Maisha ya nabiiYüklə 0,69 Mb.
səhifə1/15
tarix10.12.2017
ölçüsü0,69 Mb.
#34382
  1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   15


Maisha Ya Nabii Muhammad (s.a.w.)MAISHA YA NABII

MUHAMMAD (S.A.W.)


مَنَاهِلُ الْمُتَّقِيْنَ فِيْ سِيْرَةِ رَحْمَةِ الْعَالَمِيْنَ

Chemchem Ya Wacha Mungu

Katika Sira Ya Rehema Ya Walimwengu

(2009)
Kimetungwa na:

Kadhi Al-Allamah Sheikh: Abdulla Salih

Al-Farisi (Zanzibar)

Kimetaarishwa Na Kutiwa Maelezo Na:

Abu Ammar, Nassir Muhammad Rashid Al –Mazrui

KAZI YANGU KATIKA KITABU HIKI


Kwa hakika ulimwengu wa Kiswahili ni maskini sana katika uwanja wa literature za dini: vitabu vilivyopo ni vichache sana. Hatuna fiq-hi za Kiswahili, hatuna Tafsiri isipokuwa chache sana. Mmoja wa wenye tafsiri hizo ni mtunzi wa Kitabu hiki Sheikh Al-'Allamah Abdullah Salih Al-Farisi. Lakini ni wazi kwamba yeye katika tafsiri hio hakukusudia kutia maelezo ya undani juu ya elimu ya tafsiri, bali alikusudia kuwaokoa watu wasije wakapotoshwa na uzushi na uwongo wa Kikadiani ambao waliandika uzushi wao na kuzipotosha Aya za Qur-an. Na Sheikh kuiandika tafsiri yake kwa nia hio, inaonesha aliiandika kwa ikhalasi ya hali ya juu ya kutaka radhi za Mola wake tu. Na bila shaka anayeisoma tafsiri yake, basi anaona nuru ya ikhlasi inaanza kung'aa tangu juu ya gamba la tafsiri hio.
Alichokifanya ndugu yangu Nassir Muhammad Rashid Al-Mazrui, katika kitabu hiki, ni kukiandika upya kitabu hiki kwa kompyuta. Kisha akakitia maelezo ya chini. Maelezo yote ya chini kayatia yeye, isipokuwa ziko baadhi ya sehemu chache ambazo kuna maelezo ya Sheikh Abdallah Salih Al-Farisi mwenyewe. Katika kila penye maelezo hayo ya Sheikh Al-Farisi, huweka katika breketi maneno haya (Sheikh Abdullah Salih Al-Farisi). Kwa mfano, utakuta humu maelezo ya chini yasemayo "Mbingu hazijulikani hakika yake ni nini". Maelezo hayo ni ya Sheikh Abdallah Salih Al-Farisi mwenyewe, na kwa hivyo, baada ya maelezo hayo, mtayarishaji wa kitabu kaandika katika breketi maneno: (Sheikh Abadallah Saleh Al-Farsi), ili kutafautisha baina ya maelezo ya Sheikh Al-Farisi na maelezo yake Al-Akh Nassir Al-Mazrui. Asili ya maelezo hayo ya Sheikh Al-Farisi yalikuwa ndani ya kitabu, lakini utaona yanapendeza zaidi kukaa katika maelezo ya chini.
Vile vile katika kitabu cha asili liliandikwa neno “Qureshi” yaani kwa “Q” na baadhi ya wakati liliandikwa neno hilo hilo kwa herufi “K” yaani "Kureshi", hata ilifika hadi kuandikwa neno hili ndani ya msitari mmoja kwa uandishi tofauti. Kwa mfano, Sheikh alipokuwa anazungumzia vita vya Uhud alisema katika uk. 56 wa kopi hiyo ya asili kuwa: “Baada ya Mtume (s.a.w.) kumpiga yule Qureshi, Makureshi wengine…” Kwa hivyo, Ndugu Nassir Al-Mazrui yeye aliona kuwa ni jambo la busara iwapo litatumika neno hili kwa aina moja tu ya uandishi, na kwa hivyo alichokifanya ni kubadilisha kila penye “Q” kuweka “K” kwani hili si lenye kuathiri maudhui ya kitabu.

Ama kwa upande wangu, mimi nimeyapitia tu maelezo hayo ya Al-Akh Nassir Al-Mazrui, na nikaona kwamba kawafikishwa sana. Nimezidisha katika kitabu chenyewe neno (s.a.w.) katika sehemu zote ambazo Sheikh kamtaja Mtume (s.a.w.) pasi na kuweko sala hii ya Mtume (s.a.w), ima alisahau kumsalia au ilikuwa ni kughafilika kwa mpiga taipu Bwana Ali Hassan Mirza aliyekuwa Mwalimu katika Government School Zanzibar. Kwa hivyo, nikijua kwamba kuzidisha neno hilo hakuongezi fikra mpya ambayo mwenyewe hatoiridhia, bali kwa sababu kumsalia Mtume (s.a.w.) anapotajwa ni wajibu bila ya tafauti yoyote kwa Waislamu, basi nimeonelea bora kuliongeza kila anapotajwa.


Pia nikaona kuwa nikiongezee kitabu hicho jina la Kiarabu ambalo nahisi litavutia zaidi, nikaongeza jina مَنَاهِلُ الْمُتَّقِيْنَ فِيْ سِيْرَةِ رَحْمَةِ الْعَالَمِيْنَ Manahilu Al-Muttaqin Fii Sirati Rahmati Al-'Aalamin. Neno "Manahil" ni wingi wa neno "Manhal" na maana yake ni chemchem, na kwa hivyo ilitakiwa tafsiri iwe: "Chemchem za.." lakini badala yake nimekiita kwa Kiswahili Chemchem Ya Wacha Mungu Katika Sira Ya Rehema Ya Walimwengu, badala ya "Chemchem za." Hii ni kwa kutafuta ladha ya matamshi ya Kiswahili: nahisi hivyo kinaleta ladha zaidi.

Basi hii ndio juhudi yangu, na juhudi kubwa zaidi kwanza kaifanya Mtunzi, pili akifatiwa na Ndugu yangu Nassir aliyekitayarisha na kukitia maelezo. Tunamuomba Allah aijaalie kazi hii iwe ni kwa kutaka radhi zake na atupokelee na wote walioshiriki kwa hali na mali zao kufanikisha kazi hii.


Ahsatum.

Ndugu yenu katika dini:

Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui.

Tarehe 3/3/2009 sawa na 6/ Mfunguo Sita 1430 H.

Al-qurm Muscat Oman.


DIBAJI YA CHAPA YA KWANZA
Ninamshukuru Mwenye – ezi – M’ngu kwa kuniwezesha kutunga kitabu hiki – Maisha ya Nabii Muhammad (s.a.w.) – ambacho ninafikiri ndicho kitabu cha kwanza cha namna hii kutungwa na Muislamu kwa lugha ya Kiswahili. Uislamu umeanza miaka mingi katika nchi zetu hizi za Mashariki ya Afrika. Lakini kutunga kitabu kwa lugha hii ni jambo la karibuni hivi.

Kabla wasomaji wangu hawajaanza kuyasoma yaliyomo katika kitabu hiki, naomba wazione shukurani zangu juu ya mabwana hawa wema na wengineo ambao baadhi yao watanisamehe kama sitayataja majina yao hapa, ingawa nimewashukuru moyoni. Ninamshukuru:
 1. Bwana L . W. Hollingsworth: M . B . E . B . A . aliyekuwa Principal wa Government Secondary School Zanzibar na mtengenezaji wa Gazeti la “Mazungumzo ya walimu wa Unguja” Bwana huyu alikuwa akinitia hima kila siku kuendelea kuandika makala yangu juu ya “Maisha ya Nabii Muhammad” ambayo sasa yanatokeza katika sura ya kitabu kidogo. Na yeye ni mtu wa mwanzo kunipa shauri ya kuyakusanya makala hayo yawe katika sura ya kitabu.
 1. Bwana Abdallah Ahmad Seif Al-Hatimiy: aliyekuwa Principal wa R . B . School (Dole).
 1. Bwana Abdallah Muhammad Al-Hadhramy: Headmaster wa Government Central School Zanzibar. Wao wakinitia nguvu zile zile alizokuwa akinitia Bwana Hollingsworth na wote watatu ni walimu wangu.
 1. Bwana Muhammad Abdul-Rahman Al-Hamdany: aliyekuwa mwalimu katika Rural Boarding School – Dole – Zanzibar, na rafiki tangu utoto wetu mpaka kufa kwetu Inshallah. Bwana huyu aliyapitia makala yangu yote baada ya kumalizika, akayasoma moja moja akanionyesha kila kisichofaa kuwapo nipate kukiondosha, na kila kinachofaa kuwapo ili nikitia kikiwa hakipo, nami nilimfuata katika yote hayo. Kwani yeye ni mtu wa kufuatwa rai zake.
 1. Bwana Ali Hassan Mirza: Mwalimu katika Government School Zanzibar, na mmoja katika marafiki zangu wakubwa sana miongoni mwa marafiki zangu wengi. Rafiki yangu mwema huyu alikuwa akinipigia taipi kila nakala moja katika makala yangu 69 kabla ya kwenda kupigwa chapa bila ya kukimwa wala kufanya ukunguni. Akizipiga taipi tena kabla ya kwenda kufanywa kitabu.

Vile vile simsahau Bwana Muhammad Salim Hilal Al-Barwany, wala Bwana Amour Ali Ameir Al-Marhuby, wala Bwana Juma Aley Al-Abrawy kwa makala yao waliokuwa wakiandika kukisifu kitabu hiki kabla ya kuwa kitabu. Mwishoni namshukuru ndugu yangu Bwana Shaaban Saleh Abdallah wa Government School Zanzibar, katika kumsaidia Bwana Ali Hassan Mirza kupiga taipi muswada “Manuscript” wa kitabu hiki.


Kadhalika nitapenda kuwajulisha wasomaji wangu baadhi ya vitabu nilivyovisoma sana hata nikaandika haya yaliyomo katika kitabu hiki, ili yoyote akitaka kujua ithbati yake arejee hapo. Akisadiki atakuwa anavisadiki hivyo, na akipinga atakuwa anavipinga hivyo. Na kila binaadamu ni mwenye kumrejesha mwenziwe akikosa au ni mwenye kurejeshwa akikosa. Hakuna aliekamilika ila Mungu. Vitabu vyenyewe ni hivi:
1. Siratu Ibni Hisham: Kitabu cha Imamu Muhammad bin Is-haq aliekufa mwaka 151 A.H ambacho ndicho sahihi kuliko vitabu vya tarehe vyote vinavyotaja habari za Mtume (s.a.w.) , nacho ndicho kitabu cha mwanzo kuandika tarehe ya Mtume (s.a.w.) . Kitabu hiki kinajuilikana kwa jina la “Siratu Ibni Hisham” Jina la Bwana mkubwa aliyekiongeza yanayostahiki na akayotoa yasiyostahiki. Huyo Bwana Abdul Malik bin Hisham alikufa mwaka 213 A.H.
2. Siratul Halabiyya: Kitabu cha mwanachuoni mkubwa wa Kishafi, Sheikh Nuruddin Ali Halaby aliekufa mwaka 1044 A.H.
3. Siratun Nabawiyya: Kitabu cha Sayyid Ahmad Dahlan, Mufti wa Hijaz nzima zama zake. Bwana huyu alikufa mwaka 1304 A.H.
4. The life of Muhammad: Cha Sir William Muir aliekufa 1905 A.C.
5. Hayat Muhammad: Kitabu cha Muhammad Hussein Haykal Pasha. Waziri wa Taalimu wa Misri kila Hizbu Ahrar inapokamata Wizara, na mwandikaji mashuhuri.
6. Muhammadun Rasulu Llah: Cha Bwana Muhammad Ridha wa Skuli kubwa ya Misri inayoitwa Al-Jamial Misriyya. Na vingi vyengine lakini hivi ndivyo nilivyovisoma sana.

16 Mfunguo Nne 1361

3 rd June 1942. ABDALLAH SALEH ABDALLAH AL-FARSY.
MAMBO YALIYOMO
SURA YA KWANZA: ---------------------------------------------------21

Nasaba ya Nabii Muhammad (s.a.w.) -----------------------------------22

a. Wazee wake wanaume ----------------------------------------22

b. Wazee wake wanawake ---------------------------------------24


SURA YA PILI: -----------------------------------------------------------27

Kuzaliwa kwa Nabii Muhammad (s.a.w.) na Maisha ya utoto wake-----------------------------------------------------------------------------------28 1. Kunyonyeshwa kwake --------------------------------------30

 2. Kufa kwa Mama yake ---------------------------------------31

 3. Kulelewa kwake na Babu yake Bwana Abdul Muttalib-----------------------------------------------------------------------32

 4. Kufa kwa Babu yake Bwana Abdul Muttalib-------------33

 5. Kulelewa kwake na Baba yake mdogo, Bwana Abu Talib--------------------------------------------------------------------33

 6. Kujifunza kwake ---------------------------------------------34

SURA YA TATU: ---------------------------------------------------------35

Maisha ya Ujana wa Nabii Muhammad (s.a.w.) ----------------------36


 1. Sifa zake -------------------------------------------------------36

 2. Safari zake za biashara --------------------------------------37

 3. Kuingia katika chama cha kusaidia Wanyonge ----------39

 4. Wake aliowaowa ---------------------------------------------41

 5. Watoto na wajukuu wa Mtume (s.a.w.) ------------------47

 6. Baba wadogo wa Mtume (s.a.w.) -------------------------51

 7. Wajomba zake na mama zake wadogo --------------------53

 8. Kujengwa Al-Kaaba -----------------------------------------53

SURA YA NNE: -----------------------------------------------------------55

Kupata Utume Nabii Muhammad (s.a.w.) ------------------------------56


 1. Namna za kuletwa Wahyi -----------------------------------58

 2. Kuamrishwa kufundishwa dini -----------------------------59

 3. Waislamu wa awali kabisa ----------------------------------60

 4. Kutangaza dini kwa siri -------------------------------------63

 5. Kuidhahirisha dini -------------------------------------------64

SURA YA TANO: --------------------------------------------------------66

Kuteswa kwa Waislamu --------------------------------------------------67


 1. Wakubwa wa kuwatesa Waislamu -------------------------68

 2. Watu walioadhibiwa kwa ajili ya dini yao ----------------69

 3. Waliorejea katika Ukafiri kwa ajili ya adhabu zilizowakuta ---------------------------------------------------71

 4. Nasaha walizotoa Makureshi kumpa Mtume (s.a.w.)- --71

 5. Rai walizotoa Makureshi kumpa Bwana Abu Talib -----73

 6. Kuhamia Masahaba Uhabushia ----------------------------74

SURA YA SITA: ----------------------------------------------------------76

Mambo yaliyotokea baada ya mwaka wa tano wa Utume ----------77


 1. Kusilimu kwa Sayyidna Umar -----------------------------77

 2. Kupigwa pande kwa Banii Hashim na Makureshi -------77

 3. Kuvunjwa mkataba wa Makureshi -------------------------79

 4. Kufa kwa Bwana Abu Talib --------------------------------82

 5. Kwenda Miraji ------------------------------------------------84

SURA YA SABA: ---------------------------------------------------------92

Kuwafundisha dini Waarabu wasiokuwa Makureshi -----------------93


 1. Kusafiri kwake na kwenda Taif na kusilimu kwa Majini ---------------------------------------------------------------------93

 2. Kutangaza Uislamu siku za kuhiji -------------------------97

 3. Kusilimu kwa watu wa Madina ---------------------------101

 4. Kuhama Masahaba kwenda Madina ---------------------104

 5. Masahaba wa mwanzo waliohamia Madina ------------105

 6. Mkutano wa Makureshi kwenye nyuma ya Mashauri--108

SURA YA NANE: -------------------------------------------------------110

Kuhamia Mtume (s.a.w.) Madina -------------------------------------111


 1. Kwenda kwa Mtume (s.a.w.) mwenyewe Madina ----111

 2. Safari ya Mtume (s.a.w.) na Sayyidna Abubakar kwenda Madina -------------------------------------------------------113

 3. Kuwasili Mtume (s.a.w.) Madina ------------------------120

 4. Mji wa Madina ----------------------------------------------123

 5. Kukaa Mtume (s.a.w.) nyumbani kwa Bwana Ayyub----------------------------------------------------------------------123

 6. Kujengwa msikiti wa Madina na nyuma za Mtume (s.a.w.)--------------------------------------------------------124

 7. Kuja Madina watu wa Mtume (s.a.w.) na wa Sayyidna Abubakar -----------------------------------------------------126

h. Kupangwa udugu baina ya Muhajirina na Ansar---------128

 1. Kuamrisha Mtume (s.a.w.) baadhi ya Masahaba zake kujifunza lugha ya Kiyahudi ------------------------------130

 2. Kusilimu kwa baadhi ya wanavyuoni wa Kiyahudi ----131

SURA YA TISA: ---------------------------------------------------------133

Vita vya Jihadi na makusudio yake ------------------------------------134

Vitimbi ambavyo makafiri wa Kiarabu wamemfanyia Mtume (s.a.w.) na Masahaba zake walipokuwa Madina -----------135 1. Kuonyesha kuwa Uislamu haukusimama kwa upanga-137

 2. Tafsiri ya baadhi ya Aya za Quran zinazotaja Jihadi --140

SURA YA KUMI: -------------------------------------------------------143

Vita vikubwa alivyopigana Nabii Muhammad (s.a.w.) -------------144


 1. Vita vya Badr ------------------------------------------------144

 2. Vita vya Uhud -----------------------------------------------155

 3. Vita vya Khandak -------------------------------------------164

 4. Vita vya Hunayn --------------------------------------------172

SURA YA KUMI NA MOJA: -----------------------------------------181

Kupatana Mtume (s.a.w.) na Makureshi -----------------------------182


 1. Sulhu ya Hudaybiya ----------------------------------------182

 2. Kwenda kulipa Umra waliyozuiliwa kuifanya na Makureshi ----------------------------------------------------192

SURA YA KUMI NA MBILI: -----------------------------------------194

Kuwapelekea barua Wafalme waliokuwa karibu na Bara Arabu---195


 1. Hirak (Heraclius) Mfalme wa Dola ya Kirumi ---------195

 2. Kisra Ibarwiz (Chosroes Ebarwiz) -----------------------196

 3. Najash As-ham ----------------------------------------------196

 4. Makaukis (Pkauchios) --------------------------------------198

 5. Hawdha bin Ali Al-Hanafy --------------------------------200

 6. Mundhir bin Sawa At-Tamimy ---------------------------200

 7. Harith bin Abi Shami Al-Ghassany ----------------------200

 8. Harith bin Abi Kulal Al-Himyar --------------------------201

9-10. Jayfar bin Julanda na Abd bin Julanda Al-Azdy --------201
SURA YA KUMI NA TATU: -----------------------------------------204

Kusilimu Bara Arabu yote ----------------------------------------------205 1. Kwenda kuiteka Makka ------------------------------------205

 2. Wakuu wa Kiarabu waliokuwa wakija kwa Mtume (s.a.w.) kusilimu--------------------------------------------214

SURA YA KUMI NA NNE: -------------------------------------------216

Kuhiji ----------------------------------------------------------------------217


 1. Kuhiji kwa Sayyidna Abubakr-----------------------------217

 2. Kuhiji Mtume (s.a.w) hija ya kuaga----------------------217

SURA YAKUMI NA TANO: ------------------------------------------223

Kufa kwa Nabii Muhammad (s.a.w.) ----------------------------------224


DIBAJI


Bismillahi Rahmanir Rahim
Nimeduwaa na kalamu kwa muda wa saa nyingi nikifikiri niandike nini kitoshe kuwa ndio furaha yetu Waislamu kwa mafunzo tuliyoyapata ya Maisha ya Mtume (s.a.w.) kutokana katika kitabu cha Qadhi Sheikh Abdulla Saleh Farsy, alichokitunga kiitwacho “Maisha ya Nabii Muhammad” ni kweli kwamba hakuna malipo yoyote sisi wanaadamu tuwezayo kumlipa, bali ni kumuomba Mwenyezi Mungu amlipe kila ya kheri.
Qadhi Sheikh Abdulla Saleh ndiye mtu wa kwanza aliyetunga kitabu cha namna hii kwa lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kimeanzwa kupigwa chapa tangu mwaka 1942, ambapo mpaka sasa ni miaka 251 na bado kinaaniwa na kila msomaji hata imekuwa hii ni chapa ya 152. Hakingeaniwa namna hii ila ni kwa sababuya yaliyomo ndani yake. Mtungaji kaeleza maisha yote ya Mtume (s.a.w.), na msomaji hatakuwa na mushkeli wowote kwani kaeleza kwa namna ya kifundi na ya kuelea sana.
Kitabu cha awali cha dini kwa lugha ya Kiswahili kilichoanza kunifikia machoni mwangu ni kitabu hiki “Maisha ya Nabii Muhammad”. Baada ya kukisoma tu nikaelewa na mengi na kufungukiwa na mengi na nilimhisi mtungaji wake kuwa ni mtu wa busara kabisa. Mwenye busara mawazo yake hubashiri. Niliamua kuwa sikubali kamwe nisimwone na kusoma kwake. Mawazo hayo nilikaa nayo kwa muda wa miaka michache, na kwa baraka za Mwenyezi Mungu alinijaalia nikenda huko Unguja na kusoma kwake kwa muda wa miaka kadhaa. Ya kweli yasemwe mimi kutunga kwangu vitabu ni kwa sababu ya kushawishiwa na kitabu hiki. Kwa bahati nzuri nilipokutana na mtungaji, nikawa ni kipenzi chake, na akawa ndiye anaevisahihisha vitabu vyangu na kunitia hima kubwa na kunipa moyo na kuendelea na kazi hiyo.
Na idadi kubwa ya vitabu alivyovitunga Qadhi huyu, na kila kimoja kinashindana na mwenzake kwa uzuri na ufasaha wake. Ndivyo nilivyowaambia wenzangu tulipokuwa tukizungumza habari zake, sioni kwa nini nisitie ubeti mmoja wa shairi wa kufungia dibaji hii. Ubeti huo ni huu:-
Kitabu hiki “Maisha Ya Nabii Muhammad”

Wengi kimewafundisha Mafundisho mengi hadi

Wakajua vya kutosha Maisha yake Sayyidi

Shekhe wetu mwenye sudi Mungu ampe baraka.


SAID MUSA

TAREHE ZILIZOMO NDANI YA KITABU HIKI

ANGALIA: B.U. – Baada ya Utume. A.H. – Al Hijra

497---------------------- Kazaliwa Bwana Abdul Muttalib

540--------------------- Kazaliwa Bwana Abutalib.

545 -------------------- Kazaliwa baba yake Mtume (s.a.w.) .

546--------------------- Kazaliwa mama yake Mtume (s.a.w.) .

Agosti 570 Rajab ----- -- Kaolewa mama yake Mtume (s.a.w.) .

Aprili 571-12 Mfunguo sita-- Kazaliwa Mtume (s.a.w.) .

576 ----------------------------- Kafa mama yake Mtume (s.a.w.) (Bibi Amina).

578 -------------------------------Kafa babu yake Mtume (s.a.w.) Abdul

Muttalib.

582 ------------------------------ Mtume (s.a.w.) kenda Sham mara ya kwanza.

590 Mfunguo pili---------------Kufunguliwa chama cha kusaidia

wanyonge.

595 ----------------------------- Mtume (s.a.w.) kenda Shama mara ya pili.

595 ------------------------------Mtume (s.a.w.) kamwoa Bibi Khadija.

605---- --------------------------- Kujengwa Al-Kaaba.

Disemba 610-17 Ramadhan--Umeletwa Utume.

610 --------------------- Kuamrishwa kufundisha dini.

613-------------- 4 B.U Kuzaliwa Bibi Aysha.

Oktoba 615 Rajab --------- 5 B.U Wamekwenda Masahaba nchi ya

Mahabushia mara ya kwanza .

Mei 616 Mfunguo tatu---5 B.U Kasilimu Sayyidna Umar.


April 617 Mfunguo nne -- 7 B.U Wamepigwa pande Banii Hashim

na Makureshi wote.

Januari 620 Mfunguo mosi--10 B.U Kuvunja Mkataba wa Makureshi.

Januari 620 ---------------- 10 B.U Kufa kwa Bwana Abu Talib na

Bibi Khadija.
Februari 620 Mfunguo pili-- 10 B.U Kwenda Mtume (s.a.w.) katika Taif.

Machi 620 Mfunguo tatu---10 B.U Kaolewa Bibi Sawda na Mtume

(s.a.w).
Oktoba 620 Rajab-------------11 B.U Kusilimu watu wa Madina.

Machi 621 Mfunguo tatu-----1 B.U Kapewa ahadi Mtume (s.a.w.)

na Ansar.
Oktoba 621 Rajab-------------- 12 B.U Kwenda Miraji Mtume (s.a.w.)

na kufaradhishwa sala tano.

Machi 622 Mfunguo tatu--------12 B.U Kapewa ahadi Mtume (s.a.w.) na Ansar kuwa watamhifadhi yeye na watu wake pindi wakenda Madina.

Aprili 622 Mfunguo nne--------13 B.U Wameanza Masahaba kwenda Madina.

Mei 622 Mfunguo tano----------13 B.U Wamekutana Makureshi

katika nyumba yao ya mkutano ili kufanya shauri ya kumwua Mtume (s.a.w.)

20 Sept. 622. 12 Mfunguo sita--13 B.U Amefika Mtume (s.a.w.)

Pamoja na Sayyidna Abubakr mtaa wa Kubaa.

Januari 623 Mfunguo mosi------2 A.H. Kaolewa Bibi Aysha na Mtume (s.a.w.) .

Disemba 623 Shaaban----------- 2 A.H. Imefaridhiwa kufunga Ramadhan na kutoa Zaka.

Januari 624 Ramadhan-----------2 A.H. Vita vya Badr.

Januari 624 Ramadhan-----------2 A.H. Kafa Bibi Rukayya – mtoto mwanamke wa Mtume (s.a.w.)

Agosti 624 Mfunguo nane-------3 A.H. Kaolewa Bibi Umu Kulthum na Sayyidna Uthman.

Nov. 624 Shaaban---------------- 3 A.H. Mtume (s.a.w.) kamwoa Bibi Hafsa.

Disemba 624 Ramadhan---------3 A.H. Kazaliwa Bwana

Hassan bin Ali bin Abi Talib.

Januari 625 Mfunguo mosi------3 A.H. Vita vya Uhud.

Juni 625 Mfunguo mosi----------2 A.H. Mtume(s.a.w.) kamwoa Bibi Zaynab bint Khuzayma.

Nov. 625 Shaaban-----------------4 A.H. Kuzaliwa Bwana Huseyn bin Ali bin Abi Talib.

Februari 626 Mfunguo pili------4 A.H. Mtume(s.a.w.) kamwoa Bibi Hind bint Abi Umayya.

Juni 626 Mfunguo tano----------5 A.H Mtume(s.a.w.) kamwoa Bibi Zaynab bint Jahsh.

Disemba 626 Shaaban-----------5 A.H. Mtume(s.a.w.) kamwoa Bibi Juwayria.

Februari 627 Mfunguo mosi-----5 A.H. Vita vya Khandak.

Januari 628 Mfunguo mosi-------6 A.H. Imefaridhiwa Kuhiji

Februari 628Mfunguo pili--------6 A.H. Imefanywa Sulhu ya Hudaybiya.

Agosti 628 Mfunguo nane--------7 A.H. Bibi Ramla bint Abi

Safyan amekuja Madina

Spt. 628 Mfunguo tisa-------------7 A.H. Kaolewa Bibi Safiya bint Huyay na Mtume (s.a.w)

628 -----------------------------------7 A.H. Kapelekewa barua

Mfalme Hariki.

Februari 629 Mfunguo pili-------7 A.H. Mtume (s.a.w.) amelipa

Umra aliyozuiliwa.

Februari 629 Mfunguo pili-------7 A.H. Mtume (s.a.w.) kumwoa Bibi Maymuna.

629 ---------------------------------- 8 A.H. Kafa Bibi Zaynab –

mtoto mwanamke wa

Mtume (s.a.w) –

Januari 630. 10 Ramadhan--------8 A.H. Wameondoka Madina

kwenda kuiteka Makka.

Januari 630. 20 Ramadhan--------8 A.H. Imetekwa Makka.

Februari 630 Mfunguo mosi------8 A.H. Vita vya Hunayn.

Aprili 630 Mfunguo tatu---------- 8 A.H. Kuzaliwa Bwana

Ibrahim mtoto wa

Mtume (s.a.w)

Oktoba 630 Shaaban---------------9 A.H. Kafa Bibi Ummu Kulthum – mtoto mwanamke wa Mtume (s.a.w.) –.

630 -----------------------------------9 A.H. Kafa Najash. As-ham Mfalme wa Mahabushia

Juni 631 Mfunguo sita------------10 A.H. Kafa Bw. Ibrahim

mtoto wa Mtume (s.aw)
Februari 632 Mfunguo pili------- 10 A.H. Kaondoka Mtume

(s.a.w) Madina kwenda

kuhiji Hija ya kuaga.

Machi 632 Mfunguo tatu-----------10 A.H. Amefika Mtume (s.a.w.) Makka.

Machi 632 Mfunguo tatu-----------10 A.H. Wamesimama Arafa.

Machi 632 Mfunguo tatu-----------10 A.H. Wameondoka Makka kurejea Madina.

632 Mfunguo tatu------------------- 10 A.H. Wamerejea Madina.

632-------------------------------------10 A.H. Kupelekewa barua Wafalme wa Oman.

8 Juni 632. 12 Mfunguo sita------- 11 A.H. Kufa kwa Mtume (s.a.w.) .

10 Juni 632. 14 Mfunguo sita------11 A.H. Kuzikwa kwake.

Disemba 632 Ramadhan------------11 A.H. Kafa Bibi Fatma – mtoto wa Mtume (s.a.w.) –.

641-------------------------------------20 A.H. Kafa Bibi Zaynab bint Jahsh – mkewe Mtume (s.a.w.) – .

664------------------------------------ 44 A.H. Kafa Bibi Ramla – mke wa Mtume (s.a.w.) –.

668 ------------------------------------ 48 A.H. Kafa Bibi Hafsa – mke wa Mtume (s.a.w.) –.

670 -------------------------------------50 A.H. Kafa Bwana Hassan bin Ali bin Abi Talib.

672 -------------------------------------51 A.H. Kafa Bibi Maymuna – mke wa Mtume (s.a.w.)–

672 -------------------------------------51 A.H. Kafa Bibi Safiya – mke wa Mtume (s.a.w.) –.

673 -------------------------------------52 A.H. Kafa Bwana Abu Ayyub.

675 -------------------------------------54 A.H. Kafa Bibi Sawda – mke wa Mtume (s.a.w.) –.

676 -------------------------------------56 A.H. Kafa Bibi Juwayriya – mke wa Mtume (s.a.w.)–

677 -------------------------------------57 A.H. Kafa Bibi Aysha – mke wa Mtume (s.a.w.) –.

681 -------------------------------------61 A.H. Kafa Bwana Husseyn bin Ali bin Abi Talib.681 -------------------------------------61 A.H. Kafa Bibi Hind bint Abi Umayya – mke wa Mtume (s.a.w.) –


Yüklə 0,69 Mb.

Dostları ilə paylaş:
  1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   15
Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2023
rəhbərliyinə müraciət

    Ana səhifə