**************
Yalikuwa maisha mapya kwa Caroline,maisha yaliyoonekana kuwa ya furaha siku zote, alikipata kila alichokitaka yakiwemo matibabu ya ugonjwa wake! Katika muda wa miezi mitatu tu aliyokaa nchini Canada ugonjwa wake ulipona kabisa, hakuanguka tena. Kila mtu katika familia yake alimheshimu Caroline, aliitwa Queen!
Asubuhi aliamshwa kitandani, aliogeshwa alipigishwa mswaki, alivalishwa nguo, kitu pekee alichofanya ni kula chakula! vingine vyote vilifanywa na wafanyakazi wa nyumbani kwake, kila alikokwenda alipewa ulinzi. Maisha ya Caroline yalikuwa ya Kifalme, machozi na huzuni zote alizowahi kuwa nazo zilifutika aliishi maisha ya raha mustarehe.
Pamoja na raha zote hizo bado Harry aliendelea kuwa kichwani mwake, alimuwaza na kumfikiria kila siku! Alimuota akiwa usingizini na kuna wakati badala ya kumwita Ian kwa jina lake alimwita Harry! Bado alitamani kuonana naye na aliamini hilo lazima lingetokea maishani mwake. Kadri siku zilivyozidi kupita mawazo juu ya Harry yaliongezeka na kumkosesha raha.
Alipowasiliana na ndugu zake Arusha akitaka kujua mahali alikokuwa Harry aliambiwa aliondoka miaka mingi kwenda Ulaya kwa baba yake na haikujulikana mama yake alikuwa wapi kwa wakati huo, hakuna mtu aliyejua Harry alikuwa ulaya katika nchi gani! Ilibidi Caroline kwa utajiri wa mume wake aamue kumtafuta Harry huko huko Ulaya. Alikwenda katika ofisi za shirika moja binafsi la upelelezi na kuwaeleza shida yake.
“Nataka mmtafute popote pale duniani kwa gharama yoyote na mimi nitalipa!”
“Hiyo ni kazi ndogo kwa kuanzia utatulipa dola za Kimarekani milioni tano!”
“Pesa siyo tatizo! Ninachohitaji ni kumwona Harry kabla sijafa!”
“Hilo litafanyika!”
Caroline aliandika hundi ya kiasi hicho cha pesa, picha na taarifa muhimu za Harry na kuwakabidhi, kazi ya kumsaka Harry dunia nzima ilianza, kwanza wapelelezi walitumwa Arusha Tanzania.
****************
“Woooow! I cant believe it! Is it mine?”(Woooow! Nashindwa kuamini! Kweli ni yangu?)
“Yeah it is yours! Dont you remember that to day is 23rd August?”(Ndiyo ni yako! Umesahau kuwa leo ni tarehe 23 mwezi wa nane?)
“What happens with 23rd August?”(Kwani nini hutokea tarehe 23 mwezi wa nane?)
“Your birthday darling!And this Aeroplane is your birthday present! I want to make you the happiest woman on earth”(Sikukuu yako ya kuzaliwa mpenzi na hii ndege ni zawadi yako, nataka kukufanya mwanamke mwenye furaha kuliko wote duniani!)
Caroline aliruka kwa furaha na kumkumbatia mume wake huku akilia machozi, Ian hakuwa amemtaarifu juu ya kumnunulia ndege kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.
“I want you to go to Miami beach for a month long vacation! Go there and relax! I just need to have another Pilot who will be flying you jet!”(Nataka uende Miami ukapumzike kwa mwezi mmoja, ninachohitaji sasa hivi ni rubani mpya atakayekuwa anarusha hii ndege yako!)
Wiki moja baadaye matangazo ya rubani mpya aliyekuwa akitakiwa na tajiri Ian Smith kwa ajili ya kuendesha ndege ya mke wake yalitangazwa katika redio, televisheni, magazeti na kwenye mtandao wa Internet! Marubani sehemu mbalimbali duniani walisoma matangazo hayo. Miongoni mwa marubani waliosoma tangazo hilo alikuwa Harry ambaye kwa wakati huo hakuwa na kazi baada ya shirika la ndege la USD Airlines kufilisika. Alifurahi kupita kiasi na siku ya usaili alikuwa miongoni mwa wasailiwa waliofika katika ofisi ya tajiri Ian.
Je nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.
Nawapenda Mayatima wote na ninawaeleza wazi kuwa hawana sababu ya kujisikia wanyonge kwa sababu ya hali zao! MUNGU ANAYAJUA MAISHA YETU.
M
arubani wapatao 210
walifurika mbele ya ofisi
za Dk. Ian Smith asubuhi ya siku hiyo kwa ajili ya kufanyiwa usaili, kati ya marubani hao wote alitakiwa rubani mmoja tu kwa ajili ya kuirusha ndege ya Caroline mke wa tajiri Dk. Ian, ilikuwa ni kazi ngumu kupita kiasi kuipata nafasi hiyo.
Kila mtu alibeba makabrasha vyeti mbalimbali kuonyesha yeye ndiye alikuwa rubani bora kuliko wengine, Harry alisimama nyuma kabisa ya kundi hilo akiwa mwenye mawazo mengi, hakuwa na uhakika wowote wa kushinda katika kinyang’anyiro hicho, aliona hakuwa na sifa za kutosha kuipata nafasi hiyo.
“I worked with Kenya Airways for 5 years, later i joined British Airways where I also did another 10 years as a Pilot! Those days the wages wasn’t good so had to quit! What about you?”(Nilifanya kazi na Shirika la Ndege la Kenya kwa miaka 5, baadaye nilijiunga na Shirika la ndege la Uingereza ambako nilifanya kazi kwa miaka 10, wakati huo malipo hayakuwa mazuri ilibidi niache kazi! Vipi wewe?)
“I worked with Brazillian Airways for 4 years....... it wasn’t pay and left it for American Airlines where I’m an Imployee up this moment, I love Canada my country, need to come back and work here!”(Nilifanya kazi na shirika la ndege la Brazil kwa miaka 4, .......ilikuwa hailipi ikabidi niondoke na kujiunga na shirika la ndege la Marekani ambako nafanya kazi hadi leo hii, naipenda Canada nataka kurudi nyumbani nifanye kazi hapa!)
Harry aliysikia maongezi yote ya wazee wawili waliokuwa mbele yake wakiwa wamebeba brifkesi zao mikononi, walionekana wana elimu ya kutosha kuhusu mambo ya urubani! Hata kama ni yeye angekuwa anatafuta marubani ni lazima angewapa wazee hao, kamwe asingempa kazi mtu mwenye elimu na uzoefu kidogo kama aliokuwa nao yeye! Harry alikata tamaa, wazo la kutaka kuondoka lilimwijia kichwani lakini alipingana nalo na kuamua kujaribu.
“I’m gonna try it! It doesn’t matter I loose or gain, at least I gave it a trial!”(Nitajaribu haijalishi nitapata au sipati ili mradi nimejaribu!) aliwaza Harry, alitaka sana kupata kazi hiyo ili ajikwamue tena kimaisha, alikuwa amechoka kukaa bila kazi nchini Marekani! Aina ya ndege aliyotakiwa kuaendesha pia ilimvutia, katika maisha yake alitamani sana kuendesha ndege ya aina hiyo, ilikuwa ni aina mpya kabisa ya ndege.
“Sijui huyo mkewe yupo vipi mpaka kanunuliwa ndege ya kisasa namna hii? Lazima atakuwa bonge ya kifaa kinachomchanganya akili tajiri Ian!” Aliwaza Harry!
“Hivi huyo mke wa Ian ni mtu wa hapa Canada?” Harry aliwasikia wazee waliokuwa mbele yake wakiendelea na maongezi yao, alisogea kimya kimya hadi karibu yao ili asikie jibu la swali hilo, alitamani sana kumfahamu mwanamke huyo!
“Hapana nasikia ni Mwafrika!”
“Alitokea nchi gani?”
“ Sina uhakika alitokea nchi gani, ila niliwasikia watu wakisema ni mtu wa Afrika Magharibi lakini kuna wengine wanadai ametoka Tanzania huko Afrika ya Mashariki, kwa kweli sina jibu zuri la nchi anayotoka!”
“Ni mwanamke mwenye bahati sana, anaitwa nani?” Harry aliyaingilia kati mazungumzo yao na wazee hao waligeuka nyuma kuangalia ni nani alikuwa akiwasemesha, walionekana kutofahamu kama kulikuwa na mtu kasimama nyuma yao akiwasikiliza.
“Kwa kweli jina lake silifahamu!”
“Huwa anaonekana lakini?”
“Siyo rahisi kumwona mimi nimezaliwa hapahapa Ottawa na ninaishi katika jiji hilihili lakini hata siku moja sijawahi kumtia machoni, analindwa kupita kiasi!”
“Aisee!” Harry aliitika kwa mshangao.
Baadaye usaili ulianza marubani walianza kuingia mmoja baada ya mwingine katika chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo, marubani waandamizi wa mashirika matatu makubwa ya ndege duniani, British Airways, Lufhthansa, United Airlines walikuwa ndani ya chumba hicho kuongea na rubani mmoja baada ya mwingine wakitafuta rubani mmoja tu kati ya marubani wote waliojitokeza, ilikuwa ni kazi ngumu na maswali yalikuwa magumu, Harry alisimama nyuma kabisa akitetemeka na moyo wake ulidunda kwa nguvu, hakujiamini hata kidogo alihofia kila mtu aliyekuwepo mahali pale.
“Harry Robertson!”msichana mmoja aliyesimama mlangoni aliita na Harry alitembea kwa haraka kuelekea mlangoni ambako aliingia hadi ndani! Macho yake yalipambana na nyuso za wazee wawili waliovaa mavazi ya Kirubani.
“Naitwa rubani Rose B. Kipya! Ninatokea British Airways na huyu hapa ni rubani Reuben Kip kutoka Lufhthansa na aliyekaa kwenye kona ni rubani Martin Jackson kutoka United Airlines, kabla hatujakufanyia usaili, sijui mwenzetu unaitwa nani?”
“Ninaitwa rubani Harry Robertson!”
“Ndiyo Harry, elimu yako katika masuala ya urubani ni ipi?”
Harry alianza kuielezea elimu juu ya masuala ya urubani kisha akakabidhi vyeti vyake vyote, rubani Rose akavipokea na kuanza kuvikagua, alisoma huku akitingisha kichwa, kisha akanyanyua uso wake kumwangalia, alionekana kutokuwa na neno la kuongezea! Akavichukua vyeti vyake na kuwakabidhi marubani wenzake, nao wakaanza kuvitupia macho! Wote walipomaliza kuviangalia walinyanyua nyuso zao na kuonekana kukubali kitu fulani ndani ya nafsi zao! Tabasamu zilionekana katika nyuso zao ziliashiria ushindi kwa Harry!
“Jamani kuna mtu ana suala la nyongeza?” Rubani Rose aliyeonekana kuwa kiongozi wa usaili huo aliuliza.
“Mimi ninalo!” Alijibu rubani Martin.
“Haya uliza?”
“Kitu gani cha kwanza unachoweza kufanya kama ndege imeleta hitilafu angani na kuanza kushuka kwa kasi kuelekea baharini au ziwani?”
“Ni kuachia hewa ya oksijeni itoke ya kutosha na kuhakikisha abiria wote wamefunika pua zao mipira ya hewa hiyo midomoni na puani, kuhakikisha ndege haichomi ncha ya kichwa chake kwenye maji bali kutua taratibu juu ya maji!”Alimaliza Harry.
“Sina swali zaidi , unaweza kuondoka!” Alisema rubani Martin huku akicheka.
Hadi jioni ya saa kumi na mbili siku hiyo bado usaili ulikuwa ukiendelea, mtu wa mwisho kufanyiwa aliingia ofisini saa 1:30 usiku! Marubani walikuwa bado wapo nje ya ofisi wakisubiri matokeo yao, wasaili walikuwa wamechoka sana kiasi cha kushindwa kutoa majibu siku hiyo, waliomba wasailiwa wote wafike ofisini hapo saa nne siku iliyofuata kupata majibu yao, masaa yaliyokuwa mbele yao yalikuwa ni kama miaka kumi zaidi ya kusubiri, hawakuwa wavumilivu kiasi hicho kila mtu alitamani kufahamu ukweli siku hiyo hiyo.
“Hatuwezi kutoa majibu leo!”Alisema rubani Rose B.Kipya kwa hasira, alionekana amechoka kuliko wengine wote, isitoshe alionekana ni mama asiye na huruma hata kidogo alikuwa na moyo wa kishupavu kama mwanaume akiamua kitu ameamua.
******************
“Vipi usaili umemalizikaje?Umepata rubani?”
“Ndiyo nimepokea ripoti kama dakika ishirini zilizopita, inavyoonekana ilikuwa kazi ngumu sana!”
“Lakini mmempata rubani?”
“Hapana majibu yatatoka kesho!”
“Jamani tafadhali msiniletee rubani kijana sana, nataka rubani mzee au makamo kidogo!”
“Darling lakini hiyo inategemea sana na elimu ya mtu!”
“Iko wapi hiyo ripoti? Naomba niione kidogo, majina yao yanaweza kunionyesha nani atanifaa!”
“Hii hapa!” Dk. Ian alimkabidhi Caroline makaratasi yote ya majina na akaanza kupitia jina moja baada ya jingine, akiwa kimya kabisa! Mbele kidogo alishtuka na kusimama wima mikono ikiwa kichwani, Dk. Ian hakuwepo wakati huo alikuwa chooni akijisaidia! Caroline aliona jina kama la mtu aliyemfahamu, hakuwa na uhakika kama kweli mtu huyo alikuwa yeye, Harry Robertson!
Lilikuwa jina la mwanaume wake wa kwanza, aliyemkataa sababu ya kifafa! Aliweka chini karatasi la majina na kuanza kuchambua nakala za vyeti na maelezo yao mengine ili kuangalia kama jina hilo lilikuwa la mtu aliyemfahamu na aliweka wapelelezi binafsi wamtafute duniani kote, mwanaume aliyehisi alimpenda kuliko mwanaume mwingine yeyote duniani! Ilichukua kama dakika tatu zaidi kuviona vyeti vya Harry na tayari Dk. Ian alisharejea kutoka chooni.
“Vipi tena unatafuta kitu gani humo darling?”
“Kuna mtu jina lake limenivutia nataka kuangalia vyeti vyake!”
“Nani?”
“Harry Robertson!”
“Nilijua tu huyo utamfurahia sababu ni mwafrika mwenzako!”
“Ni mwafrika?”
“Ndiyo lakini ni kijana mdogo sana kitu ambacho wewe hupendi!”
“Nimevutiwa nae sana nipo tayari kumchukua, kifupi kesho wasaili wakija waeleze ninayemtaka ni huyo Harry peke yake, wengine waondoke zao!”
“Sawa darling!” Aliitikia Dk. Ian, pamoja na ukatili wake wote kwa Caroline hakuwa na neno, alimpenda kupita kiasi na alikuwa tayari kumfanyia lolote alilotaka. Siku iliyofuata matokeo yalipotoka jina la Harry Robertson ndilo lilitangazwa kuwa mshindi,.Harry aliruka juu na kushangilia, aliona hiyo kama bahati ya ajabu, hakujua ilikuwa ni mipango ya Caroline.
Hakuamini jibu hilo, ilikuwa ni furaha kubwa mno kwake kupata kazi tena! Aliamini ndoto yake ya kuendesha ndege kubwa ilikuwa imetimia! Alishindwa kuelewa ni kitu gani hasa kilichofanya ashinde, hakutaka kukubali kuwa yeye ndiye alikuwa rubani bora kuliko wengine wote.
Wakati akifurahia hivyo aliitwa ofisini ambako kwa mara ya kwanza alikutana na tajiri Dr. Ian Smith na kusalimiana nae, alisaini mkataba wa kazi kwa miaka mitatu na kuruhusiwa kuondoka kurejea nchini Marekani, akitakiwa kuwa kazini wiki moja baadae. Aliahidiwa nyumba nzuri, gari zuri la kutembelea siku zote ambazo angekuwa safarini! Kwa mambo hayo kila kitu alichohitaji katika maisha yake angekipata, kitu kimoja tu hakikutajwa katika mkataba wake nacho ni msichana mzuri! Hicho ndicho alichohitaji zaidi baada ya kuanza kazi.
Harry alikuwa kijana hodari wa ngono, alipenda vimwana kuliko kitu kingine chochote, alibadili wasichana kama nguo, kila msichana mzuri duniani alitaka awe wake, alipenda kutembea na wasichana wenye majina kuliko. Sura yake ya kuvutia ilimfanya awapate wasichana kirahisi, wasichana wengi walivutiwa na muonekano wake na pia kazi aliyoifanya! Kwa mshahara na marupurupu aliyoahidiwa kwa kuendesha ndege ya mke wa Dr. Ian alikuwa na uhakika wa kuwachanganya wasichana wote wa Canada kama kachumbari.
****************
Caroline alitamani sana kumwona mtu aliyekuwa na jina kama la mpenzi wake wa kwanza! Alipoambiwa kuwa Harry aliondoka kurejea Marekani alisikitika sana! Alipoulizia kama kulikuwa na picha alizoacha aliambia hakuna, alizidi kuumia. Wiki moja aliyopewa Harry kabla ya kuanza kazi aliiona kubwa mno! Na alishindwa kuelewa ingeifikia vipi! Alitamani sana kumwona Rubani mwenye jina la Harry alishindwa kuwa na uhakika kama Harry huyo ndiye Harry aliyemtafuta!
Siku za kusubiri Harry arudi kuanza kazi zilikuwa za mateso makubwa kwa Calorine, alibadilika na kuwa mtu mwenye mawazo na huzuni kila siku pamoja na zawadi ya ndege aliyonunuliwa, Dr. Ian aliigundua hali hiyo, siku zote hakupenda kumwona Caroline akisikitika, alitaka kumpa furaha maishani mwake, aliamini mateso na huzuni alizozipata maishani mwake zilitosha na hakutaka aendelee kuishi katika mateso hayo?
“Usihuzunike mke wangu, kwanza nataka Rubani akirejea tu uende kwenye nyumba yetu huko Miami Beach ukapumzike kwa mwezi mmoja! Unahitaji muda fulani kukaa peke yako na kustarehe, nitakufuata baada ya mwezi huo mmoja! Sawa?”
“Sawa lakini Rubani yupo wapi?
“Atakuja tu!”
“Mbona anazidi kuchelewa?”
“Lini tulimpa wiki moja!”
“Wiki moja ilikuwa kubwa mno! Mngempa siku tatu tu!”
“Vumilia tu mama!”
***************
Caroline alipakia kabisa mizigo yake ndani ya ndege tayari kwa safari. Siku ambayo Rubani angewasili kutoka Marekani, kila kitu alichokihitaji akiwa Ufukweni Miami kilikuwa ndani ya ndege aliyekuwa akisubiriwa alikuwa ni Rubani Harry Robertson peke yake, Caroline alikuwa na hamu sana ya safari hiyo, na si safari tu bali alitaka sana kukutana na mtu mwenye jina sawa na mwanaume aliyempenda kuliko wote, mpaka wakati huo aliamini bila kifafa wangekuwa bado wako pamoja!
“Ngriii! Ngriiii! Ngriii!” Ulikuwa mlio wa simu pembeni mwa kitanda alipojilaza Caroline akimuwaza Harry! Alinyanyuka kinyonge na kuinyanyua simu.
“Hallow nani?”
“Dr. Ian!”
“Ndiyo Darling!”
“Taarifa nzuri!”
“Taarifa gani?”
“Rubani kaja!”
“Hakyanani?” Aliuliza kwa mshangao Caroline na alinyanyuka kitandani na kuanza kurukaruka kwa furaha!
“Ndiyo na tayari nimeshamtaarifu juu ya safari yenu dakika chache zijazo atakuwa ndani ya ndege akikusubiri!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Usichelewe kumtaarifu!” Alijibu Caroline tayari sura yake ilisharejewa na furaha iliyopotea! Aliona dakika zikienda taratibu sana, alitaka sana kumuona Harry!
Nusu saa baadae mlango wa chumba ulifunguliwa akaingia Dr. Ian na kumwamsha Caroline kitandani akamwomba ajiandae kwa safari ya kwenda Miami kwani Rubani alikuwa akimsubiri ndani ya ndege, Caroline alinyanyuka kwa furaha na wote wawili walitembea hadi uwanjani ambako ngazi zilishushwa, Caroline na Dr. Ian wakakumbatiana na kupigana mabusu ya kwaheri.
“I will miss you!” (Nitakukumbuka sana) Dr. Ian alimwambia mkewe.
“Me too!” (Hata mimi pia!) Alisema Caroline.
Baadae waliachiana na akaanza kupanda ngazi kuingia katika ndege, ilikuwa ndege kubwa kuliko zote alizowahi kupanda, aliamini kweli mume wake alimpenda na alishangaa ni kwanini mawazo yake yalikuwa bado yapo kwa Harry!
Aliingia ndani ya ndege na kukaa, mtumishi ndani ya ndege alimfuata na kumfungia mkanda wake vizuri, dakika chache baadae ndege iliacha ardhi na kupaa angani! Hali ilipotulia Caroline alishindwa kuvumilia na kujikuta akiufungua mkanda wake na kuamua kwenda kwenye chumba cha Rubani, mpaka wakati huo wote walikuwa bado hawajaonana uso kwa uso! Alipoufungua mlango tu Harry aligeuka nyuma, macho yao yakagongana.
“Haaaaa! Harry ni wewe!”
“Jamani Caroline kumbe wewe ndiye mke wa Dr. Ian?”
“Ndiyo ni mimi lakini bado nakupenda Harry kwa muda mrefu sana nimekutafuta bila mafanikio!” Alisema Caroline na kuinama akimbusu Harry mdomoni.
Machozi yalikuwa yakimtoka kwa furaha aliyokuwa nayo ghafla ndege ikaanza kwenda mrama! Ikiyumba kutoka upande mmoja hadi mwingine.
Je, nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.
“No! No! No, Caroline no! Acha tafadhali! Utasababisha ajali mbaya na sote tutakufa, acha Caroline acha!” Aliendelea kupiga kelele Harry akimsukuma Caroline aliyekuwa amemwangukia miguuni na kumkumbatia akimpiga mabusu yasiyo na idadi usoni na shingoni, kwa furaha aliyokuwa amepata Caroline alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa, hakuelewa kitu alichokuwa akikifanya kilikuwa cha hatari kupita kiasi.
“Tafadhali niachie Caroline ndege itaanguka!”Harry alizidi kupiga kelele lakini Caroline hakujali aliendelea kumkumbatia kwa furaha bila kujua alikuwa akipoteza mwelekeo wa ndege na kuifanya izidi kuyumba zaidi.
Ghafla mbele yake Harry aliona maji mengi! Ilikuwa ni habari, ndege ilikuwa ikielekea majini alijua bila kufanya jambo kwa haraka ndege ingetumbukia majini na huo ndio ungekuwa mwisho wao! Akili yake ilifanya kazi kwa haraka, nguvu nyingi zikamwijia mwilini mwake akafanikiwa kumsukuma na kumwangusha Caroline pembeni, akaanza kuhangaika ili kuidhibiti ndege iliyokuwa kwa mita chache kuyafikia maji.
Kwa utaalam aliokuwa nao alifanikiwa kuikatisha kona na baadaye kuiwezesha kuelekea tena angani! Hata yeye hakuamini kilichotokea, alipoona hivyo Caroline aligundua alikuwa amesababisha hatari na hofu ikaanza kumwingia moyoni mwake, kila mtu kati yao alibana pumzi akiomba muujiza utokee, ndege ilipofika juu Harry alifanikiwa kuituliza na kuendelea na safari yao.
“Flight no 13 where are you?”(Ndege namba 13 upo?)
“ I’m back on the communication track, we were facing some technical problems, right now were ok!”(Nimerudi katika mawasiliano, nilipotea kidogo sababu ya matatizo ya kiufundi lakini hivi sasa tuko salama)
“Oh! My God we lost the touch with your plane!”(Oh! Mungu wangu tulipoteza kabisa mawasiliano na ndege yako!)
Yalikuwa ni maongezi kati ya Harry na watu waliokuwa ndani ya chumba cha mawasiliano cha ufuatiliaji wa safari za ndege za tajiri Ian Smith, kwa muda kidogo walipoteza mawasiliano kati yao na ndege iliyombeba Caroline kwenda Miami.
Harry alishusha pumzi huku akitabasamu, hakuamini kama alikuwa amefanikiwa kuidhibiti tena ndege hiyo walipambanisha macho yao na wote wakatabasamu, ndani ya mioyo yao kulijaa furaha isiyoelezeka.
“You wanted us to die after we have just met?”(Ulitaka tufe mara baada ya kukutana?)
“No! You know how much I love you, cant kill you”(Hapana! unajua nakupenda kiasi gani, Harry siwezi kukuua)
“Then why did you disturb the move?”
“Sorry Harry, just got outta my cells, it was a surprise! I didnt know you were the pilot”(Samahani harry, nilipagawa nilipokuona, kilikuwa ni kitu cha kushtua sana, sikutegemea wewe ndiye rubani niliyetafutiwa!)
“Lets not talk a lot here, do it once were in Miami! all I can t tell you is I love you Caroline and did regret for what I did, please for give me!”(Tusiongee mengi hapa tutaongea tukitua Miami, ila ninachoweza kukueleza ni kuwa nakupenda sana Caroline, nilijuta sana kwa niliyokufanyia tafadhali nisamehe!”
“Let the gone go! This is a new chapter of love and harmony!” (Yaache yaliyopota hiki ni kipindi cha mapenzi na amani!) Alijibu Caroline huku akicheka, ilikuwa si rahisi kuieleza furaha aliyokuwa nayo moyoni mwake, ilikuwa ni kama ndoto kukutana na Harry tena! Hakumuwazia kabisa Dk. Ian kichwani mwake.
************
Ndege yao ilitua katika kiwanja cha ndege cha nyumbani kwao huko Miami, saa 12:30 jioni, tajiri Ian alimiliki eneo la hekari 120 katika ufukwe huo aghali duniani! Ni watu matajiri tu waliokuwa na maeneo katika ufukwe huo, tena maeneo yenyewe yalikuwa madogo mno,mtu mwenye eneo kubwa alikuwa tajiri Ian Smith peke yake.
Nyumba yao ilikuwa umbali wa meta 2000 kutoka mahali ndege yao ilipotua. Walikuta idadi ya watu wapatao ishirini wakiwasuburi eneo hilo, waliposhuka ndani ya ndege msichana mwenye mwamvuli alimfuata Caroline na kumfunika kwa juu ili asiungue na jua na alimwomba amfuate kumpeleka kwenye gari lililokuwa maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kumpokea.
“Wait! Why are you so much hurried?”(Subiri kwanini una haraka kiasi hicho?) Caroline alimwambia msichana aliyekuwa amemfunika mwamvuli tena kwa sauti ya ukali.
“I’m sorry madame!”(Nisamehe mama!)
“Haaaaaarry!” Caroline aliita baada ya kumkemea msichana huyo.
“Yes mom!”Ndiyo mama) Harry aliitika kwa heshima zote, hakutaka mtu yeyote agundue kilichoendelea kati yake na Caroline jambo ambalo kwa hakika alijua lingeweza kuhatarisha usalama wa maisha pamoja na kazi yake.
“Please come with me!”(Tafadhali nifuate!) Caroline alimwamrisha na Harry alikwenda mbio hadi mahali alipokuwa.
“Hebu nifuate na tangu sasa unapoongea na mimi kitu chochote unisemeshe kiswahili ili hawa watu wasielewe sawa mpenzi?”
“Sawa kipusa changu!” Alijibu Harry na wote walicheka na kuongoza hadi kwenye gari ambako mlango wa gari ulifunguliwa na msichana aliyewekwa tayari kwa kazi hiyo, Caroline akaingia ndani akifuatwa nyuma na Harry! Dereva aliyekuwa ndani ya gari aliwaamkia kwa heshima zote na gari likaanza kuondoka.
“Douglas!”Caroline alimwita dereva aliyekuwa akiwaendesha.
“Yes mom!”(ndiyo mama!)
“Meet Harry the new pilot in our company, he is gonna be flying my new jet!…..Harry this is Douglas Sagawalla a senior drive in our company!”( Douglas kutana na Harry, rubani mpya katika kampuni yetu, yeye atakuwa anairusha ndege yangu .....Harry huyu ni dereva wetu wa siku nyingi anaitwa Douglas Sagawalla!)
Harry na Douglas walishikana mikono na kukaribishana huku gari ikiendeshwa taratibu kutoka uwanja wa ndege kuelekea kwenye nyumba yao iliyokuwa nyuma ya kilima kilichopambwa na majani mengi ya kijani.
Walipoifikia nyumba gari liliegeshwa na wote wakashuka, Harry alikuwa amepigwa na mshangao mkubwa kwani katika maisha yake yote pamoja na kutembea nchini nyingi duniani Harry hakuwahi kuona nyumba ya kifahari kama iliyokuwa mbele yake, ilijengwa kwa mawe ya marumaru za kung’aa na iliezekwa vioo! Alipoingia ndani ya nyumba hiyo ndiyo alizidi kushangaa zaidi, kila kitu alichokiona ndani ya nyumba hiyo kilikuwa kigeni maishani kwake.
“Caroline, mumeo ni tajiri sana eh!”
“Kwanini?”
“Nyumba hii ni nzuri mno!”
“Ahsante!”
“Lakini utakubali kuwa na mimi tena wakati umeshazoea kuishi maisha ya kifahari?”
“Ninachotaka katika maisha yangu ni furaha hata kama nitalala chini, nakupenda Harry kuliko mwanaume mwingine duniani, nipo tayari kuacha vyote hivi kama utataka iwe hivyo!” Yalikuwa maneno ya Caroline ambayo Harry hakuyaamini hata kidogo ilikuwa si rahisi mwanamke kuacha mali na raha zote alizokuwa nazo kwa sababu ya mwanaume masikini kama yeye!
Dostları ilə paylaş: |