakula vilivyouzwa mahali pale ndiyo kwanza alikuwa na siku mbili tu! Alichofanya ni kuchukua karatasi yenye orodha ya vyakula vyote na kuwakabidhi wateja wake ili wachague wenyewe, walipomaliza aliondoka kupeleka oda yao jikoni.
“Mnaonaje?” O’brien aliwauliza wenzake baada ya Caroline kuondoka!
“Itakuwa kazi ngumu kidogo!”
“Nyie niachieni mimi, si fungu ninalo mfukoni?” Kennedy alisema.
“Ndiyo!”
“Basi punguzeni wasiwasi!”
********
Caroline hakurudi tena mpaka wakati analeta chakula mezani kwao na alisaidia kuwanawisha mikono na wote wakaanza kula, hawakutaka aondoke eneo hilo ili awe karibu nao walijaribu kufanya kilichowezekana ili awazoee, baada ya chakula Kennedy alichomoa noti ya dola mia katika pochi yake na kumkabidhi Caroline akalipe kaunta!
Alipoondoka tu mezani Kennedy na wenzake waondoka mezani mbio kwenda nje kabla hawajarudishiwa chenji! Nje waliingia ndani ya teksi na kuondoka zao! Caroline aliporudi macho yake yalipambana na meza tupu! Alishindwa kuelewa walikuwa wapi, hakuwaona wakielekea bafuni! Mawazo yake yalimfanya afikiri walikuwa wamesahau chenji yao, alifungua mlango na kuanza kukimbia kwenda nje akiwatafuta lakini hakuwaona ndipo akarudi hadi ndani ambako alizikabidhi pesa hizo kwa mama mwenye hoteli na kumweleza kilichotokea.
“I have their business card here!” (Ninayo kadi yao ya biashara hapa) alisema mama huyo, akaichukua kadi na kunyanyua simu iliyokuwa mezani na kuanza kuponyeza namba ya simu aliyoiona katika kadi ya vijana wa The Three some!
“Hallow Ken speaking!” ( Haloo Ken anaongea!)
“Yeah, this is mom, you forgot you change!” (Ndio, mimi ni mama! Mmesahau chenji yenu hapa!)
“We did’nt forget, we meant it to be keep change for the girl who served us!” (Hatukusahau tulimaanisha msichana aliyetuhudumia aichukue kama zawadi yake!)
“Thanks!” ( Ahsanteni) alimaliza mama na kukata simu kisha akamgeukia Caroline huku akitabasamu.
“Kumbe hawakusahau, ilikuwa zawadi yako!”
“Oh Mungu wangu, pesa zote hiyo?”
“Ndiyo! Hapa hii ni kawaida lakini chukua hizi dola hamsini na mimi nibakie na dola ishirini au?”
“Hakuna shida mama!” aliitikia Caroline.
Kipato cha siku hiyo kilimfanya aamini kuwa kama angeendelea kufanya kazi angeweza kupata nauli ya kumrudisha nyumbani kwao Tanzania, katika muda wa siku mbili alizofanya kazi katika hoteli hiyo alishaweka akiba ya dola tisini na nne, hiyo ilimaanisha kama angefanya kazi wiki mbili angeweza kupata hata nauli na kuendelea na safari yake!
“Mimi hata nikifika Bombay tu inatosha nitakuwa nimesogea mbele, nitakuwa nazidi kuikimbia mikono ya Dk. Ian zaidi, nina hakika asilimia mia mpaka sasa hajui kama nipo hapa!” Aliwaza Caroline.
Asubuhi ya siku iliyofuata vijana hao walikuja tena hotelini kufungua vinywa vyao wakati wa kuondoka walimwachia Caroline chenji ya dola 20, waliendelea hivyo kila siku, Kennedy alikuwa karibu sana na Caroline lakini bila kumweleza kitu chochote kuhusu mapenzi! Alishangazwa sana na hali hiyo, kwani alichojua ilikuwa si kawaida ya mwanaume kutoa msaada bila kuomba mapenzi.
“Why are you doing all these to me?” (Kwanini mnanifanyia yote haya?) Kadri wema ulivyozidi Caroline alishindwa kuvumilia na kujikuta akiuliza.
