Sababu ya kumpiga tunayo! Nia ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga Nduli Idi Amin tunayo, ni lazima tumpige!



Yüklə 0,95 Mb.
səhifə8/18
tarix31.10.2017
ölçüsü0,95 Mb.
#23549
1   ...   4   5   6   7   8   9   10   11   ...   18

Caroline alisikitika sana lakini kitu alichomsikitisha zaidi kilikuwa ni dawa yake, hata hivyo ahadi kuwa daktari angefika siku iliyofuata ilimfanya ajisikie vizuri.

“Bila daktari kuja nilikuwa naaibika!” Alimwambia mama yake.

*****************

Mpaka saa nne na nusu iliyofuata Dk. Ian alikuwa bado hajapiga simu kama alivyoahidi kufanya baada ya kuingia Dar es Salaam, Caroline alitakiwa kanisani saa saa tano kamili ambako ndoa yake ingefungwa! hofu na wasiwasi wake ulirejea tena na alishindwa kuelewa ni wapi alikokuwa daktari wake!

Magari tayari yalikuwa nje ya nyumba yao, watu walishapanda na matarambuta yalipigwa ni Caroline peke yake aliyekuwa akisubiriwa, alikuwa amegoma kabisa kutoka ndani kwenda kanisani! Hali yake haikuwa nzuri siku hiyo,alijisikia dalili kama za siku za nyuma!

Ilikuwa ni siku ya saba bila kutumia dawa ya kuzuia kifafa! Na kwa mujibu wa maelezo ya daktari wake kama zingepita siku saba bila kutumia dawa hiyo ilikuwa ni lazima aanguke! Alitakiwa kunywa dawa hiyo maisha yake yote.

Siku hiyo ya harusi ndiyo ilikuwa siku yake ya saba tangu amalize dawa zake, hivyo alijua kwa vyovyote kama angediriki kwenda kanisani ni lazima angeanguka kifafa mbele za watu na huo ndio ungekuwa mwisho wa uhusiano wke na Reginald kitu ambacho kwa hakika hakukitaka kitokee, alikuwa tayari harusi iahirshwe lakini asianguke kifafa mbele ya Reginald alielewa ni kiasi gani aliuchukia ugonjwa huo.

“Mwanangu twende tu labda leo hutaanguka inawezekana hizo siku saba zitakwisha saa sita ya usiku! Si unajua siku mpya huanza saa sita usiku? Twende tu mwanangu ukafunge ndoa yako ninaamini hutaanguka! Wala usiwe na wasiwasi tusipokwenda kabisa itakuwa aibu?”

“Mama ni heri aibu ya kutokwenda kanisani si aibu ya kuanguka kifafa kanisani!”

“Hapana Caroline, nakuomba mwanangu unyanyuke twende tu!”

Kwa sababu ya heshima na utii aliokuwa nayo kwa mama yake ingawa kwa shingo upande Caroline alinyanyuka kitandani alikokuwa amekaa akilia na kulinyoosha vizuri vazi lake la harusi lililokuwa limejikunya mwilini mwake.

Alitoka hadi nje na kuingia ndani ya gari, msafara mrefu ulianza kuondoka kuelekea kanisa la Mtakatifu Joseph ambako harusi ilipangwa kufungwa! Macho yake yalikuwa bado yakibubujikwa na machozi, ilikuwa tayari saa tano na nusu ikiwa nusu saa baada ya muda uliopangwa.

**************

Reginald alifika kanisani saa nne kamili asubuhi na kuanza kumsubiri bibi harusi mtarajiwa afike lakini hadi saa nne na nusu waliyopanga kukutana Caroline alikuwa hajaonekana, alianza kuingiwa na hofu juu ya jambo lililotokea hadi asitokee kanisani mpaka muda huo!

“Au amebadili mawazo yake nini?”Reginald alimuuliza mpambe wake.

“Sidhani ila nina uhakika kutakuwa na tatizo naomba tu isije kuwa ajali!”

