Sababu ya kumpiga tunayo! Nia ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga Nduli Idi Amin tunayo, ni lazima tumpige!



Yüklə 0,95 Mb.
səhifə17/18
tarix31.10.2017
ölçüsü0,95 Mb.
#23549
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   18

Je, nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.

D

k. Colins Wiliamson 
hakuwa mtu maarufu 
masikioni mwa watu wengi wa Jiji la Ottawa, Canada. Hiyo ilitokana na ukweli kwamba juu ya utajiri wake lakini alitumia muda wake mwingi katika mashamba yake yaliyokuwa katika misitu ya Great jambo lililofanya aonekane mara chache sana katika maeneo ya mjini ambapo alikuwa anamiliki kiwanda cha maua na huko msituni alikuwa na kiwanda cha kuchana mbao.



Akiwa ni mtu mzima mwenye nywele na ndevu nyeupe, Dk. Wiliamson alikuwa ni mtu mwenye msimamo sana na maisha yake tangu alipomaliza kesi yake iliyomfanya apoteze eneo kubwa la shamba lake. Hilo lilikuwa ni jambo kubwa lililomfanya awe na uchungu sana kitendo kilichomfanya atumie muda mwingi kuwaza na kupangilia upya maisha yake baada ya nusu ya utajiri wake kuporwa kwa hila.

Ni mkulima ambaye alikuwa akitegemewa sana kutokana na misitu anayomiliki kutoa mbao kwa wingi ambazo zilihitajika kwa shughuli mbalimbali. Shamba kubwa na ambalo nusu yake iliporwa ni lile lililokuwa katika misitu ya ziwa la Great ambalo liko ndani ya mji wa Ottawa mpakani na Marekani hasa katika mji wa New York. Mbali na shamba hilo la miti karibu na ziwa hilo, pia alikuwa na mashamba mengine ya aina hiyo kando ya maziwa maarufu ya Winnipeg na Galgary.

Biashara zake za mbao alizifanya pia katika nchi jirani za Marekani na Mexico na hivyo kuingiza kipato kikubwa ambacho ndicho kilichomwezesha kununua kiwanda cha kuchana mbao ambacho alikitumia vilivyo na hivyo kuzidi kujitajirisha.

Mzee Wiliamson alikuwa na mke na watoto wanne ambao wawili kati yao walihamishia maisha yao Marekani na waliobaki ambao ni watoto wa kike wawili alikuwa akiishi nao hapo hapo kwake.

Shamba lake lilikatwa kinguvu baada ya kushindwa kesi! Karibu nusu nzima ya shamba hilo ilimegwa na Dk. Ian ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa baada ya kufanya hila na kufoji hati kadhaa za mashamba hayo na kisha kudai kwamba eneo la shamba ni mali yake. Ijapokuwa hilo jambo lilifanyika miaka mingi iliyopita, lakini hivi karibuni ndiyo kesi ilipatiwa ufumbuzi mahakamani huku yeye akiwa ameshindwa.

Kwa jinsi Dk. Ian na Mzee Williamson walivyokuwa wameshibana, haikuwa rahisi kufikiri kwamba kulikuwa na chembe za usaliti. Ni jambo lililoanza kama mzaha hivi na hata Dk. Williamson hakulipa uzito. Lakini baadae alipokuja kushtuka, haki za shamba lake zilikuwa zimepindwa na mmiliki halali wa nusu ya shamba akawa ni Dk. Ian ambaye ni rafiki yake.

Tukio hili lilimshangaza na kumchanganya sana, hasa alipogundua kwamba alikuwa amechelewa sana kwani Dk. Ian alikuwa amejiandaa vya kutosha kwa suala lile kiasi kwamba hata alipojaribu kwenda mahakamani kudai haki hiyo, alikuta amekwama na Dk. Ian ndiye aliyeonekana kuwa mwenye haki!

Kutokea hapo Dk. Ian na Mzee Williamson hawakuwahi kuonana! Sio kwa kuwa huyu yuko mbali na yule yuko mbali, ila ni kutokana na kiwango cha chuki ambacho kilizaliwa baina yao na kuota mizizi kwa haraka kama moto kwenye majani makavu.

Kupoteza haki zake kilikuwa ni kitendo kilichomuuma mno, na alijilaumu sana kwenye nafsi yake kwa kumuamini sana Dk. Ian kiasi cha kumpa siri zake ambazo alizitumia katika kumnyang’anya eneo la shamba lake. Na katika chuki hizohizo iliwahi kutokea siku ambapo Dk. Ian alimpigia simu Dk. Williamson na kumwonya kwamba kama ataendelea na jambo lolote la kumfanya adai eneo la shamba, basi atalia na Mungu wake. Japokuwa haya yalikuwa ni maneno ambayo angeweza kuyapeleka mahakamani, lakini alisita. Kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu aliamini kwamba kitendo hicho kitalipwa na Mungu siku moja.

* * * * * * * * * * * * *

Pengine ulikuwa ni wasaa wa mwisho kwa maisha ya Caroline. Kwa jinsi alivyochanganyikiwa kutokana na kupinduka na gari na jinsi treni la umeme lilivyokuwa likikaribia kwa kasi ya upepo, Caroline hakujua afanye nini ili kujinasua.

Alijilaumu sana kwa kukikaribisha kifo bila kulipiza kisasi. Ni kwa kudra za Mungu tu alijishtukia akijipinda na kuruka kando kama mwanasarakasi na treni ya umeme ikapita kwa kasi ileile na kumpita kwa nusu sentimita tu kichwani pake!

Baada ya treni kupita, Caroline akabaki ameduwaa akiangalia kama ambaye haamini kwamba tayari yuko salama. Aliangalia huku na huko kwa matumaini mapya kwamba ametoka kwenye aneo moja na amefika kwenye eneo jingine ambalo linaweza kuwa na usalama kwake.

Lakini Caroline hakuwa mjinga, alifahamu fika kwamba vyombo vya usalama vya Canada viko ‘fasti’ sana katika kushughulikia matukio ya ajali, kwa maana hiyo alijua kwa vyovyote vile, akizubaa kwa dakika chache mahali hapo, kuna uwezekano mkubwa wa kukutwa na magari ya polisi ambayo yatafika kwenye eneo hilo na hivyo kumtia mbaroni. Hakupenda kukamatwa kirahisi namna hiyo. Kukamatwa kwake kulimaanisha mashaka makubwa kwenye maisha yake. Na aliogopa sana kumaliza maisha yake kwenye sindano ya sumu atakayochomwa baada ya hukumu ya kifo kufuatia mauaji ya watu ambayo ameyafanya.

Alitaka kuinuka ili kukimbia, lakini akapata maumivu makali sana kwenye mguu wake wa kushoto. Alipouangalia, aligundua kwamba ulikuwa ukivuja damu nyingi na alipojaribu kuusogeza, upande wa goti ulionyesha kwamba umevunjika. Maumivu hayo yalimfanya alpige kelele za maumivu makali.

Lakini bado alikumbuka kwamba anahitajika kuondoka eneo hilo haraka iwezekanavyo kwa vile hapo sio mahala salama kwa yeye kubaki kutokana na tabia za polisi wa Ottawa.

Alijikongoja na kuanza kujiburuta akielekea msituni. Pamoja na kuwa alilazimika kujivuta, lakini alipata maumivu makali sana yaliyomfanya aanze kuutilia mashaka mguu wake kwamba inawezekana ukawa umekufa kabisa kiasi cha kukatwa. Hakujua huko anakokimbilia ni wapi na hakujua ni nani ambaye anaweza kumsaidia kuhusu mguu wake. Mara nyingine alilazimika kutambaa kwa umbali mrefu na mara nyingine aliinuka na kutembea kwa taabu sana akisaidia huku akishika miti.

Maeneo yote aliyokuwa akikatiza kwenye msitu huo, hapakuwa na dalili zozote za kuwapo mtu au nyumba. Jambo hili alilifurahia baada ya kukumbuka kwamba nchi nzima ya Canada itakuwa imeshapata habari za kusakwa kwake na yeyote atakayeonana naye ni rahisi kumtambua na kumripoti. Kutokana na hali aliyonayo, asingewqeza kujitoa mikononi mwa polisi au hata ya hao ambao watamkamata. Zaidi ya mguu, maumivu yalikuwa karibu kila mahali mwilini mwake.

Ilifika mahali ambapo mguu ulishindwa kabisa kuendelea kujisukuma kiasi akajikuta akijiegesha kando ya mti huku akilia. Kama kusingekuwa na maumivu makali kama yale, basi angepotiwa na usingizi kutokana na uchovu lakini haikuwezekana. Maumivu yalifunika kila kitu.

Mara akashtukia amesimamiwa na mtu, akageuka kwa ghafla huku akionyesha dhahiri kiwango kikubwa cha mshtuko.

“Who are you?” (We nani) yule mtu alimuuliza. Alikuwa ni mtu mzima mwenye sura ya ukarimu na ucheshi. Kabla hajajibu Caroline alimtazama kama anayemsoma huku moyo ukimdunda kwamba huyu ni nani na anajua nini kuhusu kusakwa kwake.

“Me?… Why do you want to know my name?” (Mimi.. Kwa nini unataka kujua jina langu?)” Alijibu.

“I’m the owner of this farm and I must know who are you and what are you doing here!” (Mimi ndio mwenye shamba hili, na lazima nijue wewe ni nani na unafanya nini hapa?)

Caroline alishindwa kujibu haraka haraka. Alishindwa kujibu kutokana na sababu nyingi ambazo alikuwa nazo. Siku zote hakuwa tayari kumtajia jina mtu ambaye hamjui. Ingawaje alikuwa na maumivu makali sana katika mguu wake uliovunjika, lakini aliweza kuongea.

“Listen my daughter, am Mr. Williamson, who is the owner of the farm. So explain yourself carefully and am will help you if you wish” (Sikiliza binti, mimi naitwa Mzee Williamson, ni mwenye shamba hili, jieleze vizuri kama una shida ninaweza kukusaidia), yule mzee alisema kwa sauti ya huruma.

Caroline akajikuta akivutiwa na sura ya uaminifu ya mzee Wiliamson na maneno yake yenye dalili za hekima.

“Excuse me, can you cure me before I axplain to you each and everything accured?” (Samahani unaweza kunisaidia dawa kabla sijakueleza yote yanayonisibu?) Caroline alilazimika kuomba hasa kutokana na maumivu makali aliyokuwa anaendelea kuyasikia. Mzee Williamson alimwinua na kumwongoza kutembea naye kuelekea kwenye nyumba yake. Alipofika huko alimweka kwenye nyumba yake ya shamba ambayo haikuwa na mtu mwingine yoyote. Alitengeneza maji ya moto na kuanza kumwosha ile sehemu ambayo ilikuwa ikivuja damu na baadae kumpaka dawa maalum kuzuia damu isiendelee kutoka.

Alipomaliza yote hayo alimletea chakula ambacho Caroline alikula kwa kasi kutokana na njaa aliyokuwa nayo. Alipomaliza kunywa maji, Mzee Williamson akawa yuko jirani yake.

“What happened?” (Nini kilikupata?) Mzee Williamson alionyesha hamu kubwa ya kutaka kujua kilichoendelea. Ni hapo ambapo Caroline aliamua kumweleza kila kitu bila kumficha, mambo yote makubwa katika maisha yake, kusakwa ili auawe na Dk. Ian pamoja na msako ambao unaendelea dhidi yake. Katika mazungumzo yote hayo, kikubwa kilichomshtua mzee Williamson ni pale alipotambua kwamba huyu aliwahi kuwa mke wa Dk. Ian ambaye yeye ni adui yake namba moja.

“You said were Dk. Ian’s wife?” (Unasema ulikuwa ni mke wa Dk. Ian?) Yule mzee aliuliza baada ya Caroline kumaliza maelezo yake huku akionekana wazi kushtushwa?

“Exactly, do you know him?” (Ndiyo, kwani unamfahamu?)

“I’m not sure. There’s someone with the same name who confused me tha I put him to be my number one enemy in my life. He snatched my farm from the case which…” (Sina hakika. Yupo mtu mwenye jina kama hilo ambaye amenichanganya sana kwenye akili yangu na mpaka sasa nimemfanya kuwa adui namba moja katika maisha yangu. Mtu huyo alinidhulumu shamba langu katika kesi iliyo…)

“He Snatched your farm? I’m talking about Dk. Ian who won the some alike case few days before we atarted these problems” (Alikudhulumu shamba? Dk. Ian ninayemzungumza mimi alishinda kesi kama hiyo siku chache kabla hatujaingia kwenye matatizo haya.”

“Yes, it’s him. He is my biggest enemy that I can’t forgive him till the day I die!” (ndio, ni yeye huyo, yule ni adui yangu mkubwa na siwezi kumsamehe mpaka siku ya kufa.)

“Why” (Kwa nini).

“He made a very bad matter for me, he snatched my farm. Fist he was my best friend that I couldn’t think that he would do such a thing to me. But he did. He left me in tears for my rights he destroyed in the court” (Amenifanyia ushenzi mkubwa, alinipora shamba langu. Huyu mtu alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana na hata siku moja sikutegemea kama ana mawazo ya kutaka kunidhulumu eneo la shamba langu, na ndivyo alivyofanya kwa kweli. Amefanya hivyo na ameniacha mimi nikiwa nalilia haki zangu ambazo amezipinda mahakamani).

Caroline akashangaa sana kusikia habari hizo. Pamoja na kujua uovu mkubwa wa Dk. Ian, lakini hakuwa amefikiria kwamba angeweza hata kujiingiza kwenye mambo ya kudhulumu wakulima.

Mzee Wiliamson alimhakikishia Caroline kwamba yeye binafsi atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba anaokoka na balaa lile na kurudi nyumbani kwao Tanzania kwa vile yeye na Dk. Ian ni maadui na kwa sababu anamsaka ili amuue, basi yeye yuko tayari kumsaidia ili asipatikane.

Kwa karibu mwezi mzima Caroline alikuwa hapo nyumbani kwa Mzee Williamson akitibiwa mguu wake na daktari wa mzee huyo ambaye karibu kila mara alikuwa akija kuhakikisha kwamba hali yake inakuwa nzuri. Baada ya kipindi hicho, Caroline alipata nafuu kubwa na aliweza hata kutembea mwenyewe bila msaada wa mtu yoyote au kuonekana na mtu kwamba aliwahi kuumia.

Ni hapo ambapo Mzee Williamson alimpa mipango yake ya jinsi atakavyofanya mpaka kumwezesha kutoroka kwenye nchi hiyo.

“I will bring to you a plastic surgery on specialist, he will make for you more than five faces that will help you in escaping. Without them you will be in trouble wherever you are seen. When we are ready will the faces you will leave for airport and fly to your homeland, it’s alright?” (Nitakuletea mtu ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza sura za bandia, kwa hiyo atakutengenezea sura za bandia zaidi ya tano na utazitumia hizo kutorokea. Kwa jinsi ulivyo, sura yako ikionekana mahali popote itakuwa ni balaa kwa sababu ni lazima watakukamata. Tukishatengeneza sura hizo, utaondoka moja kwa moja kwenda uwanja wa ndege na utaingia kwenye ndege na kuondoka kwenda nyumbani kwenu, sawa?)

“It’s alright and thank you very much Mr. Williamson” (Sawa na ninashukuru sana mzee Williamson).

Siku iliyofuata mzee mmoja wa Kijapan aitwae Sumo alifika hapo nyumbani na vifaa vyake na kufanya kazi hiyo. Ndani ya siku chache zikawa zimeshatengenezwa sura sita za bandia.

Tiketi ya ndege ikakatwa haraka haraka na siku moja baadae, Caroline akiwa na sura mojawapo ya bandia alifanikiwa kuingia kwenye ndege bila kutambulika huku kwenye moja ya mizigo yake kukiwa na sura nyingine tano za bandia kwa akiba!

Wakati anatafuta kiti chake akae, alishangaa sana kuona seti moja ya viti vitatu imekaliwa na kijana ambaye alimfahamu pamoja na mwanamke wa kizungu. Si tu kumfahamu, alishtuka sana alipogundua kwamba yule kijana alikuwa ni Dickson! Dickson ambaye zamani aliwahi kumbaka msituni baada ya kumnywesha madawa ya kulevya. Alijikuta akisimama na kumtazama kijana huyu huku akionyesha wazi kuduwaa. Akaamua kuketi kwenye viti hivyo.

Dikson aliwahi kumchangamkia kwa kumsalimia pamoja na yule mwanamke wa kizungu. Dickson alipotambua kwamba anazungumza na Mtanzania mwenzake alifurahi sana. Dickson baada ya tukio lile alikuwa ametoroka nje ya nchi na hapo ndipo alikuwa akirudi nyumbani pamoja na mke wa kizungu.

Alipoyakumbuka matukio aliyofanyiwa na Dickson, Caroline hasira zikampanda. Moyoni mwake akaapa kwamba mwanaume huyu masaa machache yajayo atakuwa ameingia kwenye orodha ya walio katika mpango wa kuuawa ambapo wengine ni Harry, Richard, Reginald, na Leonard Katunzi. Kwa kiwango ambacho alikuwa amefanyiwa ukatili na Dickson, hakuona haja yoyote ya kumsamehe.

Wakiwa wamekaa pamoja, walikuwa wakizungumza mambo mengi mbalimbali kuhusu biashara huku Caroline akijitambulisha kwa jina bandia la Vicky akiwa ni mfanyabiashara. Maskini Dickson, alizugwa na sura ya bandia aliyokuwa ameivaa Caroline. Laiti kama angelijua kwamba anayezungumza naye pale ndiye Caroline, nadhani angeruka kwenye ndege!!

Dickson alivutiwa vilivyo na uzuri wa ‘Vicky’ (Caroline) akamwambia kwa kiswahili ili mke wake asisikie kwamba watakapofika nyumbani, ni lazima wawasiliane ili waongee zaidi, kitu ambacho Caroline alikikubali.

“Huu ndio wakati wangu, mwingine nimeshampata, ni lazima nimuue haraka iwezekanavyo”, aliwaza. Lakini wazo lingine lilimjia haraka, kwamba hawezi kumuua mtu huyo kwenye ndege. Akafikiria mbinu nyingine.

* * * * * * * *

Dunia nzima zilisambazwa habari kwamba msichana muuaji aitwae Marion au Caroline anatafutwa kutokana na mauaji makubwa ambayo ameyafanya kwa nyakati tofauti. Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa kupitia televisheni, magazeti, redio na mitandao ya Internet. Mpaka humo ndani ya ndege abiria wote walikuwa na habari ya kusakwa kwa mwanamke huyo mdunguaji.

Wakati dunia ikiwa kwenye msako mkubwa hivyo pamoja na polisi wa Kimataifa wa Interpol Dk. Ian naye alikuwa akiumiza kichwa chake kwamba ni vipi atamtia mikononi mwake Caroline.

Je Caroline atafanikiwa kumuuua Dickson na ataweza kufika Tanzania salama? Usikose toleo lijalo.

Wote wawili waliishi ndani ya chumba kidogo chenye hewa finyu, hapakuwa na kitanda wala mahali pa kukaa na kila siku sakafu ilimwagiwa chumvi iliyokula miguu na makalio yao, walikula mara moja tu kwa siku, wazazi wa Caroline Dr Cynthia na profesa Kadiri walikuwa katika mateso makali mno! Hakuna mtu aliyeelewa juu ya kuwepo kwao ndani ya himaya ya Dr Ian hata balozi wa Tanzania nchini humo hakulielewa jambo hilo.

Mara kwa mara walimwomba Dr Ian awaachie huru kwa sababu hawakuwa na hatia, lakini mzee huyo katili hakuwajali, alizidi kuongeza mateso kadri siku zilivyokwenda! Aliamini hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kumfanya Caroline arudi, kitendo chake cha kutoroka uwanja wa ndege na kuwaacha O’brien na wenzake wakiwa maiti kilimwongezea hasira zaidi, usiku na mchana kundi lake la mafia lilikuwa katika msako mkali wa kimya kimya wakimtafuta Caroline lakini hawakufanikiwa.

Kila mtu aliamini Caroline au Marione kama pasipoti yake ilivyojieleza alikuwa bado yu ndani ya nchi ya Canada, makachero waliigeuza nchi hiyo ‘njendani’ lakini hawakufanikiwa kumpata. Kila mtu alizidi kuchanganyikiwa!Viwanja vyote vya ndege nchini humo vililindwa, watu walipekuliwa ipasavyo mipakani na katika bandari zote!

Njia zote za kutoka nje ya Canada ziliwekwa chini ya ulinzi mkali, Caroline akisakwa kwa udi na uvumba! Hakuna aliyejua kuwa tayari Caroline alishaondoka nchini humo kwa msaada wa Dr Wiliamson adui mkubwa wa Dr Ian na alikuwa njiani kuelekea Tanzania akitumia pasipoti yenye jina la Vicky na sura ya bandia iliyomfanya aonekane msichana mrembo..

Ni kutopatikana kwa Caroline ndiko kulikomfanya Dr Ian aongeze mateso zaidi kwa wazazi wake alizidi kuhakikisha kuwa hakuna mtu aliyefahamu kuwa watu hao walikuwa ndani ya ngome yake, isipokuwa wafanyakazi wake! Siku zote Profesa Kadiri na mkewe walikaa ndani ya mahabusu na hawakuonekana na watu kabisa!

Walikonda vibaya na miili yao ilijaa vidonda sababu ya chumvi nyingi iliyomwagwa ndani ya chumba kidogo cha mahabusu walichofungiwa! Hawakuwa na uhakika kama wangetoka salama katika himaya hiyo! Maisha yao yalikuwa mikononi mwa Dr Ian, alikuwa na uwezo hata wa kuwaua mbali kama angetaka kufanya hivyo kila siku walimwomba Mungu awanusuru na janga walilokuwa ndani yake.

*************

“Can we meet in Dar?”(Tunaweza kukutana Dar es Salaam?) aliongea Caroline na maneno hayo yalimfanya mke wa Dickson ashituke na kugeuka kuwaangalia, kwa muda mrefu walikuwa wameongea kwa kiswahili bila yeye kuelewa kilichokuwa kikiongelewa.

“Tafadhali Vicky usiongee kwa Kiingereza mke wangu ana wivu sana, utaleta matatizo tumia tu kiswahili, unajua huyu mwanamke nilimwoa sababu nilitaka kupata kibali cha kuishi Uingereza, vinginevyo nisingemwoa kabisa! Si unamwona alivyo mzee? Ninahitaji kijana kama wewe awe mke wangu au siyo?”

“Sawa tu basi tukutane Dar es Salaam!”

“Hamna shida!” Alijibu Dickson huku akimwangalia Caroline kwa macho ya mshangao sana!

“Vipi mbona unanishangaa kiasi hicho?”Caroline alijikuta akiuliza, macho ya Dickson yaliashiria wasiwasi fulani, akaanza kuhisi labda alishagundulika.

“Hapana, ni sauti yako ndio iliyonishangaza!”

“Ikoje Dickson?”

“Ni ya mtu ninayemfahamu kabisa, ingawa sina uhakika nilimwona wapi, kwani mimi na wewe tumewahi kukutana mahali labda?”

“Hapana sura yako ni ngeni kabisa machoni mwangu, kwani kabla ya kwenda Uingereza uliishi wapi?”
“Tanzania?”

‘Mji gani?”

“Dar es Salaam!”

“Mimi sijawahi kabisa kuishi Dar es Salaam!” Caroline alidanganya.

Mke wa Dickson tayari alishalala usingizi tena na tayari ndege ilikuwa ikielekea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, ilishatimu saa tisa na nusu ya alasiri! Hata Dickson pia alikuwa akiyumbisha kichwa chake kwa usingizi, Caroline alikuwa macho akiwa na karatasi ndogo mkononi alikuwa akiisoma kilichoandikwa juu yake.

“Dickson..... Reginald....... Harry........... Leonard ! Hawa wote ni lazima wafe tena kwa mkono wangu, nasikitika nimeua watu wengi sana maishani mwangu lakini sikuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kufanya hivyo!” Aliwaza Caroline!

Ndege ilitua uwanja wa ndege wa Dar es Salaam saa kumi kasoro dakika kumi na tano na watu walianza kushuka mmoja baada ya mwingine taratibu, Caroline alikuwa nyuma ya Dickson na mke wake alikuwa mbele!

Walipofika chini walianza kutembea taratibu kuelekea kwenye lango la kutokea, kichwani mwake Caroline alifikiria yaliyotokea uwanja wa ndege wa Ottawa, alihofia kukamatwa tena lakini kwa sura aliyokuwa nayo na jina alilotumia aliamini hakuna mtu angemgundua hata kama kungekuwa maaskari! Nje ya uwanja waliagana, mke wa Dickson akionyesha chuki ya waziwazi kwa Caroline!

“Tutafikia hoteli Landmark! Njoo pale hotelini saa moja na nusu jioni tuongee vizuri sawa?”

“Sawa lakini kuna kitu kimoja nataka uelewe!”

“Kitu gani hicho?”

“Nakupenda sana Dickson, sijui kwanini nimetokea kukupenda ghafla kiasi hiki!”

“Hata mimi pia!”

Aliuacha uwanja wa ndege akiamini kazi iliyokuwa mbele yake ilikuwa imeanza kutekelezwa! Aliiita kazi hiyo Operesheni Lipa Kisasi au OLK! Watu wote waliomfanyia mabaya ilikuwa ni lazima wafe na wa mwisho kufa ilikuwa ni lazima awe Harry! Ingawa hakufahamu ni wapi alikokuwa kwa wakati huo lakini ilikuwa ni lazima afe! Kwa ubaya aliomfanyia hakukistahili msamaha! Ni yeye aliyemsababishia yote yaliyotokea, ni yeye Harry aliyestahili kulaumiwa kwa vifo vya watu wote waliouawa kwa mkono wa Caroline.

“Sikumaanishwa kuwa muuaji, ni Harry aliyesababisha yote haya ni lazima afe, damu yake ni halali yangu!” Aliwaza Caroline.

Alikuwa ndani ya gari aina ya Mark II lililofanya kazi ya kubeba abiria kutoka uwanja wa ndege wa Dar es Salaam hadi mjini! Teksi hiyo ilimkumbusha ajali mbaya iliyotokea uwanja wa ndege wa Ottawa akijaribu kutoroka baada ya dereva kuruka.

“Ni lazima alikufa! Kwa jinsi alivyoruka haiwezekani hata kidogo akawa salama!”

“Nani dada?” dereva aliuliza, Caroline alikuwa ameongea kwa sauti kubwa bila kufahamu!

“Hapana nimepitiwa tu!”

“Haiwezekani lazima kuna jambo linakutatiza!”

“Babu achana nayo hayo hayakuhusu!”

“Siyo hivyo siku hizi kuna matatizo mengi duniani, si unaalewa mambo ya magaidi na mauaji yanayotokea, isijekuwa na wewe umepatwa na matatizo ya aina hiyohiyo”

“Mh!” Caroline aliguna hiyo ilimwonyesha wazi kuwa hata katika Tanzania taarifa zake zilishafika na alitakiwa kuwa mwangalifu sana!

“Tunaelekea wapi?”

“Hoteli New Africa! Ni shilingi ngapi?”

“Elfu tano tu mwanangu!” Alijibu dereva aliyekuwa na umri sawa kabisa na babu yake na Caroline.

“Ok!”


Gari ilizidi kutiwa moto mbele kidogo waliingia katikati ya jiji la Dar es Salaam maeneo ya Posta, Caroline aliona kitu kwenye moja ya kuta za nyumba! Moyo wake ulishtuka, ilikuwa ni picha yake kubwa ikiwa imebandikwa ukutani na juu yake yaliandikwa maneno “Most wanted” Reward 25m U$D! Aliikumbuka picha hiyo, ilikuwa ni picha aliyopigwa na Dr Ian kwa ajili ya hati yake ya kusafiria, alielewa lazima picha hiyo ilitolewa na mume wake wa zamani ili aweze kukamatwa kirahisi.

“Simama!” alimwamuru dereva na dereva alisimama haraka bila kusita, Caroline aliruka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye picha hiyo! Aliiangalia kwa muda na kuyasoma maelezo yake, jina lake lilitajwa kabisa akiitwa muuaji namba moja aliyekuwa akitafutwa dunia nzima! “Serial killer!” Hivyo ndivyo alivyotajwa katika tangazo hilo.

Mwili wote wa Caroline ulilowa jasho na akaanza kutetemeka, kama hivyo ndivyo ilivyotangazwa dunia nzima basi hakuwa na mahali pa kukimbilia! Alibaki amesimama mbele ya tangazo hilo akihisi mwili wake ulikuwa umekufa ganzi!

“Binti twende! Tunazidi kuchelewa, nitakuchaji gharama za kusubiri!”Alisema dereva akionyesha hali ya kuwa na wasiwasi, Caroline alitembea taratibu kurudi kwenye gari na kuingia ndani yake.

“Mbona umeonyesha kushtuka sana, unafahamu huyo dada hatari nini?”

“Hapana!”

“Wanasema aliwahi kuishi hapa miaka ya nyuma akisoma sekondari ya Jangwani,lakini mimi simfahamu!” alisema mzee huyo, Caroline alipoyasoma macho ya mzee huyo alijifunza kitu fulani! Alihisi hali ya hatari! Mzee huyo alikuwa akimkazia sana macho shingoni mwake.

“Binti mbona umevaa sura ya bandia?”Mzee huyo alimuuliza akionyesha mshangao

“Hapana siyo sura ya bandia babu!”

“Ah! Acha bwana huwezi kunidanganya mimi, nimepigana vita vya pili vya dunia sisi ndio wakongwe!”

“”Masikini mzee huyu nae afe???”Alijiuliza Caroline kichwani mwake, hilo ndilo jambo pekee lililokuwa likimfuata mzee huyo, alikuwa hatari kubwa kama tu angetoa taarifa yoyote juu yake! Hakupenda kumuua lakini alilazimika kufanya hivyo ili kujiokoa! Alikuwa ameponzwa na mdomo wake.

Hapohapo alianza kujipapasa kwenye pindo la nguo yake na kuigusa sumu yake mahali ilipofichwa, lakini hakutaka kuichukua mara moja! Walipofika hotelini, Caroline alishuka haraka na kuingia hotelini akiwa na mizigo yake!


Yüklə 0,95 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   18




Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2024
rəhbərliyinə müraciət

gir | qeydiyyatdan keç
    Ana səhifə


yükləyin