“I love you and I know you’re in problems!” (Nakupenda na ninajua upo katika matatizo)
“Who told you about my problems?” (Nani alikwambia juu ya matatizo yangu?)
“Mom told me!” (Mama aliniambia) Kennedy alijibu na kumfanya Caroline ashangae ni kwanini mama alikuwa akitangaza siri zake! Lakini pamoja na hayo alijisifu kwa kumwambia uongo vinginevyo kama angesema ukweli siri yake yote ingekuwa nje na angekuwa katika hatari ya kukamatwa!
“I loved my husband so much!He was my everthing and he died a bad death, infront of my eyes!” (Nilimpenda sana mume wangu na alikuwa ni kila kitu kwangu na alikufa kifo kibaya mbele yangu!) Caroline aliongea huku akijifanya kulia ili kumficha Kennedy ukweli, alijua wazi hakuna kitu kingine ambacho kijana huyo aliambiwa zaidi ya kuwa yeye na mume wake walikuwa wawindaji porini na mumewe alikufa kwa kukanyagwa na Tembo! Huo ndiyo uongo aliomwambia mama Suzane! Hakujua hata kidogo kuwa mtu aliyekuwa akiongea nae alifahamu kila kitu kuhusu yeye na alikuwa katika mpango mkali wa kumteka.
“Don’t worry Marione I will help you!” (Usiwe na shaka Marione nitakusaidia)
“Thank you, what is your name?” ( Ahsante, jina lako wewe ni nani?)
“My name is Kennedy, I would like you to call me Ken....This is O’brien and the one at the corner is Nicky…guys this is Marione, my friend!” (Jina langu ni Kennedy ila ningependa uniite Ken.....huyu ni O’brien na yule pale kwenye kona ni Nicky..... jamani huyu ni rafiki yangu Marione!) Kennedy alimtambulisha Caroline kwa rafiki zake, kila walipomwita Marione alijisikia furaha kwani aligundua hakuna mtu aliyemtambua.
“Thank you so much for being good people to me!” (Asanteni sana kwa kuwa watu wema kwangu!) Alisema Caroline.
Kwa siku nyingine tatu Caroline alizidi kuwaona vijana wale wakienda hotelini kula chakula na utaratibu wa Kennedy uliendelea kuwa ule ule wa kuwacha chenji ya dola 10 hadi 20 kila siku! Bila hata kutegemea Caroline alijikuta akivutiwa na Kennedy kupita kiasi, macho yake yalianza kumwangalia Kennedy kwa mtazamo tofauti, alianza kuuona uzuri wa sura yake! Hakutaka kwenda zaidi ya pale lakini alishindwa, alijaribu kwa njia zake zote asiende mahali moyo wake ulipotaka kwenda lakini pia ilishindikana, Kennedy alizidi kuuteka moyo wake siku hadi siku.
“Lakini nilishaapa siwezi kumpenda mwanaume tena maishani mwangu, eh Mungu nisaidie!” Alijisemea mwenye kichwani mwake Caroline, alionekana kuzidiwa. Alijichukia kupita kiasi kwa tabia yake yakupenda ghafla.
Wema aliofanyiwa na Kennedy ulimteka kabisa, akamwona ndiye binadamu pekee mwenye moyo wa huruma aliyekutana nae katika Cambodia, moyo wake haukushtukia kitu chochote kibaya kutoka kwa Kennedy, alimwamini kupita kiasi bila kujua kilichokuwa kikiendelea kati ya Kennedy na Dk. Ian!
“Ni huyu ndiye atanisaidia kurudi nyumbani Tanzania kwa wazazi wangu!” Hayo ndiyo yalikuwa mawazo yake.
Kila mtu hotelini alianza kuhisi kulikuwa na kitu kilichoendelea kati ya Marione na Kennedy, hata mama mwenye hoteli alilielewa jambo hili na hakuwa na kipingamizi kwa sababu njia hiyo ilimletea wateja wengi, wasichana wote waliofanya kazi katika hoteli yake walikuwa na sura za kuvutia wateja! Kwa kufuata wasichana hawa hoteli yake iliuza chakula kingi sana kwa siku. Wakati mwingine aliwaruhusu wasichana hata kwenda kulala na wateja, hiyo ndiyo ilikuwa sifa ya mama Suzane. Hilo hata Kennedy na wenzake walishalisikia.
