Sababu ya kumpiga tunayo! Nia ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga Nduli Idi Amin tunayo, ni lazima tumpige!



Yüklə 0,95 Mb.
səhifə11/18
tarix31.10.2017
ölçüsü0,95 Mb.
#23549
1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   ...   18

Msako huo haukutangazwa katika chombo chochote cha habari wala polisi hawakufahamishwa juu ya kutoroka kwa Caroline na Harry, hivyo ndiyyo Mafia walifanyavyo kazi zao! Wakuu wa mabara wa Mafia waliwataarifu wakuu wa nchi mbalimbali juu ya msako huo na katika muda wa masaa 12 tayari taarifa hizo zilishafika katika kila nchi duniani.

Mawakala wa Mafia katika viwanja vyote vya ndege walikuwa na taarifa hiyo, kila ndege iliyoingia katika viwanja vyote dunia nzima ilirekodiwa na taarifa zilitolewa makao makuu ya Mafia, huko Milano Italia na baadaye kupelekwa kwa Dk. Ian ambaye tayari alisharudi Canada kutulia akisubiri taarifa, hasira yake ilizidi kuongezeka kadri dakika zilivyozidi kusonga mbele bila Caroline na Harry, alikuwa na hamu kubwa ya kuwapata na kuwaonyesha yeye alikuwa ni mtu wa aina gani.

“Nitamuua vibaya sana huyu mwanamke na hata huyo mwanaume wake nilishaacha kuua lakini sasa narejea!”

Kila mara Dk. Ian alijiuliza ni kitu gani ambacho Caroline alikikosa kwake mpaka kuamua kutoroka na rubani aliyempa kazi yeye mwenyewe, kwake ilikuwa ni aibu kubwa kushindwa na mfanyakazi wake.

“Hivi huyu Harry ni nani mpaka aninyang’anye mimi mwanamke niliyempenda kiasi hiki?” Aliwaza Dk. Ian kisha akanyanyuka na kwenda kwenye kabati ambako alichukua faili lenye maelezo ambayo Harry aliyatoa wakati wa kutafuta kazi ya Urubani kwenye kampuni yake! Aliyasoma hadi mwisho lakini alionekana kutoelewa kitu chochote, wazo lilimwijia kichwani na kuamua kuwapigia simu watu wa kituo cha upepelezi binafsi cha Investigation& Scrutiny Centre.

“Hallow!”

“Yeah!”

“Can I help you?”(Naweza kukusaidia?)



“ Can I speak to the boss!”(Naweza kuongea na bosi wako?)

“Hold on!”(Subiri!)

Dakika kama mbili baadaye Dk. Ian alisikia sauti nzito kutoka upande wa pili, alipojitambulisha mtu aliyepokea alionekana kutetemeka, alionyesha wazi hakuwahi kupokea simu kutoka kwa mtu tajiri kama Dk. Ian.

“Dr. Ian the Rich?”(Dk. Ian tajiri?)

“Yeah!”(Ndiyo!)

“What can I do for you sir?”(Nikusaidie nini mzee?)

“I just need to know the depth of one person!”(nataka kujua undani wa mtu mmoja!)

“Name him and we shall tell you everything in a minute!”(Tutajie ni nani na tutakueleza kila kitu juu yake katika muda wa dakika moja!)

“Harry Robertson!”(Ni Harry Robertson!)

“His profession?”(Kazi yake?)

“A pilot!”(Ni rubani!)

“Give me ten minutes sir and I will get back to you with every information that you need!”(Nipe dakika kumi nitakupigia!)

“Ok!”(Sawa!) Dk. Ian alijibu na kukata simu.

Hazikutimia dakika kumi, kilikuwa ni kiasi cha kama dakika saba tu baadaye simu ikaita, Dk. Ian hakutegemea kama simu hiyo ingeweza kuwa inatoka kampuni ya upepelezi ya Investigation& Scrutiny Centre, alipoipokea alishangaa na kukutana na sauti nzito aliyoongea nayo mara ya mwisho!
”Yes! We have found him!”(Ndiyo tumempata!)

“Sure? Then tell me about him!”(Hakika? Basi niambieni kila kitu juu yake!)

“He was born Tanzania 28 years ago, went to school in the same country, he later joined a university where he did his pilot course, he was employed by the following companies USD Airlines as a pilot, quit the job and eventually employed by you a few days ago!”(Alizaliwa Tanzania miaka 28 iliyopita, alisoma katika nchi hiyo hiyo, lakini baadaye alijiunga na chuo kikuu ambako alisomea mambo ya uendeshaji wa ndege, amefanya kazi katika kampuni ya USD Airlines na baadaye aliacha kazi na hatimaye ameajiriwa na wewe siku chache zilizopita!)

Dk. Ian hakuyaamini masikio yake, halikuwa jambo rahisi hata kidogo taarifa za watu kupatikana kirahisi kiasi hicho! Alishindwa kuelewa watu hao walifanya kazi namna gani, ni kweli aliyekuwa akiongelewa alikuwa ni Harry! Ni baada ya maelezo hayo ndiyo jina Harry lilifunuka katika kumbukumbu zake, alikumbuka kumsikia mke wake akilitaja mara kwa mara! Alihisi ni Harry huyo huyo ndiye alitoroka na mke wake baada ya kuwakutanisha alipompa kazi kama rubani.

“Lazima watakuwa wanafahamiana, wote waliishi Tanzania! Haiwezekani lakini nitawapata tu!”

***********

Ndege ya Caroline ilitafuwa kila kona ya dunia bila kupatikana, haikuonekana katika mitambo ya setilaiti pamoja na Rada, Mafia walishindwa kuelewa mahali Harry na Caroline walipojificha, Dk. Ian alizidi kuchanganyikiwa. Ilikuwa si rahisi kuwaona katika mitambo kwani ndege yao ilikuwa katikati ya msitu ya Cambodia, na walikuwa chini ya ulinzi mkali wa Wavietnam!

Walikuwa wakihojiwa na maongezi kati yao yalikuwa si ya kuelewana kwa sababu kila mtu hakuielewa lugha ya mwenzake vizuri, Caroline na Harry waliongea kiingereza lakini Wavietnam nao waliongea lugha yao, katika kile kilichoonekana kama amri kutoka kwa mkubwa wao walifungwa kwa kamba na kuning’inizwa mitini vichwa chini miguu juu na viboko vilianza kupita miilini mwao! Walilia kupita kiasi kufuatia mateso hayo, waliachwa mtini kwa karibu saa nzima wakiteseka.

“Harry unaona sasa uliyoyasababisha?”

“Nisamehe Caroline, hata hivyo huu si muda muafaka wa kutupiana lawama!”

“Bila wewe haya yote yasingetokea Harry!”

“Sawa laki……!”Kabla hajamaliza Harry sentensi yake Harry alishtukia kiboko kikipita katikati ya mgongo wake.

“Hey! Where are you from? Are you Americans?”(He! Nyie ni akinanani? Nyie ni Wamarekani?)

Wavietinam waliwachukia sana Wamarekani na hilo wote wawili walilielewa vizuri, kama wangediri kutamka walikuwa Wamarekani mbele ya Mvietnam huo ndio ungekuwa mwisho wa maisha yao! Walishangaa kusikia sauti ya mtu akiongea Kiingereza lakini iliwapa matumaini kuwa angalau sasa wangeweza kujieleza vizuri.

“Answer my question are you Americans?”(Jibu swali langu nyie ni wamarekani?)

“NO! No! We’re not!”(Hapana! Hapana! sisi sio!)

“Who are you?”(Nyie ni akinanani?)

“We are Canadians can’t you see the mark on the plane?”(Sisi ni Wacanada huoni alama kwenye ndege yetu!?)

“You’re lucky to be Canadians other wise…….!”(mna bahati kuwa wacanada vinginevyo……!) Alisema mtu huyo na baadaye kuongea lugha ya Kivietinam ambayo Harry na Caroline hawakuielewa lakini walishtukia wakifunguliwa kamba na kushushwa kutoka mtini na kulazwa chini , baadaye walibebwa juujuu na kupelekwa hadi kwenye kibanda kilichokuwa karibu kabisa na eneo hilo ambako kupewa uji, miili yao haikuwa na nguvu kabisa lakini baada ya kunywa uji huo walijisikia vizuri. Mzee mmoja mwenye ndevu nyingi aliingia na kuanza kuwapaka vitu kama kinyesi cha ng’ombe katika vidonda walivyokuwa navyo miguuni, siku hiyo hawakutoka ndani ya kibanda hicho kilichooneka kuwa mahabusu walilala bila kusemeshana hadi usiku wa manane Caroline alipomwamsha Harry aliyekuwa akikoroma usingizini.

“Harry tafadhali hebu nieleze ukweli tutaondokaje mahali hapa?”

Harry alikaa kimya kwa muda wa kama dakika tatu bila kujibu kitu, alionekana kuwa katika mawazo Fulani.

“Harry niambie tutaondoka vipi hapa?”

“Tutaondoka tu ila tunahitaji kupanga mikakati!”

“Ipi?” Caroline aliuliza.

“Mpaka sasa sijaifahamu ila tutaondoka!”

“Na ndege?”

“Ndiyo kwanini tuiache ndege yetu?”

Usiku huo wa manane waliongea mengi juu ya maisha yao, hofu ya Caroline juu ya Dk. Ian bado iliendelea kumsumbua pamoja na Harry kumtia nguvu, alijua siku moja ni lazima angeiingia mikononi mwake na kuuawa kikatili! Upande mwingine wa moyo wake ulijaa majuto lakini hakutaka kumwonyesha Harry hali hiyo.

“Nimekwishakueleza kuwa Dk. Ian hatatupata hata kitokee nini! Tatizo lako wewe huniamini, kwanza tukitoka hapa kazi yetu ya kwanza itakuwa ni kubadilisha hizi sura zetu na ndege tutaiuza na kupatka mamilion ya dola tunaweza hata kuamua kurejea Tanzania, nina ndoto za kuwa Rais wa nchi hiyo kama ikitokea nikawa na pesa baada ya hapo Dk. Ian atanikamata vipi wakati nitakuwa nalindwa na dola?”

“Kweli? Lakini mbona unajiongelea mwenyewe wakati tuko wawili?”

“Samahani nilipitiwa”

***************

Asubuhi kulipokucha wote wawili waliwaamshwa na kuwapelekwa mbele ya kiongozi wao aliyeitwa Wung huko walihojiwa maswali mengi juu yao na kurudishwa tena katika kibanda chao ambako walifungiwa na kuendelea kuhudumiwa kwa kla kitu, kwa wiki nzima walibaki katika mahabusu ndani ya kambi ya Vietnam! Ilionekana hapakuwa na namna yoyote ambayo wangeweza kujiokoa, hawakuruhusiwa kutoka katika chumba chao usiku na mchana! Caroline alichoka kukaa ndani alitaka kuwa huru, walikuwa ni kama wafungwa.

************

Ulikuwa ni usiku wa manane Caroline akiwa usingizini, aligutuka na kitu kilichokuwa kikichimba ardhi jirani kabisa na mahali alipolala! Alinyanyuka haraka na kukaa, alishangaa kukuta aliyekuwa akichimba chini ni Harry.

“Vipi tena?

“Natafuta njia ya sisi kuondoka hapa! Nimeona huu mpango unafaa!”

“Mpango gani?”

“Nitachimba hapa ukutani kisha tutatoka hadi nje na kutambaa hadi tulipoiacha ndege na kuondoka zetu, nina uhakika hawatakuwa na uwezo wa kuitungua ndege yetu, ninajua nitakavyoendesha na hawatawahi kabla hatujaondoka!”

“Harry watasikia wakati ikinguruma!”

“Wewe usijali nitakuonyesha jinsi ya kufanya kazi hiyo niachie mimi!”

Aliendelea kuchimba akisaidiwa na Caroline lakini hawakufanikiwa kuutoboa ukuta siku hiyo kwa sababu hakuwa na vitendea kazi nzuri, Harry alitumia kipande cha mti alichokikuta ndani ya kibanda hicho wakati nyumba ilikuwa na ukuta mnene, kulipokucha aliacha lakini usiku ulipoingia aliendelea na kazi yake. Kwa siku mbili alifanya kazi hiyo wakisaidiana na Caroline, siku ya tatu walifanikiwa kuutoboa ukuta ilikuwa ni kati kati ya usiku watu wote wakiwa wamelala.

“Sasa?”


“Ni wakati wa kuondoka lakini wewe baki kwanza nikaangalie hali huko nje, nitarudi kukushtua!”

“Sawa darling!”

Caroline kwa kupitia tundu la ukutani alimshuhudia Harry akitambaa kwa tumbo na kupotelea gizani, alikaa kimya akimsubiri Harry arudi na alimwombea kwa Mungu afike kwenye ndege na kurudi salama ili wapate kuondoka, alitaka kuondoka Vietnam hakutaka kufika mahali pale.

Kwa saa nzima hakumwona Harry akirejea, alianza kuingiwa na wasiwasi kuwa pengine alikuwa amekamatwa. Baadaye alishtuka aliposikia ndege ikiunguruma kwa kasi ya ajabu! Kisha zilifuata kelele za watu wengi wakikimbia kuelekea uwanjani, Caroline hakuyaamini masikio yake alipoisikia ndege ikiunguruma mawinguni alishindwa kuelewa kama kweli ilikuwa ikiondoka au la!

Kwa kupitia katika tundu lilelile alitoka nje bila hata woga na kukimbia kuelekea uwanjani, hakwenda hata hatua kumi mbele yake akawa ameingia mikononi mwa walinzi watatu wa Kivietnam, walianza kumshambulia na kurejeshwa moja kwa moja katika kibanda cha mahabusu na kumfungia, walinzi walipoliona shimo ukutani walielewa kilichotokea lakini walishindwa kuelewa ni kwanini Harry aliamua kutoroka peke yake akimwacha Caroline mahali pale.

Carolne alilia hadi asubuhi, hakutaka kuamini kama kweli Harry alikuwa amemtoroka na kumwacha mikononi mwa Wavietnam! Huo ulikuwa uuaji, alijilaumu kwa kila kitu alichokifanya ni kweli alikuwa meyaharibu maisha yake mwenyewe, aligundua Harry hakuwa na mapenzi ya dhati, alikwenda kwake kuharibu maisha tu na si kingine, alijuta na kuendelea kulia, hakujua ni kitu gani kingempata kutoka kwa Wavietnam kwa kosa la kutoroka kwa Harry.

Mwanga wa jua ulipoingia ndani ya nyumba yake asubuhi kitu cha kwanza alichokigundua ndani ya nyumba ni kipande kichafu cha karatasi kilichokuwa juu ya udongo, kilikuwa na maandishi juu yake, alikichukua na kukinyoosha taratibu! Ulikuwa ni mwandiko wa Harry, ingawa uliandikwa vibaya, ilivyoonekana maandishi yaliandikwa kizani.

Caroline nasikitika kwa yote yaliyotokea najua Wavietnam watakuua, lakini hicho ndicho nilichokitaka na ndiyo maana nikakuleta hapo, nilichohitaji ni ndege na tayari nimeipata na ina wateja wanaoisubiri nchini Kenya na baada ya hapo nitaendelea na maisha yangu bora na ya starehe, nyumbani Tanzania ambako nitaitimiza ndoto yangu ya kuwa Rais! Pole sana kwa mateso utakayoyapata na kwa kukuharibia maisha yako!

Caroline hakuweza kuimalizia barua hiyo, alianguka chini na kuanza kulia machozi, mara ghafla mlango ulifunguliwa wakaingia wanaume wawili na kuanza kumburuza hadi nje ambako alibebwa juu juu hadi mahali kwenye uwazi na kuanza kufungwa kwenye mti! Alijua huo ndio mwisho wake alilia akiomba angalau muujiza utokee! Alimkumbuka Dk. Ian na wema wake.



Je nini kitaendelea? Harry atafanikiwa kufika na ndege yake Kenya wakati msako mkali unaendelea? Je nini kitampata Caroline huko Vietnam?

Fuatilia wiki ijayo

Paaa!Tchaaa!Tchaaa!”

“Mungu wangu weee!”

Ilikuwa ni mijeledi iliyotua katika mwili wa Caroline, akipigwa na wanajeshi wa Kievetnam ili aseme mahali alikokimbilia Harry! Caroline alilia akiwaeleza wazi hakuwa na jibu la swali hilo, lakini hakuna aliyeelewa, alizidi kuchapwa na Wavietnam bila huruma! Yalikuwa mateso makubwa mno kwake, damu zilimtoka karibu mwili mzima, alilia akimlaumu Harry kwa uamuzi wake wa kumteka na kumtelekeza porini mikononi mwa wauaji! Kwa hakika alikuwa amemharibia maisha yake yote, moyoni alijuta kumwacha Dk. Ian kwa ajili ya mtu ambaye hakumpenda hata kidogo, aliulaumu moyo wake na hakuwa tayari kumsamehe Harry tena milele.

“Kama hawataniua hapa ni lazima nimuue Harry siku moja, amerejea tena katika orodha ya watu niliotaka kuwaua! Nilishamfuta lakini sasa amerudi! Kitendo alichonifanyia sitakisahau maishani mwangu! Labda nife lakini nikipona…..atakuja kujuta ni kwanini amenifanyia hivi!” Alisema Caroline huku akilia, Wavietnam wale hawakuelewa alichokisema walizidi kumshushia mvua ya mijeledi wakitaka asema ukweli ambao hakuujua hata kidogo!

Mpaka saa moja jioni aliendelea kufungwa kwenye mti huo akichapwa! Karibu masaa yote alichapwa ni muda mfupi sana aliopumzishwa, kwa hakika alijua kifo chake kilikuwa kimefika! Aliikumbuka Tanzania na aliwakumbuka sana wazazi wake, alisikitika kufia katika nchi ambayo hata maiti yake wasingeiona, aliamini wangeendelea kujua alikuwa hai sehemu fulani wakati tayari alishakufa muda mrefu, mawazo hayo yalifanya machozi yazidi kumtoka zaidi.

Baadaye alichoka na kulegea kiasi cha shingo yake kuangukia pembeni, walipoona hivyo Wavietnam walijua angekufa na kwa amri ya mkuu wa kambi walimfungua na kwenda kumtupa tena katika kibanda ambacho yeye na Harry waliwekwa rumande mwanzo! Alilala sakafuni huku damu zikiendelea kumtoka, hakuwa na mtu mwingine wa kumlaumu zaidi ya Harry kwa mateso yote aliyoyapata, alitamani hata kukutana na Dk Ian tena na kumwomba msamaha ingawa alijua alikuwa mtu hatari!

“Labda anaweza kunipa msamaha, kama nikimlilia na kumwangukia miguuni na kumwambia rubani aliyenipa aliniteka na kunileta porini! Kwa hali niliyonayo nafikiri anaweza kuamini!”

Aliwaza Caroline lakini hakuwa na uhakika kama alichokiwaza kingeweza kumsaidia, aliona bora kukutana na Dk. Ian kuliko kuendelea kuwa mikononi mwa Wavietnam waliomtesa kiasi hicho kwa sababu ya kitu ambacho hakukielewa kabisa! Kwa hakika hakuelewa mahali alikokuwa Harry lakini alilazimishwa aseme.

Aliachwa alale chini bila kujigeuza akiwa katika maumivu makali hadi asubuhi alipozinduliwa usingizini na mzee wa Kivietnam, alimkumbuka mzee huyo, ndiye aliyewatibu yeye na Harry walipopatwa na matatizo mara ya kwanza. Alimnyanyua na kumkalisha kitako, kisha akachukua ndoo ya maji iliyokuwa karibu yake, akamwaga dawa nyeusi ndani yake kisha akaanza kumwogesha nayo mwilini! Alipomaliza alimlaza juu ya majani ya mgomba yaliyotandikwa chini!

Hakusema naye kitu chochote sababu walikuwa hawaelewani lugha! Baada ya kumaliza mzee huyo aliondoka lakini alirudi tena mchana na jioni kufanya kitu hichohicho na kiliendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu, Caroline alishangaa kuona akirejea katika hali yake ya zamani! Vidonda vyake vilianza kupona na mwili wake kupata nguvu, matumaini ya kupona yalirejea, katika muda wiki nzima alikuwa amepona kabisa ingawa mwili wake bado ulikuwa na makovu mengi makubwa! Hata siku moja hakuruhusiwa kutoka nje ya kibanda! Alikuwa ni kama Simba ndani ya kijumba chake, alipewa chakula mara moja tu kwa siku na watu wawili walimlinda mchana na wengine wawili walimlinda usiku! Alikuwa katika mateso makali, alimtupia lawama Harry, hakutegemea angetenda kitendo cha kinyama kiasi hicho!

**********

Ilikuwa ni usiku wa manane akiwa amelala usingizi ndani ya kibanda chake, ilikuwa ni siku ya tano tangu apate nafuu, aliamshwa usingizini na kelele za vyuma vya mlango wa kuingilia katika kibanda hicho vilivyokuwa vikifunguliwa, alishtuka kwa sababu hata siku moja hakuwahi kuamshwa usiku kiasi hicho! Hali ilikuwa kimya kupita kiasi, hata ndege hawakulia, hiyo iliashiria ulikuwa ni usiku wa saa nane ama saa tisa hivi! Alitetemeka mwili mzima.

Aliingia askari akiwa na tochi mkononi na kumulika mahali alipolala Caroline, akamshika mkono na kuanza kumburuza kwenda nje bila kusema neno lolote, huko nje aliungana na mwenzake wote wawili walimbeba juu juu kwenda naye upande wa pili wa kambi! Alijaribu kupiga kelele lakini alizibwa na mkono kwa kiganja cha mkono wa mmoja wa walinzi hao wa Kivietnam kuifanya sauti yake isifike mbali.

Alitupwa chini katikati ya vichaka viwili na askari mmoja alimshika mikono na mwingine kwa kutumia miguu yake akamgandamiza miguu! Caroline alijua kilichotaka kutokea! Ni kitu ambacho alikiogopa sana maishani mwake, aliamini walitaka kumbaka! Ghafla askari aliyemgandamiza mguu kwa kutumia mkono wake wa kushoto aliivua nguo yake ya ndani na kuichana kisha akalishika gauni lake na kulifunua akiliacha limfunike usoni na kuziacha sehemu zake za siri wazi.

“Mungu wangu! Eh Mungu wangu nisaidie! Wananiua!” Caroline hakuwa na mtu mwingine wa kumlilia, isipokuwa Mungu peke yake kwa maumivu makali yaliyompata akifanyiwa kitendo hicho cha kikatili, yalikuwa ni maumivu yasiyoelezeka! Alilia lakini walinzi hao hawakusikiliza, alipomaliza mmoja alimwachia mwenzke wakiwa wamebadilishana, ilifanyika shughuli ya masaa mawili ndipo wakamrejesha tena katika kibanda chake saa 11 alfajiri, akilia machozi, alikuwa amebakwa! Kilikuwa kilio kingine kwake na alitamani kufa kuliko kuishi.

Vitendo hivyo havikukomea siku moja, viliendelea kumtokea Caroline karibu kila baada ya siku moja, akawa mtumwa wa mapenzi! Ilikuwa ndiyo njia pekee ya maaskari wa Vietnam kujifurahisha, hawakuwa na wasichana katika kambi yao, mimba yake ilizidi kukua lakini hawakujali, kila siku walimtendea unyama huo! Kwa miezi karibu mitano aliendelea kufanyiwa hivyo.

Baadaye aligundua kuwa sehemu zake za siri zilikuwa vikivuja majimaji machafu yenye harufu mbaya, aligundua tayari alishapata gonjwa la zinaa! Hakujua hata alilipata kwa nani maana wanaume wengi waliomwngilia kwa nguvu walikuwa wengi! Hakuna mwanaume hata mmoja aliyejali kuugua kwake kila siku waliendelea kumfanyia, alikuwa ni kama mateka asiye na kimbilio.

***************

”Wewe malaya kwanini umeniambukiza ugonjwa wa zinaa?” Askari mmoja alimuuliza kwa lugha yao.

“Mimi?”

“Ndiyo, kwani nani?”



“Sio mimi afane ni nyie mlioniambukiza ugonjwa huu na hatimaye umesambaa kwenu wote, mimi sikuja hapa na ugonjwa wowote! Vitendo vyenu vya kikatili ndivyo vimenipa matatizo haya, tafadhali nitafutieni tiba!” Alisema Caroline katika sauti ya kukata tamaa!

“Unajibu jeuri siyo?”

“Hapana siyo hivyo afande!”

“ Leo nitakufundisha adabu!”

Kilichofuata baada ya hapo kilikuwa ni kipigo tu si kutoka kwa askari huyo peke yake bali aliendelea kupata vipigo kutoka kwa kila askari aliyembaka kwa madai kuwa aliwaambukiza ugonjwa wa zinaa! Kitu ambacho Caroline alikuwa na uhakika kabisa hakukifanya, alijitahidi kujieleza kwao lakini hawakujali walichofanya ni kumpiga kila siku. Ni askari mmoja tu ambaye hakudiriki kumpiga, Caroline alishangaa ni kwanini! Mara nyingi askari huyo alikuwepo kujaribu kuwazuia wenzake wasifanye hivyo.

“Caroline!” Mlinzi wa usiku alimwita katikati ya usiku, alikuwa ni mlinzi mpole ambaye hakumpiga kati ya wote waliombaka.

“Naam afande!” Alijibu Caroline kwa Kivietnam kutoka kwenye kibanda chake.

“Kwanza pole sana kwa yanayokupata!”

“Ahsante, nashukuru wewe hujanipiga!”

“Unajua kwanini sijakungusa?”

“Hapana!”

“Ni mimi niliyekuambukiza ugonjwa Caroline, kwa sababu hiyo nimepanga mpango kamambe wa kukutorosha, nimeongea na askari mwenzangu wa kambi yetu ya Kahtar! Atakuwa anatusubiri porini usiku wa leo, nitakukabidhi kwake nae atakupeleka kwa mwingine katika kambi ya Zentilio huyo atakusogeza mbele zaidi ambako utakabidhiwa kwa mwingine atakayekufikisha hadi barabarani, huko utapanda basi litakalokufikisha Phnom ambako utatafuta njia yoyote ya kuishi, ukibaki hapa nina hakika utakufa!

“Nitaweza kweli kusafiri umbali wote huo na hii hali yangu ya ujauzito? Kwani jumla zitakuwa ni kama kilometa ngapi?”

“Kilometa 105!”

“Sidhani kama nitaweza jina lako ni nani kweli?”

“Hung!”


“Hung hakuna utaratibu mwingine wa kusafiri?”

“Sina na ninaomba utoke haraka ili tuondoke ni bahati leo nalinda peke yangu, nimekuonea huruma sana Caroline, nipo tayari kufa ili nikuokoe”

“Kweli?”

“Ndio naomba utoke tuondoke!”

Tumbo la Caroline lilikuwa kubwa mno, alikuwa mzito kufanya karibu kila kitu, alijikongoja taratibu na kusimama wima kisha akatoka hadi nje, kila upande wa kambi ulitawaliwa na giza nene! Hung hakutaka kutumia tochi kwa kuogopa kuonekana, alimwambia wainame na kunyata taratibu hadi nje ya ngome kwa kupitia chooni! Hakuna mtu aliyemwona!

“Caroline itabidi ujitahidi sana kutembea sababu ni lazima nihakikishe asubuhi nimerudi hapa!”

“Nitajitahidi ingawa mimba inanipa uzito!” Aliitikia Caroline ingawa alijua wazi asingeweza, alikuwa tayari kufia mahali popote mbele ya safari lakini si kusubiri kifo chake katika kijumba cha mahabusu!

Walitembea kwa karibu masaa manne wakipita katikati ya pori na milima, wakipishana na wanyama wakali, mahali aliposhindwa kupita Caroline hasa katika mito, Hung alimbeba mgongoni na kumvusha, Caroline alichoka lakini alijitahidi kadri ya uwezo wake hakuwa na namna nyingine yoyote ya kujiokoa, saa nzima baadaye akiwa hoi walifika eneo la wazi katikati ya pori na kukaa chini, hata Hung alionekana kuwa amechoka hoi bin taaban.

Muda mfupi tu baadaye alitokea mtu aliyevaa nguo nyeusi mwili mzima na kwenda hadi mahali walipokaa Caroline na Hung na kuwasalimia katika lugha ya Kivietnam wote wakaitikia, Caroline alikuwa tayari kalala chini, maumivu ya mgongo na tumbo yalimsumbua kupita kiasi!

“Xun, huyu ni Caroline ndiye niliyekueleza habari zake katika simu ya upepo naomba umsaidie kufika Zentilio, tafadhali fanya hivyo kwa heshima iliyopo kati yangu mimi na wewe na Mungu atakusaidia!”

“Sawa nitafanya hivyo bosi!” Alijibu Xun kijana mrefu mwembamba huku akimnyanyua Caroline aliyekuwa akilalamika maumivu ya tumbo ili asimame wima waondoke!

“Siwezi! Siwezi!” Alilalamika Caroline.

“Hapana Caroline ni lazima ujitahidi tu, ni lazima Xun ufanye jambo hili usiku na asubuhi awepo hapa!” Hung alisema.

“Sawa Hung! Nashukuru kwa msaada wako lakini sijui kama nitafika nina wasiwasi nitafia njiani! Tumbo linaniuma mno!”

“Hapana utafika!” Alijibu Hung na kuingiza mkono wake mfukoni akatoa noti moja ya dola mia na kumkabidhi.

“Ahsante!”

“Hiyo itakusaidia huko unakokwenda, nimeitunza kwa muda mrefu, najua mjini utaibadilisha na kuitumia kutibiwa hospitali! sawa?”

“Sawa!Mungu akubariki!”

Caroline akawa ameingia mikononi mwa mwanajeshi mwingine, aliyekuwa na nguvu mpya! Yeye akiwa na nguvu ileile na zaidi ya hayo aliumwa tumbo kupita kiasi! Alimshuhudia Hung akiondoka, pamoja na kuwa alimbaka na kumsababishia ugonjwa alimshukuru kwa kuokoa maisha yake, machozi yalimtoka kutengana na mtu ambaye kwa hakika asingemwona tena maishani, hakuwa na uhakika wa kufika safari waliyokuwa wakienda.

***************

Walitembea umbali wa kama kilometa saba porini, tumbo liliongezeka maumivu mara mbili zaidi, lilimnyonga sana sehemu za chini ya kitovu chake na liliuma na kuachia! Lilipoachia alitembea lakini lilipoanza aliinama kwa maumivu yaliyompata, nguvu zilianza kumwishia miguuni na kumfanya ashindwe kutembea akiwa amenyooka.


Yüklə 0,95 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   ...   18




Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2024
rəhbərliyinə müraciət

gir | qeydiyyatdan keç
    Ana səhifə


yükləyin