“Sasa mbona hatokei!

Kila mtu ndani ya kanisa alianza kuhisi jambo baya lilikuwa limetokea, ilipofika saa tano kamili bila bibi harusi kutokea mawazo ya wengi yalianza kuhisi Reginald alikuwa ameachwa katika mataa! Ilikuwa ni aibu kubwa iliyopelekea Reginald kuanza kutokwa na machozi, alishindwa kuelewa ni kosa gani alilomfanyia Caroline mpaka kufikia uamuzi wa kulipa kisasi kibaya namna hiyo! Mpambe wake alimbembeleza wakati akilia na kumpa moyo kuwa lazima Caroline angefika!

Dakika chache baadaye walisikia matarumbeta yakipigwa nje ya kanisa na msafara ulionekana kuwasili, ilikuwa furaha kubwa mno kwa Reginald aliruka na kuanza kukimbia kwenda nje, mpambe wake alimfuata kwa nyuma, nje ndani ya gari lilopambwa vizuri alimwona Caroline akiwa katikati ya akinamama wawili shingo yake ikiwa imelala begani kwa mama mmoja, alipomwangalia vizuri mama huyo Reginald alimfahamu, alikuwa shangazi yake na Caroline! Alisogea hadi karibu kabisa na gari hilo.

“Shangazi poleni na matatizo mbona mmechelewa?’Aliuliza Reginald lakini hakuna aliyejibu swali lake.

“Mama nasikia kizunguzungu! Nasikia kizunguzungu siwezi kushuka garini nitaanguka!”Alisema Caroline wakati mama yake wakijaribu kumshusha garini.

“Jitahidi mwanangu!”

Caroline alijitahidi kama mama yake alivyomwomba na kwenda moja kwa moja hadi ndani ya kanisa ingawa kizunguzungu kiliendelea kumsumbua! Kwa kuwa alikuwa amechelewa padri alianza moja kwa moja shughuli ya kufungisha ndoa!

“Reginald unakubali kumuoa Caroline?”

“Ndiyo nakubali!” Reginald aliyajibu maswali yote kisha kumvalisha pete Caroline, padri akamgeukia Caroline na kumuuliza maswali yale yale lakini hakujibu kitu chochote alibaki ameduwaa! Kizunguzungu kilikuwa kikizidi kumbana.

***********************

“Excuse me!”(Samahani) Ilikuwa ni sauti ya mzungu nyuma akimuuliza mtu aliyesimama mlangoni mwa kanisa kama alimfahamu Caroline.

“Yeah!She is the one getting married today!”(Ndiye yeye anayeolewa leo!)

Bila kusita Dk. Ian alianza kukimbia kuingia ndani ya kanisa alijua msaada wake ulihitajika sana kuokoa jahazi, kwa hakika aliamini Caroline alikuwa katika wakati mgumu.

Je harusi hii itafanyika? Kifafa kitazuiliwa?Fuatilia wiki ijayo.

Sehemu ya 11

Baada ya kupata maelezo kutoka kwa mtu aliyemkuta mlangoni Dk. Ian alianza kuingia ndai ya kanisa la St. Joseph akikimbia, alipita katikati ya viti vilivyojaa watu na kwenda hadi mbele, kanisa lilikuwa kimya watu wakimsikiliza padri aliyekuwa akiendesha ibada hiyo.

Mami ya watu walifurika kanisani siku hiyo kushuhudia caroline akiolewa, Dk Ian alijua ni kiai gani alihitajika ili kunusuru harusi hiyo na kumwepusha caroline na aiba iliyokuwa mbele yake, wakati akipita watu wote kanisani waligeuka na kumwangalia, walionyesha mshangao kumwona mzee wa kizungu akikimbia katikati ya kanisa walikuwa wamebakiz kama hatua tatu kutoka mahali waliposimama caroline, Reginald wapambe wao pamoja na kuingiza mkono wake wa kulia mfukoni mwa koti lake na kutoa kichupa kidogo na kukishika kwa mkono wa kushoto kisha akaingiza tena mkono wake katika mfuko wake mwingine wa koti na kutoa bomba la sindano.