“Mama ninaomba leo nimchukue Marione twende nae ukumbini akaone ninavyopiga muziki, maana yeye kila siku analala! Hachoki?” Kennedy alimwambia mama Suzane, Caroline akiwa amesimama kando yake baada ya chakula, ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu ya jioni na muda mfupi baadae alitegemea kwenda ukumbini kwenye hoteli ya kitalii ya Triangle, ilikuwa hoteli maarufu sana katika Cambodia wakati huo..
“Mimi sina kipingamizi na pia sina wasiwasi na wewe hata kidogo! Nyie mkielewana inatosha ili mradi tu umrudishe mapema na salama!”
“Hilo halina wasiwasi hata kidogo mama!”
“Basi sawa! Au Marione unasemaje?”
“Sawa tu mama, acha leo na mimi nikafurahie kidogo maisha!” Tayari alishaanza kuisahau tabu yake.
“Basi nitakuja kumchukua saa tatu usiku!”
“Sawa tu Kennedy!”
Alipoondoka hapo Kennedy aliwaeleza wenzake juu ya mpango aliopanga na Caroline au Marione kama walivyomuita, wote walikubaliana siku hiyo wasifanye kitu chochote kibaya ili azidi kuwaamini zaidi, isitoshe mipango ilikuwa haijaandaliwa vizuri! Kweli siku hiyo Kennedy alimchukua Caroline na kwenda naye hadi ukumbini ambako walicheza muziki pamoja, alimrudisha salama salimini saa saba ya usiku! Kwa kitendo hicho imani ya Caroline kwa Kennedy ilizidi kuongezeka taratibu, katika muda wa wiki moja tu akawa hasikii wala haambiwi kwa Kennedy! Lakini pamoja na hali hiyo bado hakuwa tayari kueleza ukweli kuhusu maisha yake!
***********************
Siku tatu baadae mipango ya kumteka Caroline na kumpeleka Canada iliandaliwa, cheti cha daktari kuonyesha kuwa alikuwa mgonjwa kiliandaliwa, dawa za usingizi ziliwekwa tayari na ujanja ulifanyika tiketi ya ndege ikakatwa bila hati ya kusafiria ya Caroline kuonyeshwa, pesa iliongea.
Dk. Ian alitaarifiwa kila kitu juu ya ujio wa Caroline na alikaa mkao wa kula akimsubiri kwa hamu, aliwaambia vijana wake wapunguze mateso kwa Profesa Kadiri na mkewe Cynthia kwa sababu mtoto wao alishapatikana, wazazi wa Caroline walikuwa katika hali mbaya nchini Canada ingawa yeye Caroline hakuwa na habari juu ya jambo hilo aliendelea kuamini walikuwa nchini Tanzania na alikuwa na hamu kubwa ya kuwaona.
Kwa upande wake Dk. Ian kila kitu kilikuwa tayari kisubiri ujio wa Caroline, kila kitu kilikuwa tayari, shimo la kaburi lake lilishaandaliwa! Bunduki yake ilishajazwa risasi ishirini zikimsubiri Caroline afike! Zote zilitegemewa kuusambaza mwili wake tena kwa mkono wa Dk.Ian mwenyewe.
*************
“Marione when are you off duty?” (Marione unapumzika lini kazi?)
‘Me?” (Mimi!)
“Yeah,”(Ndiyo!)
“Every Saturday!” (Kila Jumamosi!)
“Do you like skiing?” (Unapenda kuteleza kwenye barafu?)
“Very much, but have never tried it!” ( Sana lakini sijawahi kujaribu)
“Why can’t you come with us to the virginia mountans where we shall be going for skiing next Saturday?” (Kwanini tusiende na sisi kwenye milima ya Virginia ambako tutakwenda kuteleza kwenye barafu?)
“I would love to!” (Ningependa kwenda!)
“No problem you come with us!” (Hakuna tatizo tutakwenda wote)
“But speak to mom first!” (Lakini ongea na mama kwanza!)
