Sababu ya kumpiga tunayo! Nia ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga Nduli Idi Amin tunayo, ni lazima tumpige!Yüklə 0,95 Mb.
səhifə7/18
tarix31.10.2017
ölçüsü0,95 Mb.
#23549
1   2   3   4   5   6   7   8   9   10   ...   18

“Nisaidie caroline wanataka kunihukumu kifo eti nilikubaka na kukupeleka porini kwa lengo la kukuua! Eti kweli nilifanya hivyo Caroline?”

“Sio kweli! Bila wewe mimi ningekuwa marehemu!”

Mahakama yote ilikuwa kimya hakimu alijua wazi kuwa Caroline alivunja utaratibu wa mahakama lakini alilazimika kunyamaza kwa sababu mguso alioupata kutokana na maneno ya caroline.

Wote wawili walikumbatiana na kupigana mabusu mfululizo usoni, yote hiyo ilikuwa ni furaha walionekana kama wapenzi, ingawa katika maisha yao hawakuwahi kuishi pamoja kwa hata masaa matatu.

Jaji aliwaacha wafanye walichotaka kwa sababu alijua kesi ilikuwa imefika mwisho wake, asingeweza kumfunga Reginald wakati mtu aliyedaiwa kufanyiwa unyama alikuwa akimtetea, alishangazwa sana na kilichotokea na hakutegemea caroline angeweza kufika mahakamani siku hiyo, ulikuwa ni kama muujiza.

“Mheshimiwa Jaji!” Caroline aliita.

“Naitwa Caroline! Mimi ninayediwa kubakwa katika kesi hii lakini ukweli wa mambo ninao mimi! Mheshimiwa Jaji Reginald hakunibaka wala si yeye aliyenipeleka porini bali ni Dickson yeye na mpenzi wangu Richard pamoja na msichana aitwaye Mariam Hassan waliniacha kwenye mashindano ya Miss Bongo ambako kwa bahati mbaya niliangu………!”

Alishindwa kumalizia sentensi yake kwa kuogopa kutaja kilichomuangusha mbele za watu lakini alieleza kila kitu kilichotokea na watu wote walikaa kimya wakimsikiliza yeye watu wengi akiwemo hakima walipigwa na butwaa na kushangazwa na habari alizozieleza Caroline, wengi walibadilisha misimamo yao na mtazamo waliokuwa nao juu ya Reginald.

Hata baba yake Caroline mzee John Kadiri naye alijisikia mkosaji ndani ya nafsi yake kwa ktiendo chake cha kutaka kumuua kwa sindano ya sumu kitandani wakati si yeye aliyemfanyia unyama mtoto wake, alimwonea huruma sana Reginald kwani aliteseka gerezani bure.

“Mheshimiwa hakimu Reginald hana hatia hata kidogo na ningekushauri umwachie huru na kama kuna uwezekano Dickson asakwe huyo ndiye aliyenifanyia unyama mimi, huyu Reginald ni msamaraia mwema aliyeokoa maisha yangu!” Alimaliza Caroline.

Minong’ono ya chinichini ilisikka mahakamani, Carolne alikuwa amefanya kazi yake ya kumuokoa Reginald kutoka katika mikono ya kifo tena zikiwa ni dakika chache kabla ya hukumu! Kila mtu alimwona Reginald ni mtu mwenye bahati kubwa maishani mwake na kama caroline asingefika mahakamani siku hiyo ni lazima angehukumiwa kifo!

“Kwa sababu ya maelezo ya msichana huyo sina sababu ya kumhukumu kijana huyu na kulirudisha suala hili polisi ili Dickson asakwe kwa udi na uvumba na kufikishwa mbele ya sheria tangu sasa Reginald upo huru!”

Reginald hakuyaamini macho wala masikio yake na alijikuta akilia machozi ya furaha na alimsogelea caroline walikumbatiana tena, mama na dada zake nao waliungana pamoja nao na kukumbatiana! Siku za huzini ilibadilika kuwa siku ya furaha kubwa kwao! Hakuna aliyekuwa tayari kuamini hatimaye Reginald alikuwa huru.

“Pole sana Reginald kwa yaliyokupata hii yote ni kwa sababu mimi sikuwepo, kuelezea ukweli huu!” caroline alisema wakati yeye na Reginald wakitoka nje ya mahakama ambako walialikwa na ndugu jamaa na marafiki wengi kwa furaha kubwa! Nje ya uwanja wa mahakama palibadilika na kuwa sehemu ya chereko na nderemo kufuatia hukumu hiyo.

“Pole sana kijana nafikiri utanisamehe hata mimi sikujua kwani si wewe uliyemfanyia ukatili mwanangu, nitaandaa sherehe jioni ili tuongee vizuri zaidi nafikiri utahudhuria!”

“Sina kinyongo mzee hata mimi nitapenda kukutana na wewe!”

Waliondoka mahakamani ndani ya magari yao kuelekea majumbani, Reginald aliondoka na mama pamoja na dada zake ndani ya gari la mmoja wa ndugu zake caroline, caroline aliondoka na baba yake, kwa teksi waliyokodi na jioni ya siku hiyo familia zote zilikutana katika hoteli ya continental ambako baba yake caroline pamoja na shangazi yake walifanya hafla walimwomba msamaha Reginald kwa yaliyotomtokea kwa sababu ya binti yao, caroline alimwonea huruma sana Reginald kwa yaliyompta, hasa kitendo cha kupoteza mguu kwa ajili yake alipopigwa risasi na polisi porini akijaribu kumwokoa.

Wakati wa sherehe hiyoiliyohudhuriwa pia na marafiki wengi Reginald na caroline waliongea mambo mengi kuhusu maisha yao Reginald alijaribu kumshawishi caroline kuwa yaliyotokea akubali kuwa mpenzi wake na ikiwezekana awe mke wake kabisa kwa sababu alipoteza mguu wake akijaribu kumuokoa.

Pamoja na kuujua ukweli caroline alikataa katakata alikuwa tayari kufanya jambo lolote kufidia lakini si kuwa na uhusiano kimapenzi na mwanaume yeyote yule duniani! Aliwachukia wanaume kwani walimsababishia matatizo makubwa na kumliza mara nyingi, aliuahidi moyo wake kutokuwa na uhusiano wa mwanaume kimapenzi.

“Haiwezekani Reginald ndio uliniokoa na ninashukuru sana uliniokoa lakini siwezi hata siku moja kuwa na uhusiano na mwanaume kimapenzi kwani wanaume wameniumiza mara nyingi sana!”

“kwanini?”

“Basi tu!”Alijibu caroline bado hakuwa tayari kuivujisha siri yake ya kifafa.

“Tafadhali fikiria suala hili mara mbili na ukumbuke mimi nimeharibu maisha yangu kwa sababu yako hata kama wengine walikuumiza mimi nitakupa furaha!” alisema Reginald akimshika caroline began.

“Kwani nilikumwambia baba yangu akulipe fidia itakuwa vibaya?”

“Sitaki kitu kingine zaidi yako caroline!”

“Hiyo haiwezekani kabisa Reginald, siwapendi wanaume na ningeomba tuongee mambo mengine vinginevyo itakuwa bai tena!” Alisema caroline akionyesha kuchukizwa na suala hilo na mawazo yake yalipompeleka kwa Richard, Harry na Dickson chuki yake dhidi ya wanaume iliongezeka maradufu!

“Wanaume ! Wanaume ni wanyama sana sitaki hata kuwasikia!”Alisema kwa sauti caroline.

“Kwanini?”

“Basi tu!”

Usiku wa manane shereha ilikwisha na waliachana kurejea majumbani mwao usiku wa siku hiyo katika usingizi caroline aliota ndoto akitembea na Reginald ufukweni wakiwa wamekumbatiana na kupigana mabusu lakini ghafla alitokea msichana mwingine na Reginald alimwacha caroline akilia na kuondoka na msichana huyo!

“Hii ndoto gani tena? Huyu naye ni wale wale tu!” aliwaza caroline huku akitetemeka kwa hofu!


Baada ya hapo waliendelea kuonana mara kwa mara na miezi michache baadaye Reginald alirudishwa kazini baada ya kutengenezewa mguu mzuri wa bandia ambao haikuwa rahisi hata kidogo kugundua alikuwa na kilema, aliendesha gari kama kawaida! Kituo chake cha kazi kilibadilishwa na kuhamishiwa jijini Dar es Salaam.

Hivyo walionana karibu kila siku na uhusiano wao ulizidi kukomaa kila siku iliyokwenda kwa Mungu! Lakini bado kifafa kiliendelea kumsumbua kila ilipofika tarehe yake ilikuwa ni lazima aanguke, kwa kuogopa aibu wazazi wake waliamua kumtafutia chuo nje ya nchi ingawa alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Caroline alijiunga na chuo kikuu cha Ottawa, siku ya kuiaga Tanzania alisindikizwa uwanja wa ndege na wazazi wake pamoja na Reginald wote wawli walilia wakati wakiagana, ilikuwa si rahisi kuamini walikuwa wakitenganishwa na elimu!

Alikuwa akienda nchini Canada kwa masom ya miaka mitatu katika Sayansi ya kompyuta na baada ya hapo alitegemea kuongeza elimu ya utawala hivyo alitegemewa kuishi nchini Canada kwa miaka isiyopungua minne!

Alishukuru kuondoka Tanzania kwani kama angebaki hata kwa mwezi mmoja lazima angekuwa hatarini, uzalendo ulishaanza kumshinda juu ya Reginald siku zote kijana huyo hakukata tamaa kumshawishi akubali kuwa mpenzi wake!

“Nakwenda Reginald nakushuruku sana kwa kampani yako!”

“Usinisahau caroline bado nakupenda na nitakupenda siku zote!”

“Ahsante Reginald!”

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa Reginald na ilimchukua muda mrefu kuyaona maisha yakiwa kawaida bila caroline.

Mwaka wa kwanza ulipita caroline akiwa Canada masomoni, na mawasiliano kati yao hayakukatika, waliandikiana barua pepe karibu kila siku na katika kila barua aliyoandika reginadl hakuchoka kumweleza caroline wazi kuwa penzi lake lilikuwa bado motomoto na alimwomba ajitunze ili kama uwezekano ungekuwepo siku moja wafunge ndoa!
Uvumilivu wa Reginald hatimaye ulianza kumfanya caroline aliamini penzi lake, lakini kitu kimoja alikionea aibu nacho ni siri ya kifafa, jambo hilo lilimfanya aogope kukubali ingawa alijisikia hoi katika mapenzi.

Akiwa mwaka wa pili rafiki yake mmoja waliyelala naye chumba kimoja raia wa Uingereza, Careen aliligundua tatizo lake na kuamua kumtafutia msaada.

“Ninamjua daktari ambaye amewatibu watu wengi sana hapa Canada, hata bibi yangu alikuwa na tatizo hili lakini hivi asa ni mzima!”

Kweli?”


“Ndiyo ukitaka nitakupeleka kwake!”

Siku mbili baadaye msichana huyo alimpeleka caroline kwa daktari mmoja bingwa wa magonjwa ya akili na ubongo ambaye alimpa caroline dawa za kutumia miezi sita, baada ya matumizi ya miezi sita hali yake ilibadilika akawa anapitisha hata mwezi mzima bila kuanguka kifafa.

Caroline alishangazwa na mabadiliko hayo ya afya yake akawa mtu wa furaha kubwa katika maisha yake kwani hakuwahi kutegemea katika maisha yake kuwa siku moja angepitisha hata mwezi mmoja bila kuanguka kifafa! Mabadiliko hayo yalimfanya aongeze bidii ya kuzitumia dawa hizo, hatimaye akawa anapitisha hata miezi mitatu bila kuanguka.

“Thanks you Careen!”(Ahsante Careen!) alimshukuru rafiki yake baada ya mwaka mzima kupita bila kuanguka.

Daktari alimwambia wazi kuwa katika maisha yake alitakiwa kunywa dawa hizo kila siku kwani kuacha kutumia dawea hizoiliyoitwa Centribarbitone, kwa siku saba kungemfanya siku ya nane aanguke tena!

Alipomaliza masomo yake baada ya miaka minane alikumbuka kununua dawa ya kutosha kuja nazo Tanzania.

Reginald alimtafutia kazi katika kampuni ya kompyuta ya network Africa, ambako aliajiriwa kama mtaalamu wa kompyuta na mkufunzi wa chuo kilichomilikiwa na shirika hilo! Uhusiano wake na Reginald ulizidi kukua na kukomaa! Caroline hakuwa na kipingamizi tena juu ya Reginald na kujikuta akifua mikononi mwake akawa mpenzi wake!

“Usihofu caroline mimi sitakuumiza maishani mwako!”

“Naamini Reginald nimekufanyia uchunguzi kweli unanipenda Reginald na ahsante sana kwa uaminifu wako!”

“Nashauri tufunge ndoa caroline au unaonaje?”

“Sina kipingamizi!”

“Kweli?”
”Ndiyo!”

Taarifa zilitolewa kwa wazazi wa pande zote mbili na mipango ya harusi ilifanywa kwa muda wa mwaka mzima, yalikuwa maandalizi mazito lengo likiwa ni kufanya harusi ambayo ingelitingisha jiji la Dar es Salaam.

Mpaka wakati huo Reginald hakuelewa kitu chochote kuhusu kifafa cha mchumba wake na wala hakufahamu nini kilichomfanya awachukie wanaume kiasi hicho, caroline pia hakuwa tayari kutoboa siri hiyo.

Siku nane kabla ya harusi yao caroline aligundua kuwa dawa zake zilikuwa zimekwisha alipiga simu kwa daktari wake Canada akiomba atumiwe haraka iwezekanavyo maana bila dawa hizo lazima angeanguka siku ya harusi.

“Harusi yetu itakuwa nzuri sana Reginald au siyo?”

“Sana! Maaandalizi yake ni ya nguvu!”Waliongea wakipita madukani kutafuta baadhi ya vitu kwa ajili ya harusi yao, ghafla walipokaribia kufika kwenye dula la SH Amon, waliona kundi la watu wamekusanyika ikabidi nao pia wasogee karibu kabisa ili kuona ni kitu gani kilitokea.

“Kuna nini?”Reginald alimuuliza kijana mmoja.

“Fika mwenyewe uone braza ni aibu !Kwini kafanya noma anatembea mtaani wakati anajua wazi mambo yake si safi!”

“Kivipi?”

“Fika uone mwenyewe braza!” Reginald na caroline walipenya katikati ya watu kwenda hadi mbele ili kuona ni kitu gani kilichokuwepo, walishangaa kukuta msichana mzuri akiwa amelala chini mapovu yakimtoka mdomoni.

“Masikini msichana mzuri ana kifafa!” Reginald aliongea kwa sauti.

Katika maisha yake ingawa caroline alikuwa na ugonjwa huo hakuwahi kumwona mtu aliyeanguka kifafa! Lilikuwa ni jambo la kusikitisha sana msichana mzuri alirusha mikono yake huku na kule akiuma meno yake, caroline aliogopa kuangalia na kuanza kumvuta Reginald ili waondoke.

“Twende!”

“Acha niangalie bwana!”

“Sitaki tuondoke!”

Reginald hakubisha sana walianza kuondoka pamoja kwenda dukani SH Amon kununua mavazi ya harusi pamoja na vipodozi.

“Reginald nikuulize swali?”

“Uliza!”

“Hivi ikitokea mpenzi wako akiwa na ugonjwa huu unaoweza kufanya kitu gani?”

“Ha! Kifafa mimi mwanamke mwenye kifafa wa kazi gani!”

Maneno hayo yalikuwa mkuki kwa caroline na alimwaga machozi mengi kupita kiasi, aliumia kugundua kuwa hata Reginald ipo siku angekuja kumwacha.

“Mbona unalia?”

“Ah!Ah! Ah! Ah! Basi tu!”

“Basi tu nini?”

Caroline hakujibu mawazo yalikuwe kwenye vidonge vyake alishindwa kuelewa kama vingewahi kabla ya siku saba!”

“Kama dawa hizi hazitafika sijua nitafanya kitu gani? Nitaanguka siku ya harusi!”Aliwaza caroline.

Zikiwa zimebaki siku mbili alipopiga simu aliambiwa na daktari wake kuwa dawa zilitumwa siku nne kabla kutoka Canada alishangaa ni kwanini zilikuwa hazijafika mpaka siku hiyo!
Je nini kitaendelea? Dawa zitawahi? Fuatilia wiki ijayo

Siku mbili kabla ya harusi yao ilikuwa ni hekaheka tupu nyumbani kwa shangazi yake na Caroline Upanga, kila mtu alikuwa na furaha na maandalizi yalikuwa yakienda vizuri, wazazi wa Caroline walikuwepo jijini Dar es Salaam kwa wiki nzima kutoka Arusha kwa ajili ya kuishuhudia harusi ya mtoto wao pekee.

Kilichowashangaza wengi siku tatu za mwisho walionekana watu wasio na furaha kabisa tofauti na walivyotegemewa kuwa, jambo hilo liliwafanya watu wengi kujiuliza maswali mengi.

“Labda hawakutaka mtoto wao aolewe na mlemavu kama Reginald!”

“Sasa hata kama hawakutaka watafanya nini wakati mtoto wao kampenda mlemavu? Isitoshe nasikia Reginald alipigwa risasi na kuvunjwa mfupa akimwokoa huyuhuyu Caroline alipotaka kuuawa na jambazi porini sasa wanataka aolewe na nani zaidi yake au upendo gani uzidi hapo?” yalikuwa ni maongezi ya baadhi ya majirani walioielewa vizuri historia ya Caroline na Reginald.

Wazazi wa Caroline hawakuonekana na furaha hata kidogo pamoja na kuwa mtoto wao pekee alikuwa akiolewa! Ni kweli hawakuwa na furaha na sababu ya jambo hilo haikuwa nyingine bali ni hofu ya aibu ambayo ingewapata baada ya mtoto wao kuanguka kanisani wakati wa kufunga ndoa, hilo ndilo walilolitegemea baada ya Caroline kuwaeleza kuwa dawa zake zilikuwa zimekwisha.

Walishindwa kuelewa nini kingefanyika kuzuia jambo hilo lisitokee walichanganyikiwa na matumaini yao yote yalikuwa ni kwa mzigo wa dawa aliokuwa umetumwa na Dk. Ian, daktari wa wa Caroline kutoka Canada,waliamini bila dawa hiyo Caroline angeanguka na ingekuwa aibu, hilo ndilo lililowatia hofu zaidi.

Si peke yao waliokuwa na hofu hiyo, Caroline ndio aligubikwa na wasiwasi zaidi yao,hakuelewa ni kitu gani angefanya ili kujiepusha aibu iliyokuwa mbele yake! Suluhu peke yake ilikuwa ni dawa lakini alishindwa kuelewa zilikwama wapi! Kadri masaa yalivyozidi kujivuta kwa kasi ndivyo wasiwasi wake ulivyozidi kupanda alihisi angepatwa na presha na kufa! Alikuwa tayari kwa hilo lakini si kuanguka kanisani mbele ya Reginald kwa kifafa.

“Mama kwanini msimwambie mama yake na Reginald tuahirishe harusi hii?”

“Tumejaribu hivyo, yeye alikuwa tayari kukubali lakini wajomba zake na Reginald walikataa kabisa wakidai wametumia pesa nyingi sana kujiandaa na hawana muda wa kusubiri!”

“Mliwaeleza ni kwanini mlikuwa mkiahirisha harusi?”

“Ndiyo!”

“Mlisemaje?”

“Kuwa utakuwa katika hedhi!”

“Ah! Mama hiyo tu haitoshi ungewaambia nina ugonjwa mkubwa!”

“Sasa tufanya nini?”

“Kwa kweli kama dawa hazitafika mimi sitakwenda kanisani kufunga ndoa hiyo kesho kutwa!”

Suala la kifafa lilichukua furaha yote yake na ya wazazi wake yote, walinyong’onyea kiasi cha kila mtu kugundua kulikuwa na tatizo mioyoni mwao ni shangazi yake Caroline peke yake ndiye aliyejitahidi kuchangamka ili kuondoa aibu hiyo.

Waalikwa wote walishajiandaa kwa ajili ya harusi na gharama kubwa zilishatumika hivyo haikuwa rahisi kuihairisha, kila mtu alishapania Reginald aliona masaa yakienda taratibu kupita kiasi, kila mara alimpigia Caroline simu na kuiongelea siku ya ndoa yao! Alionyesha furaha kubwa isiyo kifani lakini alishangazwa na hali ya kupotea kwa uchangamfu wa Caroline kadri siku ya ndoa yao ilivyozidi kukaribia!

“Caroline una tatizo nini?”

“Mimi?”


“Wewe ndiyo kwani naongea na nani?”

“Sina tatizo lolote!”

“Sasa kwanini uko hivyo?”

“Basi tu ndoa inanitia hofu!” Caroline alijitahidi kadri ya uwezo wake kutomwonyesha Reginald kuwa alikuwa na tatizo lililomsumbua moyoni mwake, hakutaka kabisa aelewe kuwa alikuwa na kifafa! Hiyo ilikuwa ni siri ya kufa nayo moyoni mwake.

**************

Yakiwa yamebaki masaa ishirni na nne ili ndoa yao ifungwe Reginald alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu na mtu huyo hakutaka kabisa kutaja jina lake,alidai yeye na Caroline walisoma shule moja mjini Arusha! Alichokisema katika simu hiyo kilimtia Reginald simanzi kubwa moyoni mwake na hakikuwa kitu rahisi kwake kukiamini.

“Kaka Reginald pole sana!”

“Kwanini?Maandalizi ya harusi?”

“Hapana pole kwa sababu unaoa kifafa!”

“Ninaoa kifafa? Una maana gani kusema hivyo kwanza wewe ni nani?”

“Hakuna haja ya kunijua jina ila nataka tu kukueleza kuwa Caroline ni mgonjwa wa kifafa na huanguka kati ya tarehe 26na 28 ya kila mwezi! Mimi nilisoma na ni kifafa ndicho kilichomfanya aachwe na mpenzi wake wa kwanza, Harry alipoanguka siku ya sikukuu yake ya kuzaliwa na nimesikia pia aliachwa na Richard kijana aliyeko gerezani alipoanguka siku ya Miss Bongo! Wewe kweli hujui? Au unapenda kifafa? Basi oa!” Baada ya maneno hayo tu simu ilikatika.

Reginald hakuridhika na maneno hayo kwani katika maisha yake hakuwahi hata mara moja kumwona Caroline ameanguka kifafa! Na hata hiyo tarehe 26 na 28 alikuwa naye lakini hakuanguka.

Alichukua kalamu na karatasi na kuanza kunakili namba hizo kwenye karatasi, bila kuchelewa aliipiga tena namba hiyo kwa kutumia simu yake ya mkononi lakini haikupokelewa wala kuingia,aliendelea kuipiga kwa muda mrefu lakini jibu liliendelea kuwa hilo hilo kuwa ilikuwa haipatikani!

Reginald alishindwa kuelewa asimame wapi, upande mmoja wa akili yake ulimwambia adharau lakini mwingine ulitaka ahakikishe! Alitaka kufahamu zaidi juu ya habari hiyo, ni kweli maneno hayo yalimuumiza sana moyo wake, hakuna kitu alichokiogopa maishani mwake kama ugonjwa wa kifafa na Ukoma!

Kumbukumbu zilimiminika kichwani akajikuta akiikumbuka siku yeye na Caroline walipomwona msichana aliyeanguka kifafa maeneo ya posta jijini! Alilikumbuka swali la Caroline akimuuliza kama ingetokea msichana wake akawa na kifafa angefanya kitu gani.

“Alibadilika sana nilipomjibu kuwa siwezi kuwa na msichana mwenye kifafa! Na alilia machozi, tangu jibu hilo alikosa raha kabisa nafikiri suala hili lina ukweli fulani ndani yake,si vyema kulipuuzia ni lazima nikamuulize Caroline upesi na kama ni kweli nitaachana naye leo hii hii! Sitajali gharama kubwa kiasi gani itapatikana!”Aliwaza Reginald.

Aliondoka kuelekea nyumbani kwa shangazi yake na Caroline upanga lakini kabla ya kufika aliamua kupita nyumbani kwao ambako alimweleza mama yake juu ya taarifa ya simu aliyoipokea.

Mama yake hakusikitika wala kushtushwa na habari hiyo, ilionekana si ngeni kwake.

“Mh! Reginald wewe ndio umesikia leo mwanangu?”

‘Ndiyo mama!”

“Mbona sisi tunafahamu na tulifikiri hata wewe unaelewa!”

“Hapana mama sasa kwanini hamkuniambia?”

“Tulifikiri unalifahamu jambo hilo!”

“Kama ni hivyo hakuna ndoa mama! Hebu ngoja niende kwanza nyumbani kwao nikamuulize Caroline mwenyewe!”Alisema Reginald na kutoka nje ambako aliingia ndani ya gari lake na kuanza kuendesha kwa kasi kuelekea Upanga.

Alipofika alishangazwa na umati mkubwa alioukuta mahali pale! Kulikuwa na shamshashara ya kila namna, aliwaona kama walikuwa wakipoteza muda wao kuimba na kuchambua mchele wakati hapakuwa na ndoa tena.

Alipobisha hodi mlango ulifunguliwa na shangazi yake Caroline, aliingia hadi sebuleni ambako aliwakuta baba na mama yake Caroline na kuwaamkia, alishangazwa na muonekano wa nyuso zao! Walionekana kama wakosaji na macho yao yalijaa aibu!

Baada ya salamu alipelekwa moja kwa moja hadi chumbani kwa Caroline, kitu cha kwanza alichogundua Caroline baada ya kumwona Reginald ni wekundu wa macho na alijua kulikuwa na tatizo, hakuwahi kumwona Reginald katika sura hiyo tangu amfahamu!

“Reginald vipi?”

“Vipi nini? Kwanini umeamua kunitia hasara kiasi hiki Caroline?”

“Hasara gani? Reginald mbona sikuelewi?”

“Ulijua kabisa una kifafa na hukuniambia kwanini lakini?”

Sentensi hiyo iliufanya moyo wa Caroline kufa ganzi, alishindwa kuelewa ni nani hasa aliyemwambia Reginald juu ya habari ya siri hiyo, aliinamisha uso wake kwa aibu na kuanza kulia machozi, hakusema kitu mpaka dakika kumi baadaye Reginald alipotaka kufahamu ukweli.

“Caro tafadhali niambie ukweli kumbuka harusi ni kesho! Je kweli una kifafa?”

Caroline alifikiria kumwambia Reginald ukweli lakini alishindwa kufanya hivyo sababu alijua kufanya hivyo kungemaanisha kuachwa na mwanaume kwa mara ya tatu maishani mwake sababu ya ugonjwa, alimpenda sana Reginald na hakutaka kutengana naye!

Alibubujikwa na machozi mengi na kilio chake kilifika hadi sebuleni, mama na shangazi yake walikwenda hadi chumbani kutaka kujua kilichotokea.

“Vipi tena watoto mbona mnalia?”

“Mama!”

“Naam!”


“Samahani naomba mtupe nafasi tuna maongezi kidogo!”Reginald alitamka akimwambia mama yake Caroline na bila kugoma mama aliyaheshimu maamuzi yao na wote wawili walitoka nje kutoa nafasi kwa watoto kuongea juu ya suala walilokuwa nalo!

“Caroline tafadhali nieleze ukweli juu ya jambo hili nahitaji kufahamu!”

“Watu hawapendi mimi na wewe tuoane Reginald!Kweli umeamua kuwasikiliza!”

“Ina maana ni uongo?”

“Ndiyo!Mimi sina kifafa Reginald ni maneno ya watu, ingekuwa hivyo katika muda wote huo si ningeshaanguka?”

Reginald alikaa kimya na kutafakari kwa muda wa kama dakika tano, hatimaye alifikia uamuzi wa kuyaona maneno yote aliyoyasikia kuwa ni majungu ya watu wasiopenda yeye aoe msichana mzuri kama Caroline!

Alimkumbatia na kumwomba msamaha, alimpiga mabusu usoni na Caroline aliyajibu huku akitabasamu! Kwa Reginald yakawa yamekwisha lakini kichwani kwa Caroline yaliendelea kumsumbua kwa sababu alijua wazi alikuwa na ugonjwa huo na hakuwa na dawa ya kuzuia kifafa kisimtokee siku iliyofuata ambayo ndiyo ilikuwa ya mwisho kuishi bila dawa za kuzuia asianguke. Ndani ya moyo wake bado aliujua ukweli kuwa bila dawa ni lazima angeaibika tu!

Mpaka jioni ya siku ya Ijumaa bado mzigo wake wa dawa ulikuwa haujafika, ilibidi apige tena simu Canada kwa daktari wake kumuulizia mahali dawa zilipokuwa, safari hii alimweleza kitu kilichotarajiwa kutokea bila kumficha kuwa hakutaka mchumba wake afahamu kuwa alikuwa mgonjwa!

“Once he knows that I have got epilepsy, he wont marry me doctor please help me?”(Kama akijua tu nina kifafa hatanioa, tafadhali daktari nisaidie)

“So?”(Sasa?)

“Serve my life doctor!”(Okoa maisha yangu daktari) alisema Caroline huku akilia katika simu alijua msaada pekee alikuwa ni Dk. Ian.

“It takes 14 hours flying from Ottawa to Dar es Saalam will I be there before your wedding!”(Huchukua masaa 14 kuruka kwa ndege kutoka hapa Ottawa hadi Dar es Salaam nitawahi kabla ya harusi yako?)

“Yes sir!”(Ndiyo bwana!)

“Will you pay for my tickets?”(Utalipia tiketi zangu?)

“Sure!Just make me escape this shame!”(Hakika, niepushe tu na aibu hii)

“I will be there tomorrow around 10:30, because I will be leaving tonight!(Nitakuwa hapa kesho kwani nitaondoka leo usiku!)

“Thank you I will appreciate you!’(Ahsante, nitashukuru sana daktari)

Jibu hilo lilimrudisha matumaini Caroline moyo wake ulitulia kiasi cha kutosha na hata alipowapa wazazi wake taarifa hiyo kila mmoja alirejewa na furaha yake na pilikapilika za maandalizi ya mwisho ya harusi ziliendelea.

Baadaye alipata taarifa kuwa ndege aliyotumia Dk.Ian kusafirishia dawa zake kutoak Canada ilipata matatizo ya kiufundi ikiwa angani na kulipuka! Iliua abiria wote 241 waliokuwa katika ndege hiyo.


Kataloq: wp-content -> uploads -> 2017

Yüklə 0,95 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   2   3   4   5   6   7   8   9   10   ...   18
Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2022
rəhbərliyinə müraciət

    Ana səhifə