Aliyafanya yote hayo kwa haraka huku watu kanisani wakimshuhudia, lakini walishindwa kuelewa ni nini alichotaka kufanya! Alikinyanyua kichupa juu na kulichomeka bomba la sindano ndani yake na kuanza kuyavuta maji yaliyokuwemo kwa kutumia bomba alipomaliz alikirudisha kichupa mfukoni na kuanza kumsogelea caroline aliyekuwa akiyumbayumba.

Kabla hajamfikia alishtuka kumwona caroline akianguka chini na kulala chali, alianza kutupa miguu yake huku na kule hewani, mwili wake ulikakamaaa na mapovu mengi yalianza kumtoka mdomoni, kilikuwa kifafa! Mama na baba yake walishika mikono vichwani mwao ilikuwa ni aibu kubwa mno kwa upande wao.

Minong’oni ilianza kusikika kanisani.

“Bibi harusi ana kifafa yalianza kusikika kila mahali kanisani! Watu walinyanyuka vitini mwao na kuanza kusogea madhabahuni kushuhudia kama walichokisikia kilikuwa na ukweli ndani yake, kanisa zima lilitawaliwa na vurugu, kufikia hapo haikuwa harusi tena bali fujo.

“Caroline! Caroline! Caroline kumbe kweli una kifafa sasa kwanini nilipokuuliza ulikataa!” Alisema Reginald akipiga kelele ilikuwa ni aibu kubwa kwake pia.

Alipofikiria gharama alizokuwa ameingia katika maandalizi ya harusi hiyo roho ilimuuma sana, alijua kwa hakika asingeweza kuoa msichana mwenye kifafa maishani mwake, Reginald alipiga magoti chini na kuanza kumtingisha caroline sakafuni, caroline hakushtuka alikuwa amelala chini mwili wake ukiwa umekakamaa!

Profesa Kadiri baba yake caroline alishindwa kuvumilia kuona jinsi mtoto wake alivyokuwa akitingishwa sakafuni, alimfuata Reginald akamshika na kumnyanyua.

“niachie mzee nyei si mlijua mtoto wenu ana kifafa lakini mkataka kunitapeli? Sasa Mungu amewaaibisha!Nirudishieni mahari yangu sasa hivi!”Reginald alifoka.

“kijana hebu naomba uwe mtulivu kidogo mahari yako utapata acha kwanza tushughulikie hili tatizo la mtoto!”

“Haiwezekani!”Reginald aliendelea kufoka huku akilia machozi, alimkaba profesa Kadiri shati! Padri na watu wengine waliokuwepo walikwenda na kumshika wakimzuia asifanye fujo ndani ya nyumba ya Mungu lakini hakusikia.

“Kijana mbona leo umekuwa siyo mstaarafu?”

“Nataka mahari yangu mimi niondoke hapa, nikatafute mwanamke mwingine wa kuoa haraka!” alisema Reginald.

Kauli hiyo ilimuudhi sana profesa Kadiri na kumfanya atoke mbio hadi kwenye gari lake lililokuwa nje na aliporejea alikuwa na kitabu kidogo mkononi mwake! Kilikuwa kitabu cha hundi za benki.

“Kijana unanidai shilingi ngapi?”

“Shilingi milioni moja na nusu!”

“Hakuna zaidi ya hapo?”

“Hakuna wewe nipe tu hizo zinatosha!”

“Utapokea hundi maana leo ni Jumamosi benki zimekwishafungwa!”

“Nipe tu!”

Profesa kadiri aliinama na kuandika hundi ya shilingi milioni moja na nusu mbele ya padri na kumkabidhi Reginald wapambe wake walishangilia na kumbeba Reginald juu juu na kutoka naye nje ya kanisa, watu wengi waliobaki vitini baada ya timu ya Reginald kuondoka walikuwa ni ndugu na marafiki wa familia ya caroline peke yao.

Ilikuwa huzuni kubwa na watu wengi ndani ya kanisa walisikika wakilia, wengi walimwonea huruma caroline, nje miungurumo ya magari ilisikika ishara kuwa msafara wa Reginald na ndugu zake ulikuwa ukiondoka.

Padri alibaki amesimama bila kujua la kufanya, harusi ilikuwa imevunjika baada ya bibi harusi kuanguka kifafa ndani ya kanisa! Hakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya kuwapa pole wazazi wa caroline na ndugu zake wengine pole, lilikuwa ni jambo la kusikitisha sana!Katika miaka yote ishirini aliyofanya kazi ya Mungu hilo ndilo lilikuwa tukio la kwanza kwa padri Slivinus Urio aliyekuwa akiifungisha ndoa hiyo.

Dk. Ian alisimama mahali pale kimya kabisa, hakujua kitu gani angefanya, kuchelewa kwake kulikuwa kumesababisha matatizo, ndani ya moyo wake aliamini kama angewahi kufika Tanzania angemwepusha caroline na aibu iliyokuwa imempata! Alijisikia vibaya ndani ya nafsi yake, ingawa hakuifahamu lugha ya kiswahili hali aliyoiona pale ndani ya kanisa ilimuonyesha wazi kuwa harusi ilikuwa imevunjika na hilo ndilo lilimuumiza moyo zaidi.

Dk. Ian alikuwa mzaliwa wa Newzealend kutoka katika familia ya mfanyabiashara maarufu nchini humo, Smith William! Baba yake alikuwa miongoni mwa raia wa nchi hiyo waliopigana vita vya pili ya dunia na ilipokwisha baba yake alijikuta nchini Canada na kuamua kuanzisha maisha yake katika nchi hiyo jeshini alifanya kazi kama daktari wa jeshi la Canada.

Mwaka 1949 akiwa nchini Canada alimuoa binti wa tajiri maarufu nchini humo aliyeitwa Richard Mond!Mzee huyo alimiliki viwanda vya vyuma, hoteli nyingi za kitalii, alikuwa na mashamba makubwa ya ngano na kahawa! Alikuwa mtu aliyeheshimika sana nchini humo.

Tajiri huyo aliamua kumpa Smith mtoto wake baada ya kumponyesha ugonjwa wa kuvimba viungo uliomsumbua kwa miaka mingi na kutumia tiba nyingi bila mafanikio.

Smith alimponyesha kwa wiki mbili tu kwa furaha aliyokuwa nayo tajiri Richard aliamua kumpa Smith binti yake Christine awe mke wake! Smith hakuamini maana Christine alikuwa ni mwanamke mzuri.

Baada ya ndoa yake tajiri Mond alimkaribisha Smith kuishi naye nyumbani kwake, aliwapa nyumba nzuri ya kifahari kuishi, alimfanya kuwa daktari wa familia yake na miaka miwili baadaye mwaka 1951 Dk. Smith na mkewe Christine walipata mtoto wa kwanza waliyemwita Ian!

Dk. Smith alitaka mtoto wake awe daktari bingwa kama yeye, ili kutimiza hilo alimpeleka katika shule zilizofundisha masomo hayo na mwaka 1977 alipata digrii yake ya kwanza ya utabibu kutoka chuo kikuu cha Montreal na alisoma katika chuo hichohicho digrii mbili zaidi na kuwa daktari bingwa na magonjwa ya ubongo katika umri mdogo wa miaka 26.

Tajiri Mond na mke wake walifariki katika ajali mwaka 1983 na kuiacha mali yote mikononi mwa binti yao na mumewe smith!Maisha yakabadilika na wakajikuta tayari ni mamilionea Dk. Smith alitajirika ghafla! Lakini nao pia hawakuishi muda mrefu sana walikufa miaka miwili baadaye kwa ajili ya gari vilevile na kuiacha mali yote mikononi mwa mtoto wao pekee Ian Smith.

Wakati hayo yanatokea Ian alifanya kazi katika hospitali ya rufaa ya Montreal alilazimika kuacha kazi ya udaktari na kuwa mfanyabiashara lakini alisaidia wagonjwa pale alipotakiwa kufanya hivyo! Alijipatia sifa kubwa sana katika kutibu wagonjwa wenye kifafa, hivyo wagonjwa wengi walimfuata nyumbani kwao kwa ushauri,hivyo ndivyo walivyofahaimiana na Caroline!

Miaka mitatu baadaye biashara baadaye biashara hiyo ilimuongezea utajiri mara tatu zaidi, watu walishindwa kuelewa ni kwanini hali hiyo ilitokea lakini siri kubwa ya utajiri wake ilikuwa ni kujiunga na kundi la mafia, alilitumia kundi hilo kufanya biashara yake ya madawa ya kulevya na kuwavamia watu usiku na kuwaibia mali zao.

Ni shughuli hizi haramu ndizo zilimfanya Ian atajirike zaidi hakuna mtu aliyefahamu siri hii zaidi ya watu aliofanya nao kazi! Kwa nje Dk, Ian alionekana mtu mwema na aliyesaidia watu wenye shida lakini kwa ndani alikuwa muuaji, mtu asiye na huruma aliyeua mke wake wa kwanza, Doroth kabla hata ya kuzaa naye mtoto baada ya mwanamke huyo kutoboa siri ya kazi yake Dk. Ian kujikuta matatani! Isingekuwa pesa zake angenyongwa.

Wiki mbili baada ya kutoka mahabusu alikokuwa amefungiwa mke wake alikutwa ufukweni mwa bahari akiwa amekufa baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha! Hakuna upelelezi uliofanyika kufuatia hongo alilolitembeza kwa wakuu wa polisi! Hakutaka tena kuao baada ya tukio hilo kwa kuogopa siri zake kuvuja, aliishi maisha ya upweke yaliyojaa faragha na usiri wa hali ya juu.

Caroline alizinduka na kuangalia huku na kule kanisani! Alimwona mama yake akilia machozi, kumbukumbu kuwa alikuwa kanisani kufunga ndoa zilimwijia lakini hakumwona Reginald mahali pale! Kumbukumbu za kizunguzungu alichokipata pia zilimwijia na alipojipapasa alikuta kipande cha mti kikiwa katikati ya meno yake! Aliwekewa kipande hicho kilichofungwa na kitambaa kila alipoanguka ili kuzuia kuuma ulimi.

“Padri yupo wapi Reginald?”

“Reginald………..!” Padri alishindwa kumalizia sentensi yake.

“Tufungishe basi ndoa tuondoke?”

Kwa kauli hiyo ilibidi padri amsogelee caroline na kuanza kumweleza juu ya kila kitu kilichotokea, caroline alilia machozi kwa uchungu! Kwa mara nyingine tena kifafa chake kilikuwa kimwaibisha!

Mara ghafla alishtukia kitambaa kikipita usoni kwake na kumfuta machozi yake alipogeuka kuangalia nyuma yake alimwona Dk.Ian.

“I’m sorry caroline! Very sorry for being late!All these is because of me!”(Nisamahe caroline, nisamehe kwa kuchelewa yote haya ni kwa sababu yangu!) alisema Dk.Ian akiwa amemkumbatia caroline, aliyekuwa akilia mfululizo.

“My husband to be has left me because I’m epileptic! Who is gonna marry me?”(Mume wangu mtarajiwa ameniacha kwa sababu nina kifafa nani atania sasa?”

“Don’t worry!(Usiwe na wasiwasi!)

“I wil never be happy again!”(sitakuwa na furaha tena!)

“It is my fault caroline! For that reason your happiness Is my responsibility!”(Ni makosa yangu caroline kwa sababu hiyo nina wajibu mkubwa wa kukufanya uwe na furaha!)

“Yeah!(ndiyo!)

“How?”(Kivipi?)

“I’m going to marry you(Nitakuoa!)

“Marry me?when?(kunioa mimi? Lini?)

“Today and right now!”(Leo tena sasa hivi)

“Your’re jocking Ian?”(Unanitania Ian!

Akiwa ameumia moyoni mwake kwa yaliyotokea ingawa aliahidi kutooa kabisa maishani mwake alijikuta akimfuata padri na kumweleza alichotaka kufanya ndani ya kanisa wakati huo! Padri alishangazwa na uamuzi huo na kuwaita wazazi wa Caroline pamoja na caroline mwenyewe na kuongea nao.

Caroline hakuwa na kipigamizi watu waliobaki kanisani walitangaziwa juu ya bahati iliyokuwa imejitokeza kila mtu aliruka na kushangilia, ndoa ikawa imefungwa hakun aliyekuwa tayari kuamini kilichotokea caroline hakulia tena alifurahi kuolewa na mtu aliyekifahamu kifafa chake na aliyekuwa na tiba ya tatizo hilo.

Harusi hiyo ilifuatiwa na tafrija ya nguvu iliyofanyika katika hoteli ya sheraton kwa gharama za Dk. Ian hapakuwahi kuwa na tafrija kubwa kiasi hicho katika historia ya jiji la Dar es salaam watu walikunywa na kula hadi kusaza, muda wote wa harusi hiyo caroline alionekana kucheka na kufurahi hakuwa na machozi tena.

Majira ya saa 8:30 usiku waliondoka ukumbini kwenda kulala katika vyumba vya juu ya hoteli hiyo sheraton. Walikaa katika hoteli hiyo kwa wiki mbili kwa gharama za Ian. Wakaondoka kwenda Canada reginald alipoanza kuwafanyia fujo akidai kuwa caroline alikuwa mke na alimtaka aondoke naye.

Caroline akawa ameondoka Tanzania kwenda Canada kwa mara ya pili lakini safari hiii akiwa mke wa mtu tajiri kuliko watu wote katika nchi hiyo, alijua maisha yalikuwa raha mustarehe baada ya hapo asingelia tena wala kuishi kwa majonzi! Lakini kitu kimoja tu hakukifahamu Dk. Ian alikuwa muuaji!



Je nini kitaendelea Canada? Je huo ndio mwisho wa matatizo ya Caroline? Fuatilia wiki ijayo!

N

i wanaume wengi 
waliomwacha katika 
maisha yake sababu ya ugonjwa wa kifafa aliozaliwa nao, aliwachukia wanaume wote waliomnyanyasa kwa sababu ya ugonjwa isipokuwa mwanamume mmoja tu naye alikuwa Harry! Ndani ya nafsi yake bado Caroline alimpenda Harry, alimfikiria karibu kila siku iliyopita! Harry alikuwa moyoni mwake na alikuwa tayari kumsamehe kama angekuja na kumwomba msamaha.



Lakini Harry hakufanya hivyo, baada ya kumwacha Caroline wakati huo wakisoma wote katika shule ya sekondari ya Arusha hakudiriki hata siku moja kumtafuta Caroline, kumpigia simu wala kumwandikia kadi! Hapakuwa na mawasiliano yoyote kati yao tangu Caroline ahamishwe na wazazi wake Arusha, jambo lililomuonyesha Caroline wazi kuwa Harry alimchukia na alimchukia sababu ya kifafa.

Pamoja na kuyafahamu hayo yote bado Caroline alimpenda Harry na aliamini siku moja wangekutana na kuurudisha tena uhusiano wao, hakumtaka mwanaume mwingine yeyote maishani mwake hilo ndilo aliloamini Caroline.

****************

Baada ya Caroline kuachana na Harry katika shule ya sekondari ya Arusha na yeye kuhamia shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani, kijana huyo alimalizia kidato cha nne na baadaye kuendelea na kidato cha sita katika shule hiyohiyo.

Alipomaliza kidato cha sita alichukuliwa na baba yake aliyekuwa raia wa Uingereza na kwenda nchini humo ambako alijiunga na chuo kikuu cha Manchester Air zone Institute kwa ajili ya masomo ya Urubani na ufundi wa ndege, yalikuwa ni masomo ya miaka mitano na alimaliza na kupata digrii yake.

Maisha yake yalikuwa mazuri kwa sababu baba yake alikuwa na uwezo mkubwa kipesa! Alipata kila alichotaka, alibadilisha wasichana wazuri kadri alivyotaka! Hata siku moja hakuwahi kumkumbuka Caroline, ilikuwa ni kama hakuwahi kukutana na msichana wa aina hiyo maishani mwake! Alimchukia Caroline na hakupenda kabisa kuwa na uhusiano na msichana mwenye kifafa na hata kusikia habari zake.

Kazi yake ya kwanza aliyopata baada ya kumaliza chuo kikuu ilikuwa ni katika shirika la ndege lililoitwa Air One, huko aliajiriwa kama rubani na fundi wa ndege. Hakukaa sana shirika hilo akaamua kuhamia nchini Marekani ambako aliajiriwa na shirika jingine kubwa la ndege lililoitwa USD Airlines, lilimiliki ndege nyingi na Harry alikabidhiwa ndege aina ya Boeing 737 iliyosafiri kwenda katika nchi za Mashariki ya kati kutokea Marekani.

Ilikuwa ni kazi ngumu kiasi kwamba robo tatu ya maisha ya Harry yalihamia kwenye ndege, kila siku kwake ilikuwa safari na alipopata nafasi ya kupumzika ilikuwa ni kulala na alipoamka alioga na kuingia safarini tena! Maisha yake yote yalihamia angani ni mara chache sana alikuwa nchi kavu. Sababu ya kazi nyingi hata siku moja hakuwahi kumkumbuka Caroline katika maisha yake ingawa Caroline bado aliteseka.

*****************

“Ian kweli umenioa?”

“Ni kweli huamini Caroline?”

“Sio rahisi kuamini!”

“Naomba uelewe hivyo! Niliumia sana ulipoachwa kanisani na nilijilaumu sana kukucheleweshea dawa, aibu yote uliyoipata ilikuwa ni sababu yangu ndio maana nimeamua kukuoa Caroline nataka uwe na furaha katika maisha yako”

“Utaniweza kweli na kifafa changu?”

“Ninalijua sana tatizo lako lakini bado nimeamua kukuoa, hivyo wasiwasi ondoa!”

Waliendelea kuongea wakiwa ndani ya ndege ya shirika la ndege la British Airways wakielekea Copenhagen nchini Dernmark baada ya kutoka hapo ndege ilitegemewa kuruka moja kwa moja hadi Ottawa nchini Canada, huo ndio ungekuwa mwisho wa safari yao na ni hapo ndipo maisha mapya ya Caroline yangekuwa! Mpaka wakati huo alikuwa bado haamini pamoja na kuhakikishiwa na Dk. Ian kuwa kweli alikuwa ameolewa.

Walitua kwenye uwanja wa ndege wa Ottawa saa kumi na mbili na nusu ya jioni, walipotoka nje ya uwanja Caroline alishangazwa na mapokezi yaliyokuwepo uwanjani hapo! Kulikuwa na magari aina ya benzi ya rangi nyeusi yapatayo ishirini yote yakiwa yamekuja kuwapokea wao.

Watu waliowapokea wote walivaa suti nyeusi pamoja na tai! Walipendeza na walionekana ni watu wenye uwezo lakini wote Walipiga magoti na kuwasalimia Dk. Ian na Caroline! Kwa Caroline yote yaliyokuwa yakitokea yalikuwa ni ndoto, hakuamini hata kidogo kuwa ingekuwa kweli! Hakuwahi kuwaza wala kutegemea kuwa siku moja angepigiwa magoti na mzungu akisalimiwa.

“This is my wife Caroline..... Caro meet Mr Lead, my assitant!”(Huyu ni mke wangu anaitwa Caroline.....Caro kutana na msaidizi wangu anaitwa bwana Lead!) Dk. Ian alimtambulisha Caroline kwa mzee mmoja wa makamo na baada ya utambulisho huo mzee huyo alipiga magoti chini na kumsalimia Caroline akiwa ameinamisha kichwa.

Ilikuwa ni kama mbinguni, mambo aliyokuwa akifanyiwa alizoea kuyaona akifanyiwa Malkia Elizabeth kwenye luninga na hakuwahi kufikiri siku moja angefanyiwa yeye. Waliongozwa na kupelekwa moja kwa moja kwenye gari la kifahari benzi la milango minane lililokuwa limewekwa tayari kwa ajili yao, matarumbeta yalilia kila upande wa uwanja huo na wapiga picha walikuwa na kazi ngumu kurekodi kila kilichokuwa kikiendelea.

Ndani ya gari Caroline alimkumbatia Dk. Ian na kumpiga mabusu mfululizo usoni akimshukuru kwa kila kitu alichomfanyia.

“Thank you Ian! Thank you again and again! I thank you a milion times!”(Asante Ian! Asante tena na tena na asante mara milioni moja zaidi!)

“For what!”(Unanishukuru kwa nini?) Dk. Ian aliuliza.

“Thank you for making me a Queen in my life!”(Asante kwa kunifanya Malkia katika maisha yangu!)

“Take it easy!”(Usijali!)

Msafara wa magari uliondoka kuelekea nyumbani kwa Dk. Ian katika eneo la matajiri mjini humo, kilometa kama kumi kutoka uwanja wa ndege gari lilikata kulia na kuingia kwenye ngome kubwa ya rangi nyeupe! Ndani ya ngome hiyo kulikuwa na uwazi mkubwa uliopandwa nyasi na maua mazuri ya kupendeza, magari yalizidi kusonga mbele yakipita katikati ya bustani za maua! Caroline hakuwa kuona sehemu nzuri kama hiyo maishani mwake na hakutegemea sehemu kama hizo zilikuwepo duniani.

Mbele kama kilometa moja na nusu walisimama mbele ya jumba kubwa la kifahari wanawake wengi walijipanga nje ya jumba hilo wakiwa wamevaa nguo nyeupe na wakiwa vikawa vidogo vya rangi ya Kahawia wakipepea hewani! Caroline alizidi kushangaa, mlango ulifunguliwa na wote wawili waliteremka na kusimama, wanawake wanne waliwafuata na kuanza kuwapepea wakiwaongoza kuingia ndani ya nyumba.

“Oh! Thanks God, at last I can relax, the only thing troubling me is this man, Harry Robertson! How can I get him off my mind and enjoy life with my beloved husband?”(Oh! Nakushukuru Mungu mwisho sasa napumzika, kitu kimoja tu kinanisumbua ni huyu mwanaume, Harry ninawezaje kumtoa kabisa akilini mwangu nikaendelea kufaidi maisha na mume wangu?) Aliwaza Caroline wakati akiishangaa nyumba ya Dk. Ian, ilijaa vioo na marumaru kila sehemu.

Walipitiliza moja kwa moja hadi chumbani ambako walioga na baadaye kujitupa kitandani, kwa mara ya kwanza katika maisha yake Caroline alilifaidi tendo la ndoa kwa hiari yake.

“Welcome into my life Caroline this is going to be your home forever!”(Karibu katika maisha yangu Caroline hapa ndio patakuwa nyumbani kwako milelel!)

“Thank you Ian for making me happy! I love you!”(Asante Ian kwa kunifanya niwe na furaha tena! Ninakupenda!)

“I love you too and I promise to love you forever!”(Nakupenda pia na ninaahidi kukupenda milele!)


Yüklə 0,95 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   ...   4   5   6   7   8   9   10   11   ...   18




Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2024
rəhbərliyinə müraciət

gir | qeydiyyatdan keç
    Ana səhifə


yükləyin