Kennedy alipoongea na mama Suzane hapakuwa na kipingamizi chochote, Caroline alibaki kuisubiri siku ya Jumamosi kwa hamu kubwa! Tangu siku hiyo ya Alhamisi siku zilikwenda taratibu kupita kiasi, alitaka hiyo ifike upesi ili aende na kustarehe na Kennedy kwenye barafu! Hakuelewa kitu chochote kilichoendelea, tayari alishaanza kuingia katika mapenzi na Kennedy, kuna wakati hata yeye mwenyewe alijishangaa ni kwanini ilikuwa rahisi kwake kumwamimini mtu kiasi hicho!
*********
Ndege ilitegemewa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Penh kuelekea Canada saa tisa na nusu alasiri, kila kitu kilishawekwa tayari, aliyekuwa akisubiriwa ni Caroline peke yake! Ilipogonga saa saba na nusu honi ya gari ililia mbele ya nyumba waliyoishi wafanyakazi wa mama Suzane, asubuhi ya siku hiyo Caroline alijiandaa tayari kwa safari ya kwenda milimani.
“Marionneeeeeee!” Aliita msichana aliyekuwa nje!
“Yees!”
“Ken is here!’ (Keni amefika!)
“I’m coming!” (Ninakuja!) aliongea huku akikimbia kushuka ngazi, hakutaka kumchelewesha Kennedy! Hakutaka kuonekana mtu asiyepangilia muda wake.
“What should I bring you when I come back!” (Nikuletee nini nikirudi!) Caroline alimuuliza mfanyakazi mwenzake aliyekuwa nje.
“Flowers” (Maua!), jina la msichana huyo aliitwa Flora na alipenda maua kama lilivyokuwa jina lake, hasa ya rangi nyekundu.
“I will do that!” Caroline alionekana mwenye furaha kupita kiasi, alionekana kama mtu aliyeishi Cambodia kwa miaka kumi, wakati alikuwa na wiki moja na siku chache tu! Wasichana wenzake walimwonea wivu kupata mvulana mzuri kama Kennedy aliyempa maraha yote yaliyohitajika! Caroline aliteremka mpaka mahali lilipoegeshwa gari la Kennedy! Siku hiyo tofauti na siku nyingine zote aliachiwa kiti cha mbele ambacho mara zote alikikalia Nicky! Kennedy alikuwa akiendesha, Caroline aliiona hiyo kama heshima kubwa kwake, aliwasalimia wote na kukaa kitini, akafunga mlango na baadae mkanda, gari likaondoka.
“Thank you for treating me like a queen!” (Ahsante kwa kunifanya Malkia) gari ilianza kuondoka kwa mwendo wa taratibu, Caroline alitoa mkono na kumpungia Flora, aliyesimama nje akimwangalia kwa jicho la husuda!
“See you later!” (Tutaonana baadae!) Alisema Caroline wakati gari likiondoka.
“How are you today Caroli….aahgh! Marione!” (Unajisikiaje leo Carol…..aahgh! Marione?) Kennedy aligundua alilofanya lilikuwa kosa kubwa, hata alipojaribu kurekebisha tayari alishachelewa, aliuona uso wa Caroline ukipauka ghafla, alionekana kama mtu aliyepokea habari za kifo..
“Mh!” Caroline aliguna lakini hakusema kitu chochote, kilichoendelea kichwani mwake ni msululu wa maswali juu ya namna gani Kennedy alilifahamu jina lake halisi wakati yeye alishajitabulisha kama Marione! Wakati akiwaza hayo, gari likiwa limetembea umbali wa kama kilometa tano hivi, alishutukia akiguswa na vitu kama midomo ya chupa katika kila upande wa shingo yake, aligeuka ili aone ni kitu gani kilimgusa macho yake yalikutana na mdomo wa miwili ya bastola.
“Tulia hivyo hivyo wala usifanye vurugu, vinginevyo utakufa!” Zilikuwa sauti za Nicky na O’brien.
“Ha! Kennedy vipi tena?”
“Tulia usifanye fujo, kunguni we! Unadhani wema wote uliofanyiwa ulikuwa wa bure?”
Caroline alibaki mdomo wazi kwake ilikuwa kama ndoto!
“Kwa hiyo mnakwenda kunibaka?”
“Akubake nani? Hii ni safari ya kwenda Canada kwa mumeo!”
Mwili wote wa Caroline ulikufa ganzi, alitamani ardhi ipasuke aingie ndani yake.
