“Kaza mwendo!” Alisema Xun akiwa ameshika mkono, alionekana kumvuta zaidi kuliko kumwongoza.
“Siwezi kuendelea!” Alisema Caroline akiwa amefumba macho sababu ya maumivu.
“Jikaze tu!”
“Kwa kweli siwezi! Kusonga zaidi ya hapa!”
Baada ya kusema maneno hayo tu, Caroline alianguka chini akiwa ameshika tumbo lake, alikuwa katika maumivu makali kupita kiasi, Xun alijaribu kumbembeleza ili anyanyuke waendelee safari yao lakini haikuwezekana! Caroline aligoma kabisa.
“Nikichelewa kurudi nitapoteza maisha yangu, tafadhali nyanyuka tuondoke!” Xun aliendelea kumbembeleza Caroline lakini bado aligoma.
“Siwezi kuendelea nakushukuru sana kwa kunifikisha hapa! Wewe unaweza kurudi Mungu atanisaidia kwa njia anayofahamu mwenyewe, ahsante kwa msaada wako, rudi kambini usije kupatwa na matatizo!”
Xun alikaa pale kwa karibu saa nzima na kushindwa kuvumilia zaidi, ingawa alimuonea huruma sana Caroline alilazimika kuondoka na kumwacha eneo hilo kurudi kambini! Muda mfupi tu baada ya Xun kuondoka mfuko wa mtoto ulipasuka na maji mengi pamoja na damu yakamwagika! Kichwa cha mtoto kilikuwa mlangoni! Caroline alikuwa akijifungua peke yake porini! Tena kabla ya wakati, safari ndefu aliyotembea ilimsababishia uchungu.
**************
Mkuu wa Mafia katika Cambodia, Meja Jenerali Chang Lou, alipata taarifa za ndege iliyotua porini na kulazimika yeye na wanajeshi kama ishirini kwenda kwenye kambi ya Wavietnam porini, walipoongea na mkuu wa kambi hiyo alikiri kuwa kweli ndege hiyo ilitua hapo lakini baadaye Rubani alitoroka nayo akimwacha mke wake. Mkuu wa majeshi aliomba kuonana na Caroline, walipomwaangalia katika kibanda chake asubuhi hiyo hawakumkuta! Askari aliyekuwa zamu usiku wa siku hiyo, Hung alikamatwa na kuwekwa rumande kwa kumtorosha Caroline!
Palepale bila kupoteza muda mbwa wa jeshi hodari wa kunusa harufu waliachiwa na kuingizwa ndani ya banda alilofungiwa Caroline kabla ya kutoroka ili kunusa harufu yake na baada ya hapo walianza kukimbia porini wakiifuata njia aliyopitishwa Caroline, pua zao zikiwa chini wakiifuata harufu! Maaskari walikimbia mbio nyuma yao wakiwafuata, kilometa 98 mbele mbwa walisimama kwenye uwanja wa wazi mahali ambapo Caroline na Hung walipumzika kabla hajakabidhiwa kwa Xun! Mahali hapo walilia kwa sauti ya juu kisha wakazidi kusonga mbele, kulikuwa kama kilometa tano tu mbele wafike eneo alilokuwa amelala Caroline huku kichwa cha mtoto wake kikichungulia.
Je, nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.
Akiwa peke yake porini na kwa nguvu zake zote Caroline alijitahidi, kusukuma hadi mtoto akatoka na kuanguka kwenye mchanga! Hakuwa na nguvu kabisa mwilini mwake, alilala chali akihema kwa nguvu, alionekana kama kupoteza kumbukumbu ya kitu kilichokuwa kimetokea, baada aliposikia sauti ya kitoto kikilia alikumbuka kilichotokea, hakuwa na maumivu tena.
Alinyanyuka na kukaa mikono yake yote miwili ikiwa nyuma yake ikisaidia asirudi tena ardhini! Alimwangalia mtoto wake kwa macho ya huruma, alikuwa mtoto mdogo mno, akilinganishwa na watoto wachanga, aliowahi kuwaona kwa makadirio yake mtoto huyo hakuwa hata na kilo mbili! Aliamii yote hayo ilitokea sababu ya mtoto hhuyo kuzaliwa kabla ya wakati wake! Alikuwa mtoto wa kiume, roho ilimuuma sana sababu kwa hali aliyokuwa nayo mtoto wake alijua asingeishi, alihitaji msaada mkubwa sana wa hospitali huduma ambayo kwa mahali alipokuwa asingeweza kuipata!
“Mtoto wa Harry huyu! Kaniachia mtoto kanikimbia, siji nitafika nae vipi nyumbani na hapa nilipo ni porini!Ah lakini Mungu anajua, asingeweza kunipa mtoto bila kunipa njia ya kujiokoa nae na kwa sababu ya mtoto huyu nina uhakika wa kuokoka sasa!” Aliwaza Caroline.
Alimnyanyua mtoto kutoka ardhini na kumbeba miononi mwake, alijisikia ……….na kumwekea mtoto ziwa mdomoni, alifurahi kuona mtoto akinyonya! Mpaka wakati huo kitovu kilikuwa bado hakijakatwa na hakuelewa kingekatika vipi, yeye na mtoto wake bado waliunganishwa na kitu kama utumbo uliotokea ndani mwake!
Muda mfupi baadaye alijisikia kuumwa na tumbo tena ghafla alijisikia kitu kama uchungu kikimrudia kilimuuma tumbo lake.
‘Isije kuwa nina watoto wawili!” Aliwaza Caroline uchungu ulizidi kuongezeka zaidi na zaidi, alikaa vizuri akijianda kuona kitu kilichotokea, lakini badala ya mtoto kutoka kilitoka kipande cha nyama na kuanguka chini, kikifuatiwa na damu nyingi, baada tu ya kipande hicho kutoka tumbo lilitulia tuli.
“Nafikiri hili ndilo huitwa placenta au kondo la nyuma!”Aliwaza Caroline huku akiangalia bonge hilo la nyama.
Lilikuwa bado limeungana na mtoto wake na hakujua ni kwa jinsi gani angelitenganisha na mtoto wake, sababu hakuwa na utalaamu wowote ule wa kuifanay kazi hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kujifungua, katika maisha yake hakuwahi kumwona mtu akizaa
“Sijui nitalikata vipi?” Aliwaza
Alisimama wima akiwa na mtoto wake mikononi! Kondo la nyuma likining’inia, sababu ya uzito wake aliona kama lilikuwa likimuumiza mtoto wake, alilinyanyua nalo akalibeba mkononi mwake, aliangaza macho yake huku na kule na kuona alikuwa katikati ya pori, hakujua wapi kulikuwa mashariki, magharibi, kaskazini wala kusini! Kila upande ulifanana na mwingine! Lilikuwa ni pori lenye vichaka na miti mirefu hakuamini kama kulikosa wanyama wakali.
Hapakuwa na dalili yoyote ya maisha ya binadamu katika pori hilo, ni milio ya ndege tu iliyosikika kila upande! Caroline alishindwa aelekee wapi kutoka hapo, ulikuwa ni wajibu wake kujiokoa.
“Ni lazima nisongee mbele! Siwezi kukisubiri kifo changu na mwanangu hapa!”Aliwaza Caroline na palepale aliamua kukatisha mkono wake wa kuume na kuanza kuchonga kuelekea porini zaidi, mtoto wake alizidikulia na aliendelea kumbembeleza huku akitembea katikati ya vichaka vyenye miiba mingi, alipozitupa fikra zake hadi nyumbani Tanzania aliwaona wazazi wake kimawazo, aliwaonea huruma sana pale ambapo wangepata taarifa za kifo chake! Alimwona mama yake akilia machozi huku akiliita jina lake.
“Mungu nisaidie ili siku moja niweze kufika nyumbani Tanzania na kuonana na wazazi wangu!” Aliwaza Caroline.
Kwa siku nzima alitembea porini akila matunda aliyoyaona katika miti! Hakukutana na mtu wala kuona njia za waenda kwa mguu! Hali iliyoonyesha hapakuwepo watu katika pori hilo, tayari alishaanza kukutana na wanyama kama Tembo, Twiga na Sokwe, kila alipowaona alijificha katika nyasi mpaka walipopita ndipo aliendelea! Alihofia Simba an Chui, ambao kwa hakika kama angekutana nao yeye na mtoto wake wangekuwa chakula chao! Alimwomba Mungu amuepushe na balaa hilo.
Jua lilikuwa kali mno na liliwachoma ipasavyo yeye na mtoto wake, hakuwa na nguo yoyote ya kumfunika mtoto jambo lililomlazimisha avue gauni lake na kumvalisha, yeye akabaki hivyo hivyo na kuendelea kutembea, hakuona aibu sababu hapakuwa na mtu yoyote wa kumwona porini.
Sababu ya kuunguzwa na jua mtoto alizidi kulia, Caroline alishindwa afanye kitu gani na alipomwekea titi mtoto hakunyonya tena, majira ya saa 9 akiwa tayari amekwishatembea kilomita 45 katikati ya pori mtoto wake alinyamaza kulia, akiamini alikuwa amepitiwa usingiz, kunyamaza huko kulimfanya aondokewe na wasiwasi wa kuliwa na wanyama! Akaongeza bidii ya kutembea zaidi kwenda mahali kusikojulikana akiamini ni lazima angefika mahali Fulani walipoishi watu, hata kama ingechukua wiki tatu za kutembea.
Mpaka saa 12 jioni bado mtoto wake alikuwa hajalia! Wala kujitingisha, Caroline alishtuka na kumwangalia mtoto wake, aliangua kilio alipokuta tayari mtoto wake amekwishakauka mikononi mwake! Alikuwa amekufa! Alikaa chini na kuanza kulia kwa uchungu, hakuamini mpaka alipoweka sikio lake kifuani kwa mtoto kutousikia moyo ukipiga ndipo akaamini kweli mtoto wake hakuwepo tena duniani!
Hakuwa na la kufanya zaidi ya kuuzika mwili wa mtoto wake, bila kuchelewa ingawa mwili wake haukuwa na nguvu nyingi alivunja tawi la mti na kulitumia kuchimba ardhini! Ingawa alikuwa peke yake aliamua kuuzika mwili wa mtoto wake ambaye alikuwa bado hajampata hata jina kwa heshima zote za kibinadamu.
Sababu ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha udongo ulikuwa laini na kwa kutumia mti tu alifanikiwa kuchimba shimo dogo lenye urefu wa Cm………………kwenda chini na kuweka mwili wa mtoto wake ndani kabla ya kufukia alipiga magoti …………….machozi yalikuwa yakimtoka, wakati wote wa zoezi hilo! Alikuwa na uchungu mkubwa mno kumpoteza mtoto wake ambaye pamoja na ukatili ambao Harry alimfanyia alimwachia kama ukumbusho!
Baada ya kusali Caroline alinyanyuka na kusimama wima kabisa, akiliangalia kaburi dogo la mtoto wake, roho ilizidi kumuuma na alijua mtoto wake alikuwa ametangulia na yeye angemfuata baada ya muda si mrefu! Alijua na yeye angekufa katika masaa machache tu yaliyomfuata! Hakuwa na uhakika wa kutoka katika pori hilo akiwa salama na hata kama angetoka bado aliamini asingeweza kuukimbia mkono wa Dk. Ian ni lazima siku moja angeuawa kikatili! Bado alimlaumu Harry kwa yote hayo zaidi ya yote yeye mwenyewe kwa kuukubalia moyo wake kwa kila alichomweleza!
”Safari inaendelea, ni lazima nisonge mbele, mtoto nimepoteza lakini jukumu langu la kujiokoa bado lipo palepale!”Aliwaza Caroline na kuanza kutembea taratibu, kwa hatua tatu mbele alisimama, akageuka na kuliangalia tena kaburi la mwanae! Machozi yakamtoka.
Alizidi kusonga mbele kwa masaa kama mawili giza likaanza kuingia, hakuwa na mahali pakulala zaidi ya kupanda katika mti mkubwa wa mkuyu uliokuwa jirani yake, kabla hajapanda aliwaza nyoka! Alikumbuka picha katika kitabu kimoja alichosoma akiwa mtoto ilimwonyesha mtu akipanda mti juu ya mti huo kulikuwa na nyoka mkubwa na chini ya mti alikuwepo Simba! Mtu huyo alitakiwa kuchagua ni wapi aende!
“Na mimi yasije kunipata hayo hayo!” Aliwaza Caroline lakini hakusita alikuwa kama mtu aliyekwishakata tamaa ya maisha, aliuparamia mti huo na kupanda hadi juu yake bila kupata tatizo lolote!
”Nitalala hapa hadi asubuhi, kisha safari inaendelea!” Aliendelea na mawazo kichwani mwake huku akijigeuza ili asianguke, mwili wake wote ulikuwa umechoka, alilivua tena gauni lake na kujifunga kwenye mti ili asidondoke akisinzia.
************
“Wu! Wu! Wu!”
“Uwiiiiiii! Uwiiiiii! Uwiiiii!” Mbwa walilia wakinusa chini, maaskari walipoangalia vizuri ardhini waliona damu ikiwa imemwagika katika majani, walishindwa kuelewa ni kitu gani kilitokea eneo hilo !Wote waliangaliana bila kuelewa cha kufanya!
“Sasa hii damu ni ya nini?”
“Labda amejifungua maana niliambiwa alikuwa na mimba kubwa!”
“Kweli eh?”
“Inawezekana kabisa!”
“Basi kama amejifungua hayupo mbali na mahali hapa msako uendelee!”Maaskari waliendelea na maongezi yo, ilikujua mwelekeo wa mahali alipokwenda Caroline baada ya kutoka hapo waliwategemea mbwa wao ambao bado waliendelea kunusa ardhini wakilia, kuashiria walikuwa wamekosa kitu walichokuwa wakikitafuta.
Kutoka hapo mbwa walikata kushoto na kuzidi kuelekea porini, askari wakiwafuata nyuma huku wakikimbia mbio, kila mmoja wao alionekana kuwa amechoka, hilo liliwatia hasira zaidi maaskari hao.
“Na tukimkatama sijui kitatokea nini, katusumbua sana huyu mwanamke!”
“Sasa hivi tutamkamata, inavyoonekana hayupo mbali na mahali hapa!” Walizidi kuongea wakiwafuata mbwa wao nyuma, walishangaa kuona masaa yakizidi kusonga mbele bila kumpata, walikwenda kama kilometa……….ndipo mbwa wao waliposimama tena na kuanza kulia, huku wakifukua ardhini! Maaskari wote walishangaa kuona mbwa wakitoa maiti ya mtoto katika udongo!
“Aisee kweli kajifungua mtoto kafariki na akazika hapa tena ni masaa machache tu yaliyopita si mnauona udongo ulivyo?”
“Ndiyo!”
“Achaneni na hicho kiumbe tuwasikilize mbwa nina imani hayupo mbali na maeneo haya!”
Wote waliendelea kuwafuata mbwa wao nyuma, waliokimbia bila kuchoka, ardhi ya sehemu hiyo ilikuwa ya udongo wa mfinyanzi kila mahali walipokanyanga palionyesha alama za miguu na walipochunguza mbele yao pia waliona alama za miguu ardhini, kila mtu akawa na uhakika ilikuwa ni miguu ya Caroline.
“basi kazi imekwisha kwa alama hizi tutampata sasa hivi!”
“Tena kakanyaga humu si muda mrefu!”
Waliendelea kuwafuata mbwa na alama za miguu hadi giza likaingia ikabidi wawe wakitumia tochi, walizifuata nyayo hizo hadi zikapotelea chini ya mti mkubwa wa mkuyu! Waliangalia huku na kule kuona kama ziliendelea lakini hawakuona mahali popote hata mbwa wao walishindwa kuendelea zaidi.
“Nafikiri kapanda humu mtini!”
“Inawezekana!” Walijibishana wao kwa wao na kisha kuanza kumulika kwa tochi zao mtini wakiangalia.
“Yupo humu humu tu!”
***********
Muda mfupi tu baada ya kupanda mtini kwa ajili ya kulala macho ya Caroline yaliona moto ukiwa jirani tu na maeneo hayo, alichojifunza katika historia ni kuwa mahali popote palipowaka moto kulikuwa na binadamu! Moto huo ulitokea kama kilometa tano tu kutoka eneo hilo, ingawa aliogopa sana kuingia tena mikononi mwa Wavietnam alijikuta akipatwa na ushujaa ambao hata yeye hakuutegemea na kushuka haraka mtini na kuanza kutembea akiufuta moto huo! Alipita katika vichake taratibu sababu ya kiza, badala ya mita mia tano kama alizotegemea alijikuta akitembea kama kilometa mbili ndio akaufikia moto huo.
Uliwaka chini ya miti mine mikubwa ambayo juu yake kulijengwa kibanda! Alionekana kuishi mtu maeneo hayo na aliishi peke yake, Caroline bila kuogopa alianza kupiga kelele kwa kiingereza akimwita mwenye nyumba hiyo lakini bado hali ilikuwa kimya kabisa, muda mfupi baadaye alishangaa kuona kitu kikilipuka alishindwa kuelewa kama kitu hicho kilikuwa binadamu au la!
Badala ya Caroline kukimbia alibaki amesimama eneo hilo, bila kujua cha kufanya, mwili wake wote ulikuwa ukitetemeka kwa hofu, badala ya kitu hicho kukimbia hali ikawa kimya kabisa, dakika kama ishirini hivi baadaye alisikia nyasi zikitingishika nyuma yake, alijua ni mnyama mkali lakini hakuwa hivyo alikuwa ni binadamu akitembea kuelekea mahali aliposimama Caroline.
“Wewe nani?” Aliuliza kwa lugha ya Kiingereza mzee huyo mwenye ndevu nyingi nyeupe na mgongo wake ulikuwa umepinda, kabisa na alikuwa amenyoosha upinde wake tayari kuachia mshale!
“Tafadhali usiniue sina matatizo yoyote, nahitaji msaada!”
“Nimekuuliza wewe ni nani? Na unatafuta kitu gani hapa?”
“Tafadhali naomab ushushe mshale wako chini ili nikueleze!”
“Sema kwanza wewe ni Interpol?”
“Hapana mimi siyo polisi ninaitwa Caroline, ninakimbia kuokoa maisha yangu, wanataka kuniua!” Alisema Caroline na alipomaliza tu sentensi hiyo mzee …………..upinde na kushusha mshale chini, akamsogelea karibu na wote wawili wakakaa chini, Caroline alimsimulia kila kitu kilichotokea katika maisha yake, tangu kifafa hadi Dk.Ian na alivyokutana tena na Harry!
“Mjukuu wangu kwanini ulimwamini tena?”
“Ni shetani tu aliniingia babu!”
“Ninamfahamu vizuri Dk. Ian baba yaek Smith niliwahi kufanya naye biashara!”
“Ulifikaje hapa porini babu?”
“Ni habari ndefu sana ila niliua watu wengi sana nikiwa na gaidi la Kimataifa Carlos na hivi sasa dunia inanitafuta hakuna mtu yeyote anayejua niko hapa, ninaishi hapa peke yangu kwa miaka ishirini na sita!”
“Sawa babu utanisaidiaje mimi kufika nyumbani?”
“Kwanza kabisa naomba nikueleze wazi kuwa hivi sasa ni lazima ……………….! Ninawafahamu mafia sababu nimefanya nao kazi, ninajua wapo njiani wanakuja na watafika hadi hapa! Kifupi hutakiwi kabisa kukaa hapa!”
“Sasa nitafanya kitu gani?”
“Subiri hapohapo nije!”Alisema mzee huyo na kuondoak aliporudi baada ya kama dakika tano hivi alimchukua Caroline na kumzungusha nyuma ya nyumba yake kulikokuwa na mti mkubwa sana, upana wa mti huo usingeweza kupungua mita……………….ulionekana kuwa miongoni mwa miti mingi ya zamani, alishangaa kumwona mzee huyo akibandua sehemu Fulani katika mti ndani yake ikaoneana sehemu kubwa iliyowazi.
“Mjukuu wangu ingia hapa, utajificha nitakuhudumia kila kitu ukiwa humo, mpaka nitakapoona hali ni nzuri kukusaidia!”
“Sawa babu!”Aliitikia Caroline na gome la mti lilirudishwa mahali pake, ndani kikawa kiza.
Dakika tatu tu baada ya kumfungia Caroline ndani ya mti nyumba ya mzee…………….ilivamiwa na kundi la mbwa, walimwangusha chini na kuanza kumng’ata! Sekunde chache baadaye wakaingia askari wenye bunduki na kuwaamuru mbwa wamwachie mzee huyo.
“Tueleze yule msichana yupo wapi?”
“Ngojeni kwanza, msinipige subirini kwanza!” Alijibu mzee huyo.
Caroline aliyasikia maneno hayo kutoka ndani ya mti na kujua ni lazima mzee……………….angewaonyesha mahali alipokuwa! Alijua mwisho wake umefika, alilia kwa chungu, hakuwa tayari kurudi tena kwa Wavietnam kupitia katika ufa wa mti alishuhudia mzee……………akipigwa kupita kiasi tena bila huruma, mbwa wao waliendelea kumng’ata bila huruma!
”Yaani kweli huyu mzee hatasema?”Alijiuliza Caroline bila kupata jibu alipofikiria kutoka ili akimbie alishindwa sababu mbwa wangemwona na kumkamata!
Je nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo
Wazazi mikononi mwa kifo
B
aadae taarifa za kutoroka
kwa mke wa Dk. Ian,
Caroline kadiri tena pamoja na ndege aliyonunuliwa ambayo thamani yake ilikuwa zaidi ya dola milioni mia mbili, zilianza kutangazwa karibu na vyombo vyote vya habari duniani! Hiyo ikimaanisha redio, magazeti, televisheni hadi ndani ya mtandao wa intaneti! Karibu kila binadamu alilielewa jambo hilo ingawa hawakuelewa kitu chochote juu ya msako ulioendelea kimya kimya, Mafia hawakutaka kutangaza juu ya msako huo, walitaka kutumia mtandao wao kuwakamata Caroline na Harry kirahisi.
Taarifa zilipowafikia wazazi wa Caroline, mama yake Dk. Cynthia na baba yake Profesa Kadiri walichanganyikