Tayari ilishatimu saa 1:10, ndani ya nyumba hiyo walipokelewa na watumishi wa ndani na wote wakaketi vitini, wasichana wawili walioonekana kama wahindi wekundu walijitokeza na kuwanza kumpepea Caroline kwa kutumia vikawa. Alikuwa ni kama Malkia ndani ya himaya ya mumewe, yote hayo yalimshangaza Harry.
“Hebu mmoja wenu aende akampepee yule mgeni wangu pale, hapa mmoja tu ananitosha!” Aliamuru Caroline.
Kauli hiyo ilimfanya mmoja wa wasichana hao kuondoka na kwenda kuanza kumpepea Harry mara moja, Harry alizidi kushangazwa na yote yaliyotokea ndani ya nyumba hiyo, ni mara ya kwanza katika maisha yake alijisikia Mfalme, hakuwahi kufanyiwa mambo kama hayo maishani mwake, saa nzima baadaye Caroline aliwafukuza wasichana waliokuwa wakiwapepea pamoja na wafanyakazi wengine wote ndani ya nyumba yake, wakabaki wao wawili tu!
“You can just go to bed, I will be ok!”(Nendeni tu mkalale sitakuwa na tatizo lolote!) aliwaambia wafanyakazi wake.
“Thank you madame! Will he sleep in the visitors lounge so that we can go and make the bed ready?”(Ahsante mama je mgeni atalala kwenye chumba cha wageni ili tukakitayarishe kitanda chake?)
“Just go I will handle that!”(Nendeni tu hilo nitalishughulikia!)
Baada ya wafanyakazi kuondoka Caroline bila woga wala kumfikiria mume wake Ian, aliyemnusuru katika matatizo aliyokuwa nayo ya kuachwa na wanaume sababu ya kifafa! Alinyanyuka kwenye kiti alichokaa na kuhamia katika kiti alichokaa Harry, lilikuwa kochi la kukaliwa na watu wawili! Aliuzungusha mkono wake wa kulia begani kwa Harry! Kumbukumbu zote za yaliyotokea wakiwa katika shule ya sekondari ya Arusha zilimwijia kichwani mwake, Caroline alishindwa kuvumilia na kujikua akimwaga machozi mfululizo.
“Ha! Mbona unalia tena?”
“Nimekumbuka ulivyonifanyia shuleni Arusha, ulinidhalilisha sana Harry tena mbele ya wasichana wako eti sababu nilikuwa na kifafa!”
“Caroline…Caroline…..Caroline….. tafadhali sana nisamehe, nimekwisha kuomba msamaha, hebu kubali kunisamehe na usahau yaliyopita!”
“Sawa Harry lakini….!”
“Nisamehe mpenzi!” Alisema tena Harry na kumkumbatia Caroline, tayari walikuwa wakibembea katika anga za mahaba. Dakika chache zilizofuata bila kujitambua walijikuta wapo kama walivyozaliwa na yaliyoendelea kati yao yalikuwa ya kuhatarisha maisha yao kama tajiri Ian Smith angeufahamu ukweli huo!
“I missed you!”(nilikukumbuka sana!)
“Me too, Caroline, cant you believe me?”(hata mimi pia Caroline hauwezi kuniamini?)
“No body can make me feel the way you do! My old man cant do it like this! Ohoooooo!” Caroline alizidi kulia kimahaba akiwa katikati ya mikono ya Harry.
Harry hakuyaamini macho wala akili yake kuwa mwanamke aliyekuwa amelala naye kitandani alikuwa Caroline! Mke wa mtu tajiri kupita kiasi duniani, Ian Smith. Ni kweli alimfahamu Caroline tangu shuleni lakini aliyekuwa naye kitandani hakuwa Caroline aliyemzoea.