Je, nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.
W
aliingia Khartoum
Sudani saa 12:30
asubuhi, wote wakiwa wamechoka kupita kiasi. Harry hakuwa na uhakika kama Waarabu aliokuwa nao ndani ya gari wangemlipa pesa zote walizomuahidi kwa malipo ya ndege aliyoiiba kwa Dk. Ian na kumwacha Caroline katika matatizo makubwa.
Alichowaza wakati huo kilikuwa pesa hakukumbuka hata kidogo kuwa alimwachia Caroline kazi ngumu kwa kitendo alichokifanya, aliamini mikononi mwa Wavietnam asingetoka salama! Ni lazima wangemuua baada ya yeye kutoroka, kwa upande mwingine moyo wake ulimuuma sana kusababisha kifo cha mwanamke aliyempenda!
Alijua wazi ni kiasi gani Caroline alimpenda kwa dhati, lakini kwa ugumu wa moyo aliokuwa nao Harry aliyaweka mawazo hayo pembeni na kufikiria pesa ambazo alikuwa na uhakika baada ya kuzipata ni lazima angechukua madaraka ya nchi jirani ya Jamhuri ya Sokomoni, aliutamani sana Uraisi wa nchi hiyo na kwa kutumia pesa ambayo angelipwa baada ya biashara haramu aliyoifanya ingekuwa kwake kushinda katika uchaguzi wa Vyama vingi uliotegemewa kufanyika nchini humo miezi tisa mbele.
Gari lao lilisimama mbele ya jengo la ghorofa nne lililojengwa kwa vioo karibu kila mahali! Watu wengi walionekana kuingia na kutoka ndani ya jengo hilo, wazee wenye ndevu nyingi aliokuwa nao walishuka garini na kumwonyesha ishara kwamba naye alitakiwa kushuka, bila kuchelewa wala kusita Harry alianza kuwafuata wazee hao kwa nyuma, walipandisha jengo hilo hadi ghorofa ya nne na kila mahali walikopita kulikuwa na ulinzi mkali.
Lango la ghorofa ya nne lilifunguliwa na walinzi wawili wenye miraba minne na wote walikuwa na bunduki mikononi mwao,hali hiyo ilimtia hofu sana Harry! Kwa mara ya kwanza alihisi kutetemeka na kichwani mwake mawazo ya kudhulumiwa yalianza kumwingia, kwa mahali alipokuwa hata kama wazee wale wangeamua kumuua hakuna mtu angefahamu. Mawazo hayo yalimfanya asite kidogo kuingia ndani lakini baadaye aliupa moyo konde na kuingia huku akitembea kwa unyonge.
Walikwenda moja kwa moja hadi ndani kabisa ya jengo hilo, walivuka milango mitatu iliyokuwa na walinzi wa sampuli kama aliyoikuta kwenye lango la kwanza na kila mlinzi alikuwa na bunduki aina ya SMG, hali ya hatari ilitanda kila mahali na hakuna neno lolote lililoongewa zaidi ya “Asalam Aleykum!”.
Waliingia moja kwa moja ndani ya chumba kidogo kilichoandikwa “Comference Room” na humo waliwakuta wazee wengine watano wenye ndevu nyingi kama walivyokuwa aliongozana nao, ilivyoonekana kufuga ndevu ulikuwa utamaduni wao!Wote waliketi kuizunguka meza kubwa iliyokuwemo ndani ya chumba hicho, wazee wale waliendelea kuongea katika lugha ambayo Harry hakuilewa lakini alihisi kilikuwa ni Kiarabu, aliingiwa na wasiwasi zaidi kuona hashirikishwi katika maongezi hayo.
Mara ghafla milango miwili iliyokuwa nyuma ya chumba hicho ilifunguliwa wakaingia wanaume wawili wenye misuli wakiwa wameshika bunduki mikononi mwao, alipowaona Harry alihisi mkojo ukimpenya sababu ya woga, kwa hakika hakuamini kama eneo hilo lingekuwa na usalama kwake! Alianza kujilaumu ndani ya nafsi yake kwa kitendo cha kuwaamini wazee hao na kuwapa ndege kabla ya malipo.
Dostları ilə paylaş: |