Sababu ya kumpiga tunayo! Nia ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga Nduli Idi Amin tunayo, ni lazima tumpige!Yüklə 0,95 Mb.
səhifə16/18
tarix31.10.2017
ölçüsü0,95 Mb.
#23549
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   18

Rais aliyekuwa madarakani kwa wakati huo, Pedro Kinasho aliiongoza nchi hiyo chini ya chama cha SPMD, kwa hakika katika kipindi hicho chama hicho kilishapoteza umaarufu na chama cha CKMW ndicho kilikuwa kikitamba nchini humo. Mwaka huo ndio ulikuwa mwaka wa kwanza kwa nchi ya Sokomoni kushiriki uchaguzi wa vyama vingi.

Kwa sababu lengo la Harry lilikuwa ni kutumia pesa aliyokuwa nayo ili aingie madarakani, alijichomeka katika chama hicho kama mfadhili lakini lengo lake likiwa ni baadaye kushika uongozi wa chama hicho na kugombea Urais, alikuwa kijana mdogo mno lakini kwa sababu alikuwa na pesa watu wengi ndani ya chama hicho walimwamini katika muda mfupi na kumtaka hata aongoze chama chao.

“Lengo langu si kuongoza chama wala nchi hii ninataka kusaidia tu!” alisema Harry kila alipohojiwa na waandishi wa habari.

Harry hakutaka kuionyesha nia yake waziwazi lakini miezi michache baadaye alijikuta akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho na kukubali mara moja ni kipindi hicho ndio alimwaga pesa zaidi katika chama, chama chake kikapata umaarufu kupita kiasi, watu wengi walikihama chama Tawala na kujiunga na chama chake! Ilikuwepo kila dalili kuwa chama cha CKMW kingeshinda na kuingia Ikulu na hiyo ingemfanya Harry kutimiza lengo lake la kuwa Rais!

Hata mara moja Harry hakuwahi kumfikiria Caroline na mambo aliyomfanyia, kwanza alikuwa na uhakika Caroline alikuwa marehemu! Asingeweza kutoka mikononi mwa Wavietnam salama.

“Acha afe ni jambo la kawaida wakati mwingine kuua ili uingie Ikulu tena ni afadhali mimi nimeua mtu mmoja tu! Vipi wanaua mamia ya watu kama inavyotokea huko Bosnia na nchi nyingine?” Aliwaza Harry, mpaka wakati huo alikuwa na uhakika asilimia mia moja ni yeye ndiye angekuwa Rais wa nne wa nchi ya Sokomoni na alihakikisha hilo linawezekana kwa kutembea kila pembe ya nchi ya Sokomoni akipiga kampeni na kumwaga misaada mbalimbali kwa wapiga kura, pamoja na umri wake kuwa mdogo wananchi wa Sokomoni walimwamini na kuahidi kumpa nchi.

**************

Kizunguzungu kilizidi kumbana Caroline akiwa amesimama nje ya vyoo ndani ya ndege hiyo, ilikuwa tayari ni sekunde ya ishirini na tano tangu aiguse sumu aliyoitumia kuwapaka O’brien na wenzake! Kwa mujibu wa mzee Nelson aliyempa sumu hiyo kama asingenawa katika muda wa sekunde thelathini hata yeye angekwenda na maji! Milango yote ya chooni ilikuwa imefungwa na ndani yake ilisikika milio kama ya pikipiki ndogo aina ya Vespa ambazo hupatikana sana Zanzibar, hapakuwa na dalili yoyote ya watu hao kufungua milango ya vyoo ili Caroline anawe, kwa hakika alijua kifo chake kimefika. Alijitemea mate mikononi ili anawe lakini hayakutosha na alipoiangalia saa yake ya mkononi tayari ilikuwa ikikimbilia sekunde ya ishirini na tisa.

“Siwezi! Siwezi kufa naona hivihivi!” Alijisemea kwa sauti ya chini Caroline.

Bila aibu yoyote Caroline alichuchumaa, akalegeza sketi yake na kuishusha chini kwa kasi ya ajabu na aliishusha pamoja na nguo yake ya ndani, alikuwa amepata jibu la tatizo lake kama vile maji yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye mpira wa maji uliotoboka ndivyo mkojo wake ulivyomtoka, aliutumia mkojo wake mwenyewe kunawa tena kwenye veranda ya ndege.Hakuona aibu wala kuwa na hofu yoyote moyoni mwake.

Wafanyakazi wa ndani ya ndege walikishuhudia kitendo alichokifanya na kwa haraka walitembea hadi sehemu aliyokuwa amechuchumaa na kuanza kumhoji maswali, alionekana kutokuwa na jibu la kuwaridhisha lakini kwa sababu alikuwa mteja hawakuwa na jambo la kumfanya.

“My bladder was full, I had nothing to do except this!”(Mfuko wangu wa mkojo ulikuwa umejaa na sikuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya hii!) aliwajibu wafanyakazi hao huku akitabasamu.

Kwa jinsi wafanyakazi wa ndege hiyo walivyoambiwa juu ya Caroline, alikuwa mgonjwa aliyekuwa akisafirishwa kwenda nyumbani kwao Canada, kwa sababu hiyo hawakushangazwa sana na kitendo alichokifanya walifikiri yote yaliyotokea yalikuwa ni sababu ya ugonjwa wake,hawakukasirishwa sana na kitendo hicho na badala yake walimsaidia na kumrudisha hadi kitini ambako alikaa na kujifanya amelala.

Kutoka mahali alipolala hakusikia sauti wala kelele yoyote ya mhemo wala mkoromo kutoka mdomoni wala puani mwa O’brien na Kennedy aliolala katikati yao, hiyo ilimwonyesha kabisa kuwa tayari walishakata roho! Aliponyoosha mikono yake yote miwili kujaribu kuwagusa, alishangazwa na jinsi miili yao ilivyokuwa migumu, ilikuwa ni kama ubao. Bila kutegemea alijikuta akinyanyuka na kuketi, akamfunua Kennedy na kumwangalia, mwili wake ulishabadilika rangi na kuwa kama mkaa. Alishangazwa na jinsi sumu hiyo ilivyofanya kazi, katika muda mfupi tayari ilishaua.

“Mh! Hii sumu si mchezo! Sijui aliitengeneza kwa kutumia nini?” Aliwaza Caroline, aliwapekua Kennedy na O’brien mifukoni na kuwakuta wakiwa na jumla ya Dola laki mbili na nusu za Kimarekani zote alizichukua na kuzizamisha katika nguo yake ya ndani, alifurahi kuzipata pesa hizo na aliamini ni lazima zingemfikisha Tanzania ambako msako wake wa mauaji ungeendelea, alikuwa amepania kuua, kuwaua watu wote waliomfanyia mabaya zaidi sana alitamani kumuua Harry.

Dakika chache baadaye sauti ya msichana akitangaza kuwa ndege ingetua kwenye uwanja wa ndege wa Ottawa katika muda wa dakika kumi na tano ilisikika, msichana huyo aliwataka watu kukaa vitini, kunyoosha viti vyao na kufunga mikanda yao vizuri kabla ndege haijatua, ili kuepuka viti vya akina Kennedy kurekebishwa na wafanyakazi wa ndege jambo ambalo lingefanya igundulike kuwa walikuwa wamekufa, Caroline aliifanya kazi hiyo mwenyewe na kuwafunika vizuri kwa kofia zao usoni kama vile walikuwa usingizini. Kwa sababu ya kukakamaa hawakuweza kukaa vizuri.

“Can I help you?”(Nikusaidie?) mmoja wafanyakazi wa ndege alimuuliza Caroline.

“Thanks! I appriciate.......”(Ahsante! Ninakushukuru......!)

“Why is he so stiff?”(Kwanini amekakamaa kiasi hiki?) Mfanyakazi wa ndege aliuliza akitaka kumgusa O’brien.

“No!No!No!No! dont disturb, let him enjoy his sleep!”(Hapana! Hapana! Usimsumbue! Mwache afaidi usingizi wake) alisema Caroline kwa sauti ya juu, mfanyakazi huyo alionekana kushangazwa na mabadiliko aliyokuwa nayo Caroline aliyepakiwa ndani ya ndege akiwa hajitambui kabisa.

“How are you doing at the moment?”(Unajisikiaje sasa hivi?)

“Very fine!”(Najisikia vizuri!)

“You were so sick when the brought you!”(Ulikuwa unaumwa sana walivyokuleta!) Aliuliza mfanyakazi wakati akiondoka kuelekea kwenye kiti chake na dakika kumi baadaye ndege ilikuwa ikiserereka ardhini kwenye uwanja wa Ottawa.

Moyo wa Caroline ulidunda! Alijisikia hofu kubwa kupita kiasi, alijua kwa hakika nje ya uwanja alikuwepo Dk. Ian akimsubiri kwa ajili ya kumuua, ilikuwa ni lazima afanye chochote kilichowezekana lakini asiingie mikononi mwa mzee huyo mwenye roho mbaya.Tayari alishawaua Kennedy na wenzake hivyo kilichokuwa mbele yake ni kutoroka tu.

Alikuwa mtu wa kwanza kufika mlangoni ndege iliposimama na kutulia, alifanya kila kitu kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha kuwa hagunduliki na hakuna mfanyakazi yeyote wa ndege aliyemwona wakati akitembea kuelekea mlangoni.Mlango ulipofunguliwa alikuwa mtu wa kwanza kuziteremka ngazi kutoka ndani ya ndege hiyo abiria wengine wengi walifuata nyuma yake. Alijua wazi muda si mrefu angekuwa akitafutwa hivyo ilikuwa ni lazima apotee kabla mambo hayajaharibika.

Ingawa hakujua ni mlango gani angepitia lakini hakuwa tayari kupitia mlango wa kawaida wa abiria ambako ni lazima angekutana ana kwa ana na Dk. Ian na huo ndio ungekuwa mwisho wa maisha yake.

“Pesa ni sabuni ya roho! Kwa pesa hii niliyonayo lazima nitatoka uwanjani bila kujulikana!” Alijipa moyo Caroline.

Baada tu ya kuteremka aliizunguka ndege na kuanza kukimbia akiwa ameinama kuelekea upande wa pili wa kiwanja kulikokuwa na majengo makubwa yaliyojengwa kwa mabati, hakujisikia mgeni sana kuwa nchini Canada, nchi hiyo ilikuwa ni kama nyumbani kwa sababu aliishi hapo muda mrefu enzi za mapenzi yake na Dk. Ian. Pamoja na hayo yote bado mwili wake ulitetemeka kwa hofu kubwa aliyokuwa nayo moyoni mwake.Alijua nje ya uwanja huo kulikuwa na mtu aliyekuwa na hamu kubwa ya kumuua kama kisasi kwa mabaya aliyomfanyia..

“wo!wo!wo!” Zilikuwa ni sauti za kundi la Mbwa kama watano hivi waliokuwa wakibweka huku wakimkimbiza Caroline, nyuma yao alikuwepo askari mwenye bunduki! Mbio hizo zilimfikisha kwenye uzio wa senyenge uliokuwa mwisho wa kiwanja hicho, hapakuwa na sehemu zaidi ya kwenda! Mbwa walipomfikia walimvamia na kumwangusha chini, walianza kumuuma kwa meno mpaka askari alipofika na kuwaamuru waache.

“Who are you?”(Wewe ni nani?)

“Marione!” Alidanganya.

“Why are you running? Are you a crack dealer?”(Kwanini unakimbia? Wewe ni muuza madawa ya kulevya?)

“No!No! Not at all!”(Hapana! Hapana!)

“Then why are running?”(Sasa kwanini unakimbia?)

“Listen, can you save my life?”(Sikiliza, unaweza kuokoa maisha yangu?)

“It depends!”(Inategemea!)

“What if I give you ten thousands USD? Will you let go of me?”(Vipi kama nikikupa dola elfu kumi utaniachia niondoke?)

“Definately!”(bila shaka!)

Bila kusita wala kupoteza muda Caroline alilipandisha gauni lake na kuingiza mikono yake ndani ya nguo ya ndani na kulichomoa bulungutu la noti alilokuwa nalo na kuhesabu dola elfu kumi, akamkabidhi askari huyo! Meno yote thelathini na mbili ya askari yalionekana, ilikuwa furaha kubwa mno kwake, kuingia kazini na kutoka na dola elfu kumi?ni jambo ambalo hakulitegemea kabisa siku hiyo.

“Then show me the way out of the Airport without being noticed!”(Nionyeshe njia ya kutoka nje ya uwanja wa ndege bila kugundulika!)

“Come with me!”(Nifuate!) Aliamuru askari na Caroline alianza kumfuata kwa nyuma, mbwa wote walikuwa kimya hakuna hata mmoja aliyediriki kubweka.

“Mtu wa hatari yuko ndani ya uwanja! Tayari amekwishaua watu watatu kwa sumu, maaskari kaeni chonjo! Mtu huyu ni mwanamke, ni hatari na inaaminika anaua kwa kutumia sumu ya kukausha mwili!” Ilikuwa ni sauti kutoka katika spika zilizokuwepo uwanjani hapo, ilisikika wakiwa wametembea kama hatua ishirini hivi mbele, bahati nzuri kwa sababu ya kubabaika na pesa alizopewa askari hakuisikia sauti hiyo lakini Caroline alijua muda si mrefu angesikia na mambo yangebadilika.

Alijikunja na kulishika pindo la gauni lake, akaanza kulipapasa taratibu mpaka alipofikia sehemu alipoizamisha sumu yake, aliingiza vidole viwili katika sehemu aliyoifumua na kuivuta karatasi ilimofungwa sumu hiyo, aliifungua taratibu na kuchukua kiasi kidogo kwa kutumia vidole viwili, gumba na cha shahada baada ya kumaliza alikiingiza kikaratasi ilimofungwa sumu ndani ya pindo la gauni lake.

Sauti ya spika ziliendelea kutangaza juu ya mtu aliyekuwa akitafutwa, Caroline alishindwa kuelewa ni kwanini askari huyo hakusikia, bila kusita wakati wakitembea alimsogelea na kumwekea mkono wake begani, hapohapo akampaka sumu.

“Let me empty my bladder!”(acha nikojoe kwanza!)

“No problem just go on!”(Hakuna tatizo endelea!)

Caroline alitembea kwenda pembeni ambako alichuchumaa na kuanza kukojoa huku akiutumia mkojo wake mwenyewe kuinawa sumu aliyoigusa kwa mikono yake, alipomaliza alinyanyuka na kuendelea kumfuata askari.

“Is it very far from here?”(Ni mbali sana kutoka hapa?)

“No! we’re ab...out to be the...re!” (Hapana tumekaribia kufika!) alisema askari na sekunde chache baadaye alianguka chini kama mzigo na kutulia tuli! Kuona hivyo mbwa walianza kubweka kwa nguvu, alipogeuka kuangalia nyuma kundi kubwa la watu waliovaa mavazi ya rangi nyeusi lilikuwa likija mbio kuelekea eneo alilokuwa, alipotaka kukimbia mbwa mmoja alimrukia na kuliuma gauni lake.

Je, nini kitatokea? Je, Caroline atafanikiwa kuondoka uwanja wa ndege au ataingia mikononi mwa Dk. Ian? Fuatilia wiki ijayo!

I

likuwa ni ndani ya uwanja 
wa ndege wa Ottawa, tayari 
ilishatimu saa 2:30 ya usiku, Caroline alikuwa akijaribu kujiondoa mdomoni mwa mbwa walioling’ata gauni lake, walikuwa ni mbwa wanene na wenye nguvu kiasi kwamba ilikuwa kazi ngumu kuling’oa gauni lake katikati ya meno yao! Mbwa wengine walikuwa wakibweka na kundi kubwa la watu ambalo baadaye aligundua walikuwa ni maaskari lilizidi kumkaribia na hatimaye kumfikia.Maaskari waliwaamuru mbwa waache kumshambulia Caroline na walitii amri hiyo, mwili wake wote ulikuwa ukitetemeka kwa hofu! Kukamatwa kwake kulimaanisha kuingia mikononi mwa Dk. Ian na hilo lilimaanisha kifo chake na kama si kuingia mikononi mwa Dk. Ian angeingia mikononi mwa sheria kwa kosa la kuwaua O’brien na wenzake na kama ingethibitika alitenda kosa hilo kwa sheria ya Canada ilivyokuwa angehukumiwa kifo kwa kuchomwa sindano ya sumu.

Mawazo hayo yalimfanya aumie sana moyoni mwake, hakutaka kufa kabla hajalipiza kisasi kwa Harry na wenzake na hakutaka kufa kabla ya kuwaona wazazi wake, hakuwa na fikra hata kidogo kuwa baba na mama yake walikuwa katika mji huohuo tena ndani ya mateso makali, waliteswa kila siku na Dk. Ian kama kisasi kwa kitendo alichofanya mtoto wao.

“Haiwezekani ni lazima nijiokoe!”Aliwaza Caroline wakati akinyanyuliwa ardhini na mmoja wa maaskari na kuanza kupigwa kwa kirungu kichwani, alipasuka juu ya jicho na kuanza kuvuja damu!

“Who are you?”(Wewe nani?)

“Me?”(Mimi?)

“Yeah! who do you think is the shit am I speaking to?”(Ndiyo! Wewe unafikiri ni kinyesi gani ninayeongea naye?) Aliuliza askari kwa ukali.

“I’m Marione!”(Mimi ni Marione!)

“Why are you running?”(Kwanini unakimbia?)

“They want to kill me! I beg you to save my life and I will pay you any amount of money if you won’t let me out of the airport through the front exit”(Wanataka kuniua, naomba muokoe maisha yangu! Nitawalipa kiasi chochote cha pesa kama tu hamtanipitisha mlango wa mbele wakati wa kutoka ndani ya uwanja!)Caroline aliongea huku mkono wake tayari ukiwa umeshika noti kumi za dola mia mia! Ilikuwa si rahisi kukumbuka ni muda gani alizitoa sehemu alipozificha! Alikuwa ameamua kutumia pesa kujiokoa.

Jeshi la polisi nchini Canada katika kipindi hicho lilikuwa katika wakati mgumu, ni wiki hiyo hiyo wanajeshi wa jeshi hilo pamoja na wale wa zimamoto walikuwa wamegoma kufanya kazi sababu ya maslahi kidogo, wachache walikuwa kazini na hao walikuwa tayari kwa lolote ili mradi wameonyeshwa pesa, waliruhusu hata wafanyabiashara wa madawa ya kulevya kupita katika uwanja huo kama tu walipewa pesa!

Kitendo cha Caroline kuwatajia pesa kilikuwa ni faraja kubwa kwao, walipoona noti za dola mia mia mikononi mwake, walihisi mate yakiwadondoka! Tangu asubuhi ya siku hiyo walikuwa hawajapata rushwa ya aina yoyote, mmoja wao alizidaka pesa hizo kwa mkono wake wa kulia na kumwamuru Caroline asimame.

“Give us some more!”(Tupe zaidi ya hizi!)

“How much?”(Kiasi gani?)

“Ten thousand U$D!”(Dola elfu kumi!)

“That’s a lot!”(Hizo ni nyingi sana!)

“Then come with us!”(Basi tufuate!)

“No! I’m not ready!”(Hapana! Sipo tayari!) Alijibu Caroline, hakuwa tayari kupitishwa mlango wa mbele ambako kwa uhakika alijua Dk. Ian alikuwa akimsubiri tayari kwa kumuua, mpaka wakati huo alikuwa na uhakika kila kitu alichokifanya ndani ya ndege kilishajulikana na alishangaa ni kwanini maaskari hao walikuwa hawajagundua kilichotokea pamoja na vipaza sauti kuendelea kupita kelele na yeye mwenyewe Caroline kuvisikia.

Bila kuchelewa wala kusita alidumbukiza mkono wake ndani ya chupi alimoficha pesa zake, hakutaka kuzitoa zote, alijua maaskari wangeingiwa na tamaa baada ya kuziona na hata kumnyang’anya. Kwa utaalam wa ajabu huku akitumia mkono mmoja kama vile mtu aliyekuwa akijikuna ngozi yake ya ndani, Caroline alihesabu noti moja moja mpaka zikatimia nane kisha akazivuta na kuzitoa nje.

“This is the only money I have! Please help me out of the Airport through the rear gate!”(Hiki ndiyo kiasi pekee cha pesa nilichonacho! Tafadhali nisaidieni nitoke nje ya uwanja kupitia mlango wa nyuma!)

Hizo nazo askari alizidaka na wote walionekana kuridhishwa, walianza kutembea naye upande wa pili kulipokuwa na giza nene ambako walimweleza kulikuwa na mlango wa nyuma, vipaza sauti vilizidi kupiga kelele vikitoa taarifa juu ya mwanamke muuaji aliyekuwemo ndani ya uwanja, yeye alisikia kila kitu lakini maaskari walionekana kutotilia maanani maneno hayo.Mbele kidogo wazo liliingia kichwani mwa Caroline.

“I have to be very smart, I’m not supposed to leave any mark or foot steps behind me!”(Lazima niwe makini sana, sitakiwi kuacha alama yoyote nyuma yangu!) Aliwaza Caroline na ni dakika hiyo hiyo wazo la kuwaua maaskari wote waliokuwa wakimsindikiza lilimwijia, alijua hao ndio wangekuwa chanzo cha yeye kukamatwa baada ya kugundua ndiye aliyekuwa akitafutwa.

Aliinama na kuligusa pindo la gauni lake mahali alimoficha kipaketi chenye sumu aliyopea na mzee Nelson porini, yeye aliita sumu hiyo sumu ya ukombozi ingawa iliondoa maisha ya watu katika kujiokoa kwake! Tayari kwa kutumia sumu hiyo alishauwa watu wanne na alijua mbele yake ilikuwa ni lazima aue watu wengi zaidi ikiwa ni pamoja na Harry, Richard, Reginald, Dickson na Leonard Katunzi, huyu alikuwa mwandishi wa habari aliyemwandika yeye magazetini kuwa alikuwa na kifafa! Alitaka kumuua sababu alimuaibisha sana.

Wakati ameinama maaskari waliokuwa naye walibaki kumshangaa bila kujua alichokuwa akifanya, haikumchukua hata sekunde tano kuitoa sumu hiyo kwenye pindo na kuishika mkononi, kwa sababu ya giza hakuna askari aliyegundua alichokuwa akifanya, akachukua kiasi kidogo cha unga huo na kuushika katika mkono wake wa kulia.

“Hawa nao zamu yao imefika, si walengwa lakini inabidi wafe ili wasikwamishe mipango yangu, nikiwaacha hai hawa lazima watatoboa siri na nitashindwa kuondoka Canada!” Aliwaza Caroline roho na akili yake ilishaharibika, hakuwa binadamu wa kawaida tena! Kwa wakati huo kwake kuua kilikuwa kitu kidogo sana ili mradi anaokoa maisha yake, hata yeye mwenyewe alijishangaa! Katika maisha yake hakuwahi kuwaza kitu kama kuua mtu.

“I have a bad thirsty can I have some water?” (nina kiu mbaya sana, naweza kupata maji kidogo?)

“We have watertapes everywhere, one of the tapes is right behind you!”(Kuna mabomba kila mahali uwanjani moja ya mabomba hayo liko nyuma yako!) mmoja wa maaskari hao alimwambia Caroline.

Tayari walishalifikia kwenye geti la kutoka nje ya uwanja kupitia mlango wa nyuma, Caroline pesa zake zilikuwa zimemsaidia! Alichofanya ni kuanza kuwaaga maaskari hao kwa kuwapa mkono wake wa kulia uliopakwa sumu, alihakikisha anamgusa kila askari na sumu hiyo, alipomaliza aliwahi haraka sana kwenye bomba la maji lililokuwa nyuma yake na kunawa vizuri kisha akarudi mpaka mahali waliposimama maaskari na kuanza kuongea nao huku akiwashukuru kwa wema waliomtendea.

Alibaki nao kwa dakika kumi, halikuwa lengo lake kubaki eneo hilo lakini alitaka kuhakikisha sumu imefanya kazi miilini mwao ndio aondoke na kama ingeshindwa ingebidi awapake tena kwa mtindo huohuo wa kuagana.Zilipotimia kama dakika kumi hivi, alishangaa kumwona mmoja wa maaskari hao akiyumba na baadaye kuanguka chini haikuchukua muda mrefu akafuatiwa na mwenzake na kila aliyeanguka chini hakusema kitu chochote alibaki kimya akitupa miguu yake huku na kule, jumla ya maaskari saba walikuwa wamelala chini hiyo ikifanya idadi ya watu aliowaua kufikia kumi na moja.

Mbwa walianza kubweka tena, Caroline hakutaka kupoteza muda zaidi katika eneo hilo alichofanya ni kukimbia haraka kutoka nje ya ngome ya uwanja, mbwa walimfuata kwa nyuma lakini kabla hawajamfikia tayari alishafunga lango na kujisikia yuko salama. Aliangalia macho yake huku na kule kuona kama kulikuwa na mtu yeyote mwenye kusababisha hatari lakini macho yake hayakukutana na kitu chochote cha aina hiyo.

Alikichukua kipakiti chake na kukirudisha kwenye pindo la nguo yake, alikisukuma na kukiingiza ndani zaidi ili kisipotee, wazo la kurudi ndani na kuzichukua pesa alizowapa maaskari lilimwijia kichwani lakini aliogopa kufanya hivyo.

“Naweza kurudi nikapambana na matatizo bure!” Aliwaza Caroline.

Alichofanya ni kuanza kukimbia kuelekea mbele ya uwanja, ilimchukua kama dakika mbili tu akawa ameshajichanganya katikati ya makundi ya watu waliokuwepo uwanjani hapo bila kugundulika! Alifanya kila kitu kwa uangalifu, alielewa wazi msako dhidi yake ulikuwa ukiendelea. Alijificha nyuma ya nguzo kubwa ya jengo la uwanja akihakikisha asingeonekana, macho yake yalielekezwa kwenye lango kubwa la kutokea uwanjani.

Haikuwa kazi ngumu kwa macho yake kumgundua Dk. Ian, mwili wake wote ulitetemeka na alihisi mkojo ukimpenya, alimwogopa sana mtu huyo kwake ilikuwa ni bora kukutana na shetani ana kwa ana kuliko kukutana na Dk. Ian! Aliamini kifo chake kilikuwa mikononi mwa mwanaume huyo aliyewahi kuwa mume wake lakini yeye mwenyewe ndiye akayaharibu mambo baada ya kudanganywa na Harry, mwanaume aliyejifanya kumpenda.

Kwa harakaharaka alirudi kinyumenyume na kujificha nyuma ya mgahawa mkubwa wa McDonald uliokuwepo uwanjani hapo, alisimama eneo lenye giza akiwa na uhakika kwa asilimia mia moja kuwa asingeweza kuonekana, akiwa hapo aliweza kumwona Dk. Ian akiwa ameshika mikono yake kichwani akishuhudia machela tatu zikitolewa ndani ya uwanja huo, maiti za kina O’brien na wenzake zilikuwa zikitolewa nje ya uwanja.

Kila mtu aliyekuwepo uwanjani hapo alionekana kushangaa kupita kiasi, Caroline aliisikia sauti ya Dk. Ian kutoka sehemu aliyojificha ikifoka, mzee huyo aliahidi ni lazima ampate Caroline! Watu wengi hawakumwelewa. Caroline alisikia kila kitu na kuzidi kuingiwa na hofu.

“A serial killer is within the Airport, she is a woman! Tall, black and beautiful, she has already killed for men! If you suspect any person with the same features please notify the police immediately!”(Muuaji anayeua watu mfululizo yupo ndani ya uwanja, ni mwanamke, mrefu, mweusi na mzuri, tayari amekwishaua wanaume wanne! Kama ukimhisi mtu yeyote mwenye sifa kama hizo tafadhali julisha polisi haraka!) Sauti ya kipaza sauti iliendelea kusikika.

Kila mtu uwanjani hapo alionekana mwenye hofu, polisi walipita huku na kule wakijaribu kumtafuta mwanamke mwenye sifa zilizotajwa! Kuona hivyo Caroline aligundua eneo alilokuwa halikuwa na usalama, alikimbia kwa haraka akiwa ameinama hadi eneo yalipoegeshwa magari yaliyoonekana kama ya kukodi. Alilisogelea moja lililokuwa na dereva ndani yake na kufungua mlango.

“Yes madame! Need a ride?”(Ndiyo mama! Unahitaji usafiri?)

“Yes!”(Ndiyo!)

“Where should I take to?”(Nikupeleke wapi?)

“City centre!”(Jijini katikati!)

“Three U$D!”(Dola tatu!)

“No problem! If you drive fast and pass through the rat-rat routes I will pay you more!”(Hakuna matatizo na kama ukiendesha kwa kasi kupitia njia za panya nitakulipa pesa zaidi!) Alisema Caroline, kwa hofu aliyokuwa nayo mwili wake ulikuwa ukitetemeka! Dereva alimwangalia na kuonyesha mshangao.

Dereva alikuwa miongoni mwa watu waliolisikia tangazo la mwanamke aliyekuwa akitafutwa ndani ya uwanja wa ndege, muonekano wa Caroline ulimtia hofu kubwa, aliingiwa na wasiwasi kuwa huenda mwanamke aliyekuwa akitafutwa ndiye alikuwa ndani ya gari lake!

Hofu kubwa ilimpata na alihisi hata yeye angekuwa miongoni mwa watu ambao wangeuawa. Kwa kupitia kona ya jicho lake la kushoto aliweza kumchunguza Caroline kwa makini na bila shaka yoyote alijua ni yeye! Alishindwa kuelewa ni nini kingempata, jasho jingi lilimtoka kiasi cha kulowanisha shati alilovaa, mapigo yake ya moyo yalienda kasi kuliko kawaida.

Mbele kidogo walifika darajani, lilikuwa daraja kubwa ambalo chini yake ilipita treni ya umeme iliyokwenda kwa kasi, bila kutegemea Caroline alimwona dereva akifungua mlango wa gari lililokuwa likitembea kwa mwendo wa kasi, aliruka na kuachia usukani, gari lilianza kuacha njia! Caroline alijaribu kwa uzoefu wake wote kuzuia gari lisianguke lakini iliendelea kuserereka na kubinuka likijigonga kwenye vyuma vya pembeni mwa daraja! Mara ghafla tairi ya mbele ilipasuka, gari likarushwa juu na kuanza kuanza kudumbukia chini kulikokuwa na reli, lilipotua chini lilikuwa katikati ya reli na treni la umeme lilikuwa hatua chache kutoka mahali lilipokuwa gari.

“Mamaaaaaaaaaaaaaaaaaa!” Caroline alilia tena kwa kiswahili akijua mwisho wake ulikuwa umefika, mwisho bila kulipiza kisasi.


Kataloq: wp-content -> uploads -> 2017

Yüklə 0,95 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   18
Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2023
rəhbərliyinə müraciət

    Ana səhifə