Harry alijua jambo alilofanya lilikuwa ni hatari na alihofia sana lakini kwa upande mwingine jambo hilo lilikuwa njia ya yeye kujipatia utajiri kwani wakati wowote kwa kumtumia Caroline angeweza kuchota mamilioni ya pesa katika akaunti za tajiri Ian na kutajirika, alimshukuru Mungu kumkutanisha na Caroline tena.
“Kila kitu hupangwa na Mungu! Unafikiri nisingekuacha ungempata vipi tajiri Ian, ilikuwa ni lazima nikuache ili ukutane na mtu mwingine!”
“Ni kweli, lakini elewa bado nakupenda sana Harry sidhani kama katika maisha yangu nitampenda mwanaume mwingine kama ninavyokupenda wewe!”
“Najua! Hebu kwanza nieleze vizuri kuhusu kifafa chako!”
“Sina tena kifafa!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Ilikuwaje?”
“Ian alinitibu!”
“Kwani yeye daktari?”
“Ndiyo! Watu wengi sana wamepona!”
Siku hiyo hawakulala mpaka asubuhi, Caroline akimsimulia Harry yaliyotokea katika maisha yake, aibu zote alizozipata kutonana na ugonjwa wa kifafa mpaka kufikia kitendo cha kuachwa kanisani siku ya harusi na tena mbele ya padri.
“Pole sana!”
“Hivyo ndivyo ilivyo lakini nimekwishasahau!”
“Pamoja na hayo yote hivi sasa unaishi maisha mazuri au siyo?”
“Ndiyo lakini mume wangu ni mzee sana ninahitaji kuwa na kijana kama wewe ndiyo maana nataka wewe uendelee kuwa rubani wangu siku zote ili uzibe mapengo yaliyopo kwa Ian, ndiyo Ian ni tajiri lakini mimi kama mwanamke ninahitaji zaidi ya mali na chakula!”
“Usiwe na wasiwasi nitaziba mapengo yote ili mradi uniahidi kuficha siri!”
“Umeoa Harry?”
“Bado!”
“Safi kabisa, Mungu alikutunza kwa ajili yangu!”
*************
Mwezi mmoja ulikatika Harry na Caroline wakiishi ufukweni kama mke na mume, Caroline alifaidi maisha kupita kiasi! Ian alipopiga simu akitaka kuungana na mkewe kama walivyoahidiana Caroline alikataa.
“No! Not now, I need to be alone for another month Ian!”(Hapana! Ninahitaji kuwa peke yangu kwa mwezi mwingine mmoja!)
“Why?”(Kwanini?)
“No reasons but I need to be alone!”(Hakuna sababu lakini nahitaji kuwa peke yangu!)
“Ok! But take great care of yourself! How is Harry?”(Sawa! Lakini uwe mwangalifu sana! Harry anaendeleaje?)
“Doing fine, he is a good boy! Good than any body else in your company!”(Hajambo, ni kijana mzuri nafikiri kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya kampuni!)
“Sure?”(Kweli?)
“Yeah!”(Ndiyo!)
Wafanyakazi wote ufukweni walishangazwa na hali iliyoonekana kati ya Harry na Caroline, hawakuonekana kuwa kama mtu na bosi wake, picha iliyoonekana kati yao ilikuwa ni ya mtu na mpenzi wake walishangazwa na kitendo cha watu hao wawili kutembea wakiwa wameshikana viuno! Kuogelea pamoja na kulala katika nyumba moja wakati nyumba ya wageni ilikuwepo pembeni.
Kilichowafanya wawe na uhakika zaidi ni kitendo cha wafanyakazi wote kuondolewa ndani ya nyumba kila ilipotimia saa moja jioni jambo ambalo halikuwa kawaida kabisa ya kila wageni walipokuja kukaa katika nyumba hiyo kutoka Canada au kwingineko kokote duniani.
************
Thomson alikuwa mmoja wa wafanyakazi katika nyumba ya tajiri Ian Smith, kabla ya kubla ya kuhamishiwa Miami aliishi nchini Canada akifanya kazi katika nyumba ya Dk. Ian.
