Sababu ya kumpiga tunayo! Nia ya kumpiga tunayo! Na uwezo wa kumpiga Nduli Idi Amin tunayo, ni lazima tumpige!Yüklə 0,95 Mb.
səhifə13/18
tarix31.10.2017
ölçüsü0,95 Mb.
#23549
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   18

“ Here we are!” (Tumefika!) alisema dereva na kupiga honi lakini kabla lango halijafunguliwa walitoka maaskari watatu na kulizunguka gari mmoja wao akimuhoji dereva aeleze alikuwa mgeni wa nani, alijitambulisha kwao na kuwaeleza kuwa aliwabeba wageni wa Dk. Ian! Aliposema hivyo tu lango lilifunguliwa, gari likaingia na watu wote waliokuwemo ndani ya gari wakaandika majina yao katika kitabu na kutia saini! Profesa Kadiri na mke wake walishangazwa na utaratibu huo. Kabla maaskari hawajaliruhusu gari mmoja wao alipiga simu ndani ya nyumba ya Dk. Ian .

“Who are they?” (Ni akina nani?) ilikuwa sauti nzito ya Dk Ian.

“Profesa Kadiri and Dr. Cynthia, they have claimed to be your Inlaws do you know them?” (Ni Profesa Kadiri na Dk. Cynthia wanadai wao ni wakwe zako! Unawafahamu?)

“Yes! They have come for their deaths! Rope them immediately and take them to the torture room! I don’t want to see them, they will undergo pains until their daughter Caroline is found, understood?” (Ndiyo, wamevifuata vifo vyao! Wafungeni kamba haraka na muwapeleke kwenye chumba cha mateso, sitaki kuwaona watateseka mpaka siku mtoto wao atakapopatikana! Umenielewa?)

“Yes, Sir!” (Ndiyo Bwana!)

Dereva wa teksi aliruhusiwa kuondoka na hapo hapo bila kuchelewa Profesa Kadiri na mke wake waliwekwa chini ya ulinzi na kufungwa kamba mikono na miguu, wakabebwa na kwenda kutupwa kwenye chumba cha mateso, watu wengi waliopelekwa huko hawakurudi salama.

“Please don’t treat us badly, we’re his inlaws!” (Tafadhali msitutende vibaya, sisi ni wakwe zake!) mama yake Caroline alisema huku akilia lakini hakuna aliyejali, yeye na mume wake wote walikuwa mgongoni mwa maaskari wenye nguvu wakipelekwa kwenye chumba cha mateso.

***************************

Harry na Jet

Ulikuwa ni mpango kamambe uliyopangwa kufanyika bila makosa, kwa utundu wake Harry aliichokonoa ndege ikiwa angani ili isiweze kunaswa na rada za nchi mbalimbali duniani, alijua alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba na hakutaka kupatikana, ilikuwa ni lazima afike nchini Kenya ambako angeiuza ndege hiyo kwa dolla za kimarekani milioni mia moja na themanini na tisa, huo ndio ungekuwa mwisho wa umaskini wake! Angekuwa tajiri tangu siku hiyo na si ajabu ndoto yake ya kuwa Rais ingetimia! Kwa mafuta yaliyokuwemo ndani ya tenki la ndege alikuwa na uhakika wa kufika mpaka Nairobi bila kutua mahali popote safari ambayo ingemchukua si zaidi ya masaa sita akiruka kwa mwendo wa kasi angani!

Alijua wazi kabisa kuwa alimwacha Caroline katika mateso makali kupita kiasi, alijua angekufa lakini hakuumia moyoni kwani alichokitaka yeye ni pesa na alikuwa ameipata. Kilichompeleka nyumbani kwa Dk. Ian kutafuta kazi hakikuwa ajira bali kuiba ndege hiyo, hakutegemea hata kidogo kukutana na Caroline pale! Hiyo ilikuwa ni bahati mbaya sana kwake, hakuwa na mapenzi na Caroline tangu shuleni isingewezekana ampende ukubwani, hicho ndicho alichoamini Harry!

“Ni bahati mbaya sana kwake! Halikuwa lengo langu hata kidogo kumfanyia yaliyotokea, lakini pia nisingeweza kusafiri naye kwenda kuiuza ndege hii ingekuwa hatari zaidi!”

Kabla hata ya kwenda nyumbani kwa Dk. Ian kutafuta kazi ya urubani Harry alishalipwa asilimia tano ya pesa zote kama tangulizo na sehemu ya pesa iliyobaki angemaliziwa baada ya kuifikisha ndege hiyo! Hivyo ilikuwa ni lazima kazi hiyo ikamilike na aliwafahamu vizuri wateja wake! Hawakuwa watu wema hata kidogo, walikuwa wauaji waliomiliki mtandao ulioitwa Al-qaeda ambao matawi yao yalisambaa sehemu mbalimbali duniani, walioihitaji ndege hiyo walikuwa na tawi lao nchini Sudan katika jiji la Khartoum ndiyo waliomiliki kiwanda cha madawa kilicholipuliwa na Marekani. Hata kama angejaribu kuwakimbia na hiyo asilimia tano ni lazima wangempata! Woga juu ya watu hao ndizo zilimfanya ashindwe kubadili nia yake pamoja na kuwepo kwa vipindi alivyomuonea huruma Caroline wakiwa Miami.

“I’m so sorry for Caroline, I know she is innocent! But I have put her into troubles!” (Namsikitikia sana Caroline, najua hana hatia na nimemuweka katika matatizo makubwa!) aliwaza Harry.

Masaa saba tangu aruke toka Vietnam Harry alitua na ndege yake kaskazini mwa Kenya karibu kabisa na mpaka wa nchi hiyo na Sudan, ulikuwa ni usiku wa manane! Baada ya kutua katika kiwanja cha muda kilichojengwa tayari kwa kazi hiyo Harry aliteremka kwenye ndege na kulakiwa na wazee wa nane wenye ndevu nyingi, alipowaangalia aligundua walikuwa Waarabu, wawili kati yao aliwafahamu! Ndiyo alioongea nao nchini Marekani juu ya mpango huo. Walimkumbatia na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya, baadae walimtambulisha kwa wazee wengine ambao pia walimshika mkono wa pongezi, kulikuwa na vijana wengine wawili wao walikuwa Waafrika kama yeye, aliambiwa walikuwa ni marubani waliotegemea kuirusha ndege hiyo kwenda Ujerumani kwa ajili ya kubadilishwa ili isitambulike.

Makabidhiano ya ndege hiyo yalichukua kama dakika ishirini tu, gari la mafuta ya ndege lililokuwa uwanjani hapo liliijaza ndege ya mafuta tayari kwa safari, marubani waliaga na kuingia ndani ya ndege! Harry alishuhudia ndege ikiacha ardhi taratibu na yeye alipakiwa ndani ya moja ya magari yaliyokuwepo uwanjani hapo tayari kwa safari ya kwenda Khartoum ambako malipo yangemaliziwa.

“Hivi kweli watanilipa hawa? Sijaingizwa mjini kweli?” alijiuliza Harry wakati magari yakichukua kasi.

********************************

Akiwa ndani ya mti Caroline aliendelea kushuhudia askari wakimsulubu mzee Nelson Peace, babu aliyejitolea kumsaidia, askari walizidi kumshinikiza aeleze ukweli wa mahali alipojificha! Kwa kipigo alichokipata mzee huyo, Caroline alikosa uhakika kama asingewaonyesha mahali alipokuwa. Roho yake ilimuuma sana kujua alikuwa ameingia tena mikononi mwa Wavietnam kitu ambacho hakutaka kabisa kitokee, pamoja na kipigo chote kilichotolewa bado mzee huyo hakudiriki kuyaonyesha maficho ya Caroline!

Kitendo kilichokuwa kikitokea kilimkumbusha enzi za watoto wake walipocheza mchezo wa kujificha ulioitwa kombolela! Alikumbuka kitu kimoja walichoamini watoto kuwa ukiuma meno huku umejificha mtu aliyekutafuta asingekuona, pamoja na kuwa mtu mzima Caroline alilazimika kuuma meno yake akiamini asingeonekana.

Mbwa walizidi kubweka wakiuzunguka mti aliojificha na waligalagala hadi chini kwa kilio, alielewa wazi walikuwa wakiwaonyesha ishara maaskari kuwa mtu waliyekuwa wakimtafuta alikuwa ndani ya mti huo! Maaskari walisogea hadi eneo hilo na kuanza kuuzunguka mti huku wakimburuza mzee Nelson chini ili awaonyeshe mahali alipokuwa Caroline lakini hakusema! Waliangalia juu ya mti lakini hawakumuona, mbwa nao walizidi kubweka wakiuzunguka mti huo mkubwa.

“Show us the girl, you goddamn oldman or else you are dead!” (Tuonyeshe huyo msichana aliyekuwa mzee vinginevyo tunakuua!) walizidi kumpiga mzee huyo, Caroline alitetemeka kupita kiasi na alihisi mkojo ukimpenya! Kwa kipigo alichopewa mzee huyo alijua kama yeye wangemkamata wangemuua kabisa. Mawazo yake yalimrudisha kwa baba na mama yake, alisikitika kufa akiwa mbali nao.

Je, nini kitaendelea? Harry atalipwa? Caroline atakamatwa? Wazazi wa Caroline watapatwa na nini? Wiki ijayo.

A

liendelea kujificha ndani 
ya tundu lililokuwemo 
ndani ya mti, lakini kwa kuchungulia kupitia katika upenyo uliokuwepo kati ya gome la mlango na mti wenyewe alishuhudia mzee Nelson Peace akiendelea kupokea kipigo kutoka kwa maaskari wa Kivietnam, tena wakati huo hata mbwa walikuwa wakimshambulia kwa kumuuma na meno yao makali yenye ncha, tayari walishaacha kubweka kuuzunguka mti!Pamoja na mateso yote aliyoyapata mzee Nelson hakudiriki kutaja mahali alipomficha Caroline! Alionekana kuwa mtu aliyekuwa tayari kufa yeye lakini si kuonyesha mahali alipokuwa binti huyo! Caroline alimshukuru Mungu kwa jambo hilo ingawa hakuwa na uhakika kama lingedumu kwa muda mrefu.

Dakika kumi na tano baadae mzee alikuwa hoi bin taabani kwa kipigo na maaskari wale walianza kumvuta kuelekea porini, Caroline alijua walimpeleka huko kumuua, hapakuwa na kitu kingine ambacho wangeweza kufamnyia, alijisikia huruma sana moyoni mwake kwa sababu alijua mzee huyo aliutoa uhai ili kuokoa maisha ya msichana asiyemfahamu! Machozi ya uchungu yalimtoka Caroline.

Baada ya maaskari kuondoka wakimvuta hali ilikuwa kimya kabisa, Caroline aliendelea kujificha ndani ya mti huo hadi jioni giza lilipoanza kuingia, tayari ulikuwa usiku mwingine! Kadri masaa yalivyozidi kusogea ndivyo giza lilivyozidi kuongezeka na lilikuwa kubwa zaidi ndani ya tundu alilojificha! Hali ilimtisha lakini alishindwa kufikiria kutoka ndani ya tundu kwa kuogopa kukamatwa, hakutaka kabisa kurudi tena mikononi mwa Wavietnam.

Mpaka majira ya kama saa tisa za usiku hivi, ingawa hakuwa na uhakika sana Caroline alikuwa bado yu ndani ya tundu, alikuwa hajapata hata lepe moja la usingizi, alikuwa bado yu katika maumivu aliyoyapata wakati wa kujifungua na uchovu wa safari ndefu ya kutembea kwa miguu. Kichwani mwake kulijaa mawazo mengi juu ya namna gani angeweza hatimae kufika Tanzania! Hiyo ndiyo nchi aliyoiota katika mawazo yake, aliamini kama ingetokea akafika Tanzania maisha yake yangebadilika! Alipowafikiria baba na mama yake ndiyo alizidi kuitamani Tanzania.

Pamoja na tamaa ya Tanzania, wazo moja tu lilimsumbua kichwani mwake, wazo la mauaji. Ilikuwa ni lazima awaue watu wote waliomfanyia ubaya katika maisha yake, hasa Harry! Alimchukia mwanaume huyo kupita kiasi, hakutaka hata kusikia jina lake! Aliamini ni yeye aliyeyaharibu maisha yake baada ya kuwa ametulia na Dk. Ian, ni yeye aliyemfanya awe mtu wa kusakwa na Mafia dunia nzima! na alijua kama siku moja angejikuta mikononi mwa mtu huyo adhabu yake isingekuwa nyingine zaidi ya kifo! Kwanini afe sababu ya makosa yaliyofanywa na Harry? Hilo ndilo swali lililomsumbua kichwani mwake.

“Naomba tu nisiingie mikononi mwake kabla sijalipiza kisasi, ni lazima niwaue Harry na wenzake ndipo Dk. Ian aniue! Ndiyo nastahili kifo kwa mabaya niliyomfanyia, lakini asiniue kabla sijatimiza kazi yangu!” Aliwaza Caroline akiwa ndani ya mti, orodha ya majina ya watu aliotakiwa kuwaua alimwijia kichwani mwake!

“Harry, Richard, Reginald na Dickson ni lazima wafe, walichangia sana kuharibu maisha yangu, lakini Harry atakuwa wa mwisho! Kama nitafika Tanzania nitajificha hadi nimalize kwanza kuwaua wenzake ndipo nitammalizia yeye na baada ya kifo chake sitakuwa na haja ya kuishi zaidi!” Aliwaza Caroline, alikuwa amekataa tamaa ya maisha kabisa hasa alipoufikiria umbali uliokuwepo kati ya mahali alipokuwa na nchi aliyotaka kwenda akiwa hana hata senti moja mfukoni!

Ghafla wadudu kama panya wakubwa walianza kudondoka kutoka eneo lililokuwa juu yake na kuanza kutafuna nyama za vidoleni mwake, hao ndiyo walimfanya aanze kufikiria kutoka ndani ya tundu, asingeweza kuyavumilia mateso aliyokuwa akiyapata.

Alivumilia kwa muda lakini baadae alishindwa na kuamua kukiondoa kipande cha gome kilichofunika tundu hilo na kuruka hadi nje ambako alipambana na giza nene kupita kiasi! Akiwa amesimama nje alisikia miungurumo ya manyama wakali kama Simba, hao ndiyo waliongeza hofu yake zaidi, aliogopa sana kifo cha kuliwa na wanyama, alikuwa tayari kufa kifo kingine chochote lakini si kifo cha kutafunwa hadi mwisho!

Hakuwa na mahali pengine pa kujificha zaidi ya kuingia ndani ya kijumba cha mzee Nelson! Alinyata taratibu na kuusogelea mlango wa nyumba hiyo, ulikuwa wazi na ndani yake pia hapakuwa na mwanga wowote ule! Akiwa ndani alipapasa kitanda na kuona mahali kilipokuwa akalala juu yake. Baadae alikumbuka kuwa hakufunga mlango na kurudi tena hadi mlangoni, ulikuwa na mlango wa miti uliotengenezwa vizuri, hakujua jinsi ya kuufungua kwa sababu haukuwa na komeo, ikabidi aurudishie tu mahala pake na kurudi tena kitandani ambako alijilaza na kuendelea na mawazo juu ya Tanzania na kilichokuwa mbele yake!

Masaa mawili baadae alisikia kitu kikijivuta nje! Alijua ni nyoka mkubwa kupita kiasi, alinyanyuka na kukimbia hadi mlangoni ambako aliushika mlango na kuugandamiza ili usifunguke, kitu hicho kilizidi kujivuta kuelekea mlangoni, Caroline alizidi kuingiwa na hofu na kuzidi kuusukuma mlango zaidi, kitu hicho kilipoufikia mlango kilitulia na baadae alisikia mlango ukigongwa taratibu! Kitendo hicho kilimfanya ahisi aliyekuwa nje alikuwa ni binadamu kwani mnyama asingeweza kugonga namna hiyo!

“Sijui ni nani? Au ndio wale maaskari wamerudi tena?” Alijiuliza Caroline huku akitetemeka mwili mzima! Na kadri mlango ulivyozidi kugongwa ndivyo hofu yake ilivyozidi kupanda.

“Who is there?” (Nani anagonga?) Hatimaye alijikuta akiuliza baada ya mlango kuwa umegongwa sana lakini bila sauti yoyote kusikika!

“Me?”( Mimi)

“You? Who and what are you?” (Wewe ni nani?)

“It is me Nel!” (Ni mimi Nelson)

Kauli hiyo ilimfanya aikumbuke sauti ya mzee Nelson Peace, pamoja na kuitambua bado hakufungua mlango mara moja, hakuamini kama mzee huyo alikuwa peke yake, alihofia watu walimtanguliza ili agonge na wamkamate.

“Lakini wamejuaje kuwa nipo humu?” Aliwaza Caroline huku macho yake yakichungulia nje, ingawa hali ilikuwa ya giza hakuona mtu yeyote aliyesimama wima zaidi ya aliyeonekana kulala chini, aliufungua mlango na kukuta kweli aliyekuwa amelala chini ni mzee Nelson.

“I’m sorry Nelson!” (Nisamehe Nelson)

“For ...wh..at?” (Kwa kosa gani?)

“For causing you all these troubles!” (Kwa kukusababishia matatizo yote haya!)

“Mention not, I was rea..dy to sacri..fice my li..fe for ..you!” (Usijali, niliku..wa tayari kupo......teza maisha yangu sab.....abu ...yako!) Alisema mzee huyo kwa shida kubwa.

“Won’t they come back?” (Hawatarudi kweli?) Caroline aliuliza kwa hofu, aliwaogopa sana wavietnam.

“I’m not sure, I guess they wont! They know I’m dead!” (Sina uhakika, nahisi hawawezi kurudi wanajua nimekufa!)

“Sure?” (Kweli?)

“Yeah!” Aliitika mzee Nelson.

Alimbeba na kwenda kumlaza kitandani, baada ya kuwekwa kitandani mzee Nelson alimweleza Caroline jinsi hali yake ilivyokuwa mbaya na kiasi gani hakuwa na matumaini ya kupona, mwili wake ulikuwa umeharibiwa vibaya mno kwa kipigo na kwa sababu hiyo alimruhusu asubuhi ya siku iliyofuata Caroline aendelee na safari yake amwache yeye afe peke yake kwani kifo ndio alichokihitaji na alimwelekeza njia ya kupita hadi kuingia mjini Penh! Kwa mtu mwingine ushauri huo ungeweza kuwa mzuri na wa busara lakini kwa Caroline alionekana tofauti kidogo.

“Siwezi kukuacha hapa porini, umenisaidia sana mzee Nelson ni lazima nami niwe tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako, kama maaskari watakuja basi acha waje na lolote litokee lakini siwezi kukuacha ufe peke yako” Alisema Caroline na aligundua tiba ya kumsaidia mzee huyo ilikuwa ni kumkanda na maji ya moto.

Alimuuliza kama alikuwa na kiberiti sehemu yoyote ndani ya nyumba ili apate kuwasha moto na kuchemsha maji ya kumkanda, jibu alilolipata hakulitegemea!Hapakuwa na keberiti ndani ya nyumba yake, moto ulipatikana kwa kupekecha vijiti viwili! Katika maisha yake Caroline hakuwahi kufanya jambo hilo hata mara moja na hakuja kama angeweza!

Alikumbuka kusoma upatikanaji huo wa moto katika historia tena akiwa shule ya msingi! Hakuwa na njia nyingine ya kupata moto zaidi ya hiyo na lengo lake lilikuwa kumsaidia mzee Nelson, aliulizia mahali vipande vya mti vilipokuwa na kuonyeshwa, akavichukua na kuviweka chini, akavuta nyasi kutoka darini mwa kibanda hicho na kuzivunjavunja kisha akaziweka sambamba na vijiti na kuanza kupekecha, ilikuwa kazi ngumu na alifanya kwa karibu masaa mawili ndipo moto ukapatikana, mikono yake ikiwa imechanika vibaya!

Caroline alifurahi kupita kiasi na alichofanya ni kuzidi kupuliza nyasi ili moto usizime, huku akiongeza nyasi zaidi! Aliongeza kuni na moto ukawa mkubwa! Akausogeza katikati ya mafiga matatu yaliyokuwa pembeni na kuchukua chungu kilichokuwa pembeni na kukijaza maji akakikalisha juu ya mafiga hayo, alizidi kuchochea kuni katika moto na haukupita muda mrefu maji yalichemka, tayari ilishagonga saa kumi na mbili asubuhi mwanga ulishaanza kuonekana nje ya kibanda.

Bila kuchelewa maji yakiwa bado ya moto alichukua kipande cha nguo cha mzee Nelson na kukidumbukiza ndani ya maji hayo kisha kukitoa na kumkanda nacho! Aliendelea kufanya hivyo kwa karibu saa nzima huku Mzee huyo akilalamikia maumivu aliyokuwa akiyapata lakini Caroline hakuacha kwani ndiyo tiba pekee aliyokuwa nayo! Baadae alimwacha.

Kazi hiyo ilifanyika kila siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku tatu mfululizo hali ya mzee Nelson ikaanza kuwa nzuri! Akawa na uwezo hata wa kukaa na kusimama mwenyewe bila msaada wa mtu! Mpaka wakati huo hapakuwa na mtu wala askari aliyejitokeza eneo hilo kumsaka Caroline.

Siku ya tano mzee huyo tayari alikuwana uwezo wa kutoka hadi nje, maji ya moto yenye chumvi aliyokandwa na Caroline kila siku yalimsaidia! Kwa siku zote hizo waliishi pamoja wakila matunda yaliyokuwa ndani ya kibanda hicho, siku ya sita mzee Nelson alitembea pake yake hadi porini na kurudi na majani mengi ya kijani na kumkabidhi Caroline akimwomba ayachemshe, Caroline alifanya hivyo na maji ya mazito ya kijani yalipatikana baada ya kuchemshwa! Mzee huyo akawa anakunywa maji hayo kila siku asubuhi na jioni, wiki moja baadae alikuwa mzima wa afya! Tatizo pekee lililomsumbua likawa ni makovu na vidonda mwilini.

**************

“Caroline!” Ilikuwa ni alfajiri na mapema mzee Nelson alipoliita jina hilo, Caroline alikuwa bado yu usingizini.

“Naam babu! Aliitika baada ya kuitwa kama mara tatu hivi.

“Nakushukuru kwa wema wako wote, umeokoa maisha yangu!”

“Wewe ndiye umeniokoa zaidi, bila wewe ningekuwa tayari nimekwishakamatwa na tayari ningekuwa marehemu, ulikuwa ni wajibu wangu mimi kukusaidia sababu nilikusababishia matatizo makubwa sana!”

“Usijali, ninachotaka kukuuliza ni kuwa, ni kitu gani unachotaka nikusaidie kwa sasa?”

“Nataka kufika kwetu Tanzania!”

“Lakini ujue Mafia wanakusaka na siyo rahisi kuwakwepa mjukuu wangu!”

“Lolote litakalotokea njiani ni sawa babu lakini ni lazima nirudi nyumbani!”

Mzee Nelson alisikiliza kwa muda huku akimwangalia Caroline usoni, alielewa ni jinsi gani msichana huyo alikuwa jasiri na asiyeogopa, hakutegemea msichana mdogo kama huyo kuwa shujaa kiasi hicho wakati alikuwa akitafutwa na watu hatari, Mafia. Kwa hakika alijua asingefika alikokuwa akienda! Asingefika Tanzania! Sehemu fulani njiani ni lazima angekamatwa na kuuawa, roho ilimuuma sana mzee huyo kwani alitokea kumpenda sana Caroline kama mjukuu wake.

“Kwanini wewe na mimi tusihame pamoja kwenda sehemu nyingine humu humu porini mpaka hali itulie? Miaka mitano baadae hakuna mtu atakayekuwa anakutafuta, hapo ndipo utaweza kujitokeza.”

“ Miaka mitano? Hapana babu, nashukuru kwa msaada wako lakini niache tu niendelee na safari yako na ningependa kesho nisonge mbele!”

“Kweli?”

“Ndiyo, ninachokuomba wewe ni kunipeleka mjini huko mbele nitajua mwenyewe cha kufanya, si unaweza kumpeleka kwa farasi wako?”

“Ndiyo!”

“Basi usiwe na wasiwasi, nipeleke kesho!”

“Lakini utakuwa usiku maana mimi huwa siingii mjini mchana!”

“Hakuna matatizo tukikaribia tu uniache, nitaingia mwenyewe! Kwani ni umbali gani kutoka hapa?”

“Siyo mbali sana!”

*****************

Siku iliyofuata saa mbili usiku waliondoka porini kuelekea mjini Penh wakitumia farasi ya mzee Nelson aliyeitwa Gaze, Caroline alikuwa amekaa nyuma na mzee Nelson akiwa amemkumbatia! Ulikuwa usiku wa kiza kinene lakini bado mzee huyo alimpeleka farasi kwa kasi ya ajabu! Alikuwa na uzoefu na njia, kulikuwa na baridi kali kupita kiasi usiku huo, meno ya Caroline yaligongana.

Tofauti na aliyosema mzee Nelson kuwa mjini palikuwa karibu, walisafiri kwa karibu masaa matatu katikati ya pori bila kufika, wakipishana na wanyama wakali wa kutisha. Caroline alichoka kukaa mgongoni kwa farasi.

“Bado tu!”

“Bado kidogo!” Alijibu mzee Nelson huku akicheka, ilivyoonyesha kulikuwa bado kuna umbali mkubwa sana lakini hakutaka kumvunja moyo Caroline, masaa mawili baadae taa zilianza kuonekana kwa mbali, hiyo ikaashiria walikuwa wakiingia mjini! Walikuwa wamesafiri kwa masaa saba porini! Mbele kidogo kama kilometa kumi farasi alianza kupunguza mwendo taratibu na hatimae alisimama na mbele chini ya mti mkubwa!

“Mjukuu wangu Caroline mimi kama nilivyosema huwa siingii mjini, nina miaka zaidi ya ishirini porini ninajua siku yoyote nikikanyaga mjini nitakamatwa, hivyo msaada wangu unaishia hapa! Nakutakia safari njema mjukuu wangu, nimefurahi sana kuishi nawe kwa siku hizi chache, ni matumaini yangu utarudi tena siku nyingine!” Alisema mzee Nelson, uso wake ulionyesha huzuni kubwa.

‘Sawa babu, ahsante kwa kila kitu , kwani utakuwa unaishi hapo hapo?”

“Hapana, nitahama, siwezi kuishi pale tena, nitatokomea ndani ya pori zaidi!”

“Sasa mwisho wako utakuwa kitu gani maishani?”

“Kufia porini tu siwezi hata siku moja kujitokeza, nitauawa!”

Walikumbatiana na kuagana, roho ilimuuma sana mzee Nelson kwa sababu alielewa Caroline asingefika alipokuwa akienda, ni lazima angekufa! Alibaki amesimama eneo hilo kwa muda mrefu akishuhudia Caroline akiishia gizani.

“Caroline!” Mzee Nelson alimwita, moyoni alikuwa akisikia huruma zaidi.

“Naam babu!”

“Tafadhali sana rudi, huko unakokwenda kuna matatizo makubwa mjukuu wangu!”

“Usijali babu, Mungu atanisaidia ni lazima nifike nyumbani nionane na wazazi wangu na nina kazi ya kufanya!” Alijibu Caroline na kuzidi kutokomea gizani kuelekea mjini.

******************

Jua la siku hiyo lilipojitokeza tayari alikuwa katika mji wa Penh ulikuwa ni mji mdogo lakini wenye watu wengi kuliko Dar es Salaam, kila mtu alionekana kutembea kwa kasi ya ajabu kuelekea kazini, watu wa mji huo walitumia punda zaidi kama usafiri wao na walivaa kofia kubwa za mikeka vichwani mwao! Kwao ulikuwa ni kama mtindo, hata wanawake pia walivaa hivyo.

Kila mtu aliyepita karibu yake alimshangaa Caroline alionekana ni mtu tofauti kabisa na wakazi wa eneo hilo! Rangi ya ngozi yake na hata ufupi wa nywele zake uliwashangaza wengi. Alishinda akizunguka huku na kule katika mji huo hadi usiku ukaingia, hakuwa na mahala pa kulala, na pia njaa ilimsumbua kupita kiasi, siku hiyo alilala katika veranda na hakula kitu chochote. Aliishi hivyo kwa siku mbili, siku ya tatu alishindwa ikabidi aingie katika hoteli moja kuomba msaada.

Mama mwenye hoteli hiyo alikuwa mzungu mzee na aliongea kiingereza cha kimarekani, Caroline alimfuata na kumuuliza shida yake ya njaa, mama huyo hakuuliza maswali mengi ila aliagiza apewe chakula, wakati akila chakula hicho Caroline aligundua mama huyo alikuwa akimwangalia sana, alishindwa kuelewa ni kwa sababu gani alifanya hivyo ila aliomba Mungu asijemgundua kuwa ndiye aliyekuwa akitafutwa na Mafia!

‘You are so beautiful, what’s your name my granddaughter?” (Wewe ni mzuri sana jina lako nani mjukuu wangu?)

“Marione, thank you for your kindness! (Naitwa Marione, ahsante kwa wema wako!) Caroline alimdanganya jina, hakutaka kabisa kulitumia jina lake halisi, aliamini jina hilo pamoja na sura yake vilikuwa almasi kwa wakati huo.

Baada ya hapo mama huyo alimdadisi Caroline mambo mengi juu ya mahali alikotokea na alikuwa nchini humo kufanya kitu gani, alizidi kumdanganya kuwa mume wake na yeye walikuwa wawindaji na walikwenda wote kufanya kazi hiyo katika misitu ya Cambodia lakini bahati mbaya mume wake alikufa kwa kukanyagwa na tembo!”

“Kwa hiyo mimi nimetembea kutoka porini hadi hapa!’

“Mungu wangu pole sana!’

“Ahsante bibi!”

“Ukitoka hapa utakwenda wapi?”

“Sina pa kwenda!”

Mama huyo aliyejulikana kwa jina la Suzanne alikubali kumpa Caroline kazi ya kuhudumia katika hoteli yake, siku iliyofuata alimpeleka dukani na kumnunulia nguo nzuri zaidi, alipendeza na kuvutia! Akaanza kuishi katika hotelihiyo pamoja na wasichana wengine waliyofanya kazi za kuhudumia na kupika. Kwa Caroline hiyo ilikuwa bahati kubwa, aliamini kwa utaratibu huo huo angefika Tanzania kwa wazazi na hatimae kulipa kisasi kwa watu waliomfanyia mabaya!

****************

Siku yake ya kwanza kazini ni wavulana watatu wa kimarekani ndiyo aliowahudumia, yeye ndiye aliyepanga kuhudumia wateja ambao hawakuielewa lugha ya kivietnam! Kila alipowapelekea huduma wavulana hao walinong’onezana kitu, hakuelewa walikuwa wakiongea nini juu yake, lakini alijua wazi walimteta yeye! Walipomaliza kula chakula mmojawao alimwita.


Kataloq: wp-content -> uploads -> 2017

Yüklə 0,95 Mb.

Dostları ilə paylaş:
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   18
Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©muhaz.org 2023
rəhbərliyinə müraciət

    Ana səhifə