Pamoja na kuwa mfanyakazi lakini alikuwa rafiki mkubwa na mpelelezi wa tajiri Ian, alishirikiana na Ian mara nyingi katika mauaji, ni yeye aliyewatilia sumu katika chai wafanyabiashara wanne wa Kijapani walipokuja na mamilioni ya dola ufukweni iami kuongea biashara na Ian Smith! Wakafa na maiti zao kuzamishwa baharini, hakuna mtu aliyefahamu kilichotokea na pesa zote walizokuwa nazo zilichukuliwa na Ian kwa sababu hiyo Ian alimwamini Thomson kuliko mfanyakazi mwingine yeyote.
Thomson alikuwa miongoni mwa watu walioshangazwa na tabia ya mke wa bosi wake pamoja na rubani na kuamua kufuatilia nyendo zao taratibu hakutaka kufanya haraka asije kushtukiwa.
Ilikuwa ni katikati ya usiku, Thomson alikuwa nyuma ya dirisha la chumba cha kulala cha nyumba ya tajiri Ian, alisikia sauti za watu wakiongea, alipotupa macho ndani kupitia katikati ya mapazia aliwaona Harry na Caroline wakiwa wamekumbatiana.
“Caroline!”
“Naam!”
“Unanipenda kweli?”
“Ndiyo nakupenda sana!”
“Upo tayari kuacha vyote kwa ajili yangu?”
“Ndiyo!”
“Hakika?”
“Ndiyo!”
“Basi hakuna haja ya kurudi tena kwa Ian, tuondoke zetu kesho!”
“Kwenda wapi?”
“Nitakueleza mbele ya safari tutakwenda wapi!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Lakini Ian siyo mtu mzuri sana harry atatuua kama tumeamua hivyo ni lazima twende mahali ambako kwa hakika hatatupata!”
“Hawezi kutupata!”
“Huko tutaishije?”
“Tutaiuza ndege hii na tutapata mamilioni ya dola, tutabadili sura zetu na kuishi maisha ya raha mustarehe na Ian atatutafuta maisha yake yote bila kutupata au wewe unaonaje?”
“Sawa tu!”
Thomson alizidi kuchungulia dirishani na kuyasikia maneno waliyokuwa wakiongea, hakuelewa chochote sababu waliongea kwa kiswahili! Lakini hilo halikuwa kikwazo kwake, aliyoyaona kwa macho yalitosha! Roho ilimuuma sana kuona mke wa bosi na rafiki yake wake anachezewa kiasi hicho, alitamani aikamilishe kazi ya kuwateketeza wote wawili kwa moto ndani ya nyumba hiyo lakini alishindwa kufanya hivyo kwa sababu ilikuwa ni lazima awasiliane na tajiri Ian na kumweleza juu ya alichokishuhudia.
Alinyata na kwenda hadi nyumbani kwake ambako alinyanyua simu na kuanza kuzungusha namba za Canada nyumbani kwa mzee Ian!
“Hallow Ian Hapa!”
“Ndiyo shikamoo mzee!”
“Unasemaje Thomson mbona simu usiku huu?”
“Mzee kuna jambo ambalo kwa kweli ni lazima nikueleze ingawa sitakiwi kabisa kufanya hivyo!”
“Jambo gani hilo?”
“Siyo siri mama analala chumba kimoja na rubani wake, nimewaona kwa macho yangu sasa hivi wapo chumbani wakifanya mapenzi!”
“Una uhakika?”
“Asilimia mia moja!”Alijibu Thomson na simu ikakatwa, hiyo ilitosha kuonyesha ni hasira kali kiasi gani aliyokuwa nayo Ian kwa wakati huo! Thomson alimfahamu vizuri sana Ian, alipofanya hivyo ilimaanisha vifo vya watu.
**********
Mwili wa Ian ulikuwa umevimba alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Miami asubuhi hiyo, kila mtu alishangaa ni kwa nini safari hiyo ilikuwa ya dharura kiasi hicho kawaida yake kabla ya safari alitoa taarifa siku mbili kabla ya safari yake.
“They have to die! A very bad death!(Ni lazima wafe kifo kibaya sana!)
Je nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo utamu ndio sasa umeanza.
Ilikuwa ni hali ya mawingu
na ukungu katika anga
yote ya Miami asubuhi hiyo katika kipindi hicho cha mwaka, baridi ilitanda kila mahali,ndege ya Caroline ilikuwa ikikatiza katikati ya mawingu kuelekea mahali ambako Caroline hakupafahamu! Ni Harry peke yake ndiye aliyeelewa mahali walikokuwa wakielekea.
Pamoja na hali hiyo bado Caroline hakuonyesha wasiwasi wowote, alimwamini Harry kupita kiasi, asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameamua kumwacha kabisa mzee Ian, mtu aliyemponya kifafa na kumtoa katika umasikini akamfanya kuwa Malkia! Maisha ambayo Caroline hakuwahi kuyafikiria yangetokea katika uhai wake.
Ni mzee Ian ndiye alifuta machozi na huzuni katika maisha ya Caroline, lakini alikuwa akimwacha kwa sababu ya Harry! Kijana mwenye sura nzuri ya kuvutia, mpenzi wa kwanza katika Maisha yake, aliyemwonyesha nini ilikuwa maana ya kupendwa na umuhimu wa mapenzi katika maisha ya mwanadamu!
Lakini ni Harry huyo huyo ndiye aliyemwacha Caroline sababu ya kifafa miaka mingi wakisoma katika shule ya sekondari huko Arusha nchini Tanzania! Caroline hakuwahi kuumia kama kipindi hicho katika maisha yake ilikuwa kidogo tu achanganyikiwe.
Shule ilimshinda ikabidi ahamishiwe Dar es Salaam, wazazi waliamua kumuondoa Arusha ili kumuepusha na huzuni pamoja na aibu aliyoipata baada ya kuachwa na Harry! Lakini yote hayo Caroline hakuyajali na hakutaka kuyakumbuka, alimpenda Harry aliamini bila yeye yasingekuwa kamili.
Caroline alimpenda Harry kupindukia na alifanya yote aliyokuwa akitenda kuufurahisha moyo wake, hakutaka kufikiria mara mbili wala kuuona ubaya na hatari ya jambo alilokuwa akilifanya, alitaka kuwa na furaha katika maisha yake hata kama furaha hiyo ingedumu kwa wiki mbili tu! Ni Harry peke yake aliyekuwa hiyo furaha aliyoitafuta na si kitu kingine chochote. Pamoja na kuolewa na mwanaume mwenye mali na tajiri bado maisha yake hayakuwa na furaha.
“Harry I missed my period!”(Harry sikupata siku zangu za mwezi huu)
“Sure?”(Hakika?)
“Yeah!”(Ndiyo!)
“You’re kidding Caroline!”(Unatania Caroline)
“Nope!”(Hapana!)
“Then that’s good news, eventually we’re gonna have our first baby girl(Basi hiyo ni habari njema hatimaye tunapata mtoto wetu wa kwanza wa kike!)
“You like baby girls isn’t?”(Unapenda watoto wa kike au siyo?)
“Most men do like baby girl!”(Wanaume wengi hupenda watoto wa kike!)
“Me too!”(Mimi pia!)
“Caroline are you sure you pregnant? Don’t make me euphoric for nothing!”(Lakini una uhakika una mimba? Usinifanye nifurahi kupita kiasi kumbe hakuna kitu!)
“Ok! Lets give it one week more!”(Basi acha tuipe tena wiki nyingine moja zaidi tuangalie!)
Ndege ilizidi kukatisha katikati ya mawingu, Caroline akiwa amekaa kando ya Harry aliyekuwa akiendesha ndege hiyo kwa kasi ya ajabu lakini kwa uangalifu! Hakuonekana kuwa mtu mwenye hofu moyoni mwake hata kidogo, lakini ndani ya akili ya Caroline kulijaa mahangaiko kisawasawa, alimfahamu vizuri Dk. Ian na alijua kabisa jambo walilokuwa wakilifanya lilikuwa ni la hatari kubwa! Alijua ni kiasi gani Dk Ian alimpenda na pia kiasi gani angekasirika baada ya kuambiwa kuwa mke wake alitoroka na mtu mwingine, mbaya zaidi alitoroka na ndege ya kifahari ya pesa nyingi aliyomnunulia siku chache kabla kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.
Caroline alijua mbele yake kulikuwa na kifo! Alijua ni kiasi gani kitendo cha kuua kilikuwa kidogo kwa Dk. Ian! Alipomwangalia Harry alimhurumia ingawa yeye hakuonekana kujali kitu chochote, Caroline aliamini kitendo walichokuwa wakifanya kilimaanisha kufungua milango ya kaburi ili wadumbukie ndani!
“Harry where are we flying to!”(Harry hivi tunaelekea wapi!)
“I will let you know!”(Nitakujulisha baadaye!)
“I need to know!”(nahitaji kufahamu!)
“Don’t worry darling we are going to hide somewhere in a very wonderful place! Where Dk. Ian will never see us again!”(Usiwe na wasiwasi mpenzi, tunakwenda kujificha mahali pazuri ambapo Dk. Ian hatatuona tena!)
“You sure of what you talking ‘bout’?” (Una uhakika na kitu unachokiongelea?)
“Positively sure!” (Uhakika wa nguvu!)
“Mind you, Dr Ian is a dangerous person Harry, I know he doesn’t joke, he is so mean! Once he says kill, he means it! And I know thats what he is going to say”(lakini kumbuka Dk. Ian ni mtu hatari sana Harry! Namfahamu vizuri, ni mtu ambaye humaanisha ayasemayo, akisema ua hatanii na ninajua hicho ndicho atasema baada ya kusikia nimetoroka na wewe!) Alisema Caroline.
“Don’t worry Caro, he wont see us even if he uses a Microscope!”(Usijali Caroline, hatatuona hata kama atatumia darubini!) Alijibu Harry huku akicheka na baadaye walipigana mabusu kwa midomo yao laini na safari ikaendelea.
Kwa masaa karibu matano yaliyofuata ndege ilizidi kukatisha mawingu kuelekea mahali ambako Caroline hakupafahamu, alikuwa usingizini na katika usingizi huo alimwota Dk. Ian! Alikuwa amefungwa kamba akimwagiwa mafuta ya petroli mwili mzima ili achomwe moto, Dk. Ian alisimama mbele yake akifurahia kitendo hicho, baada ya kulowanishwa vizuri na petroli Dk. Ian alikabidhiwa kiberiti, akachomoa njiti moja na kuiwasha kisha akamtupia Caroline mwilini mwake, akashika moto na kuanza kuungua, alipiga kelele akiomba msaada lakini hapakuwa na mtu wa kumsaidia!
Ghafla Caroline alizinduka usingizini akipiga kelele, macho yalikuwa yamemtoka na mwili wake wote ulikuwa ukitoka jasho jingi!
“Vipi Caroline?” Harry aliuliza baada ya kumwona Caroline akishtuka na kuketi.
“Ndoto tu!”
“Ndoto? Ndoto gani ya kukushtua namna hiyo?Umeota unadumbukia shimoni nini? Maana hizo ndizo huwa ndoto za kutisha zaidi!”
“Afadhali ingekuwa hiyo ya kudumbukia shimoni!”
“Kwani umeota ndoto gani?”
“Nimemwota Dk. Ian!”
“Anafanya nini?”
“Amewaamuru watu wake wanimwangie mafuta ya petroli halafu yeye akanilipua na kiberiti!”
“Ah wapi!” Harry alisema huku akicheka.... “hilo ni jambo lisilowezekana kabisa, hiyo ni ndoto tu! Atakupata wapi Dk. Ian!”
“Unasema tu Harry! Si ajabu ipo siku atanipata kweli, na si ajabu wewe hautakuwepo siku hiyo!”
“Kwanini unasema hivyo Caroline?” Aliuliza Harry akionyesha huzuni kubwa.
“Sababu sikukuona katika ndoto yangu!”
“Nope!(Haiwezekani)
Nusu saa baadaye Caroline alipotupa macho yake nje kupitia dirishani aliuona msitu mkubwa kupita kiasi, hiyo ilimwonyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kutua, mbele kidogo waliona uwazi mkubwa usio na miti, kilikuwa ni kama kiwanja cha ndege kilichokuwa katikati ya pori, hakupaelewa mahali pale palikuwa ni wapi! Ndege ilizidi kushuka chini kuelekea ardhini, Harry akiwa kimya kabisa akili yake ilikuwa imeishia kwenye mtambo wa kuendeshea ndege.
“Harry unatua porini?”
“Tunatua kwa muda tu ili tupumzike kisha tutaendelea na safari yetu!”
“Una uhakika na uwanja huu?”
“Unaonekana hauna matatizo si ajabu uliwahi kutumika siku za nyuma!”
“Harry lakini inaweza kuwa hatari kwanini tusiendelee mbele mpaka kwenye mji wowote mkubwa ndio utue?”
“Naogopa kutua katika viwanja vikubwa huko nina hakika Dk. Ian atatukamata!” Alijibu Harry akizidi kuipeleka ndege taratibu ardhini ambako alifanikiwa kutua bila matatizo! Kilikuwa ni kiwanja cha ndege kamili lakini alishindwa kuelewa ni watu gani waliokitumia.
Baada ya kutua ardhini alifungua mlango na kuruka hadi ardhini Caroline akimfuata kwa nyuma, walikuwa katikati kabisa ya pori! Hapakuwa na dalili ya watu kuishi mahali pale, palitisha kupita kiasi.
“Harry hapa mahali sio pazuri! Ni bora tuondoke!”
“Kwanini?”
“Mwili wangu unachezwa na machale! Tutapata matatizo makubwa hapa!”
“Wewe ni muoga sana Caroline, niamini mimi! Unapokuwa na mimi tafadhali punguza wasiwasi!”
“Sawa lakini.....!” Kabla hajamaliza sentensi yake alishtukia Harry akipiga kelele, mshale wenye ncha kali ulikuwa umepenya kwenye bega lake la kushoto.
Harry alianguka chini akipiga kelele, damu nyingi zilikuwa zikimtoka kwenye mkono wake, Caroline alilala chini karibu kabisa na Harry, alipoinama tu mshale ulipita mahali alipokuwa amesimama na kusimama wima kwenye bodi la ndege yao! Hiyo ina maana asingelala mshale ungezama mwilini mwake. Hofu kubwa ilimwingia Caroline moyoni, hakuamini kama mishale ile ilitoka kwa wafuasi wa Dk. Ian! Ilikuwa si rahisi afahamu walikuwa mahali pale, Harry alizidi kulia akiomba msaada.
“Unaona sasa Harry! Nilikuambia hapa sio mahali pazuri palinitisha mimi!”
“Nisaidie Caroline!”
“Nifanye nini sasa?”
“Ungoe huu mshale!”
“Acha nijaribu lakini sina uhakika kama nitaweza!” Alijibu Caroline na kujaribu kuuvuta mshale huo huku Harry akilia kwa maumivu lakini ilishindikana kuutoa. Damu nyingi ziliendelea kumbubujika.
“Nifanye nini sasa?”
“Basi te...na nas...ikia mw...ili unai...shiwa ngu...vu! Nina wasiwasi mshale huu una sumu!” Alijibu Harry kwa sauti ya chini huku akikakatakata maneno na baadaye alikaa kimya.
“Harry! Harry! Harry!” Caroline aliita lakini Harry aliendelea kuwa kimya.
Ghafla kundi kubwa la watu waliovaa nusu uchi wakiwa wamefunikwa na kitambaa kidogo mbele kuficha sehemu zao za siri walijitokeza wakiwa wamevuta pinde zao tayari kuachia mishale, walitembea hatua za taratibu wakiisogelea ndege na waliimba wimbo ambao Caroline alishindwa kuuelewa ulikuwa katika lugha gani! Watu hao walivaa kofia kubwa za mikeka vichwani mwao kiasi kwamba haikuwa rahisi kuziona nyuso zao lakini kwa kuwaangalia ngozi za miili yao Caroline aliweza kuwafanananisha na wazungu au wahindi wekundu!
Akili ya Caroline ilimrudisha moja kwa moja katika filamu ya The Vietnam war, aliyowahi kuiangalia miaka mingi kabla, alihisi watu wale walikuwa Wavietnam! Alishtuka na kuogopa zaidi alipokumbuka jinsi walivyowaua maaskari wa Kimarekani katika filamu hiyo.
Watu wasiopungua mia tano waliizunguka ndege ya akina Caroline na wengine ishirini kati yao walisogea mbele kuwafuata Caroline na Harry mahali walipolala,walivuta pinde zao kama watu waliokuwa wakisubiri amri ili waachie mishale iliyokuwa katika pinde hizo!Kwa haraka haraka alipohesabu Caroline alikadiria mishale isiyopungua kumi na moja ingeingia mwilini mwake, alilia kwa uchungu na alipomwangalia Harry aligundua alikuwa hajitambui tena.
“Hogree magrii tanui!” Caroline alisikia sauti hiyo kutoka kwa mtu mwenye ndevu nyingi aliyesimama nyuma ya watu hao ishirini, wakazidi kuzivuta pinde zao! Akajua mwisho wa maisha yake umefika.
***************
Dakika ishirini na tano baada ya ndege ya Caroline kuruka kutoka Miami, ndege ya Dk. Ian ilitua ufukweni na kupokelewa na Thomson pamoja na wafanyakazi wengine! Dk. Ian alikuwa akilia machozi na rangi ya ngozi yake ilibadilika kwa sababu ya hasira, mmoja wa wafanyakazi alishangaa kumwona Dk. Ian akilia, tangu aanze kazi kisiwani hapo hakuwahi hata siku moja kumwona Dk. Ian akilia, hakuwa kufikiri iko siku angeyaona machozi ya mtu tajiri kama huyo.Sababu ya mambo hayo alijikuta akitabasamu! Hakutegemea Dk. Ian angemwona lakini bahati mbaya alikishuhudia kitendo hicho.
Kwa hasira aliyokuwa nayo alimgeukia kijana huyo na kuanza kumuuliza maswali ni kitu gani kilimfanya acheke katika kipindi hicho cha majonzi!
“Why are you laughing you sonofabitch! Do you think I want to buy your teeth?”(unacheka nini wewe mtoto wamalaya! Unafikiri nataka kununua meno yako?) Aliuliza Dk. Ian kwa hasira.
Kila mfanyakazi aliyekuwepo uwanja wa ndege aligundua hasira aliyokuwa nayo Dk. Ian, wote walitetemeka kusikia akimtukana mwenzao kiasi hicho na hawakujua ni kitu gani kingempata, bila kuchelewa kijana huyo alianguka miguuni kwa Dk. Ian na kuanza kumlamba miguu akimwomba msamaha.
“Forgive me sir! You are the most respected man on the planet, I didnt intend to make you annoyed!”(Nisamahe bwana! Wewe ndiye mtu unayeheshimika zaidi duniani, sikufanya makusudi kukukasirisha!) Alisema kijana huyo lakini badala ya Dk. Ian kumsamehe alichomoa bastola yake mbavuni na kummiminia risasi zisizo na idadi damu nyingi zikamtoka, baada ya shughuli hiyo Dk. Ian alianza kutembea kuondoka eneo hilo.
“Burry his body immediately, Thomson come with me to my house for a meeting! Where is Caroline’s plane?”(Ufukieni mwili wake haraka wewe Thomson nifuate kwenye nyumba yangu ili tufanye mkutano! Iko wapi ndege ya Caroline?)
“They left twenty minutes ago!”(Wameondoka dakika ishirini zilizopita!)
“To?”(Kwenda wapi?)
“They said goodbye to nobody!”(Hawajamuaga mtu!)
“These people are tired of living! they cant get out of my hand, why didnt you kill them”(Watu hawa wamechoka kuishi! hawawezi kunitoroka mimi! Kwanini hukuwaua) Alisema Dk. Ian kwa hasira huku machozi yakimtoka! Siku hiyo hata Thomson alitishwa na hali aliyokuwa nayo tajiri yake hata siku moja hakuwahi kumwona Dk. ian akiwa na hasira kiasi hicho.
“I hastated!”(Nilisita!) Alijibu Thomson akimfuata Dk. Ian kwa nyuma.
Je nini kitatokea? Harry amekufa? Na nini kitatokea mahali walipo Harry na Caroline? Watu gani wamewateka? Je, Dk. Ian atafanikiwa kuwapata? Fuatilia wiki ijayo.
S
iku hiyo hiyo Dk. Ian aliitisha
mkutano wa haraka na
kuanza kugawa majukumu ya kuwasaka Caroline na Harry popote walipokimbilia duniani, aliamini wasingeukwepa mkono wake uliosambaa dunia, kupitia mtandano wa Mafia!
“Nilijitoa Mafia sasa narudi sababu ya hawa mbweha wawili na nitawapata tu!” Alifoka kwa hasira Dk. Ian mbele ya wafanyakazi wake waliokusanyika ndani ya nyumba yake, hali ilikuwa mbaya na ilimtisha karibu kila mtu aliyekuwepo katika mkutano huo, wafanyakazi wote hawakuwahi kumwona Dk. Ian akiwa amekasirika kiasi hicho. Walishindwa kuelewa ni nini kingewapata Caroline na Harry kama wangekamatwa.
“Yaani kweli Caroline pamoja na wema wote niliomfanyia amenitoroka tena na ndege niliyomnunulia mwenyewe kwa mamilioni ya dola? Haiwezekani lazima nimpate! Na siku akipatikana nitamchinja kwa mkono wangu mwenyewe!”
“Usijali mzee, atapatikana wala usiwe na wasiwasi hiyo sisi ni kazi yetu!”
Baada ya mkutano huo Dk. Ian alipiga simu kwa kila mwakilishi wa Mafia katika mabara yote duniani, akianzia na Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Asia, Ulaya, Afrika na mengine na kuwajulisha kuwa alikuwa amerejea tena rasmi katika Umafia na alitaka watu waliotoroka na ndege yake wakamatwe haraka iwezekanavyo na kuuawa bila serikali ya nchi yoyote kufahamu!
“Sitaki muwataarifu polisi, kazi hii haitushindi, watafutwe kimya kimya hadi wapatikane, ikibidi kuilipua ndege wote wafe hata hivyo ndege ikiungua siyo tatizo sana kwangu!”
“Sawa bosi!” Ndiyyo alivyoitikiwa na karibu kila mtu mwakilishi aliyempigia simu.
Dostları ilə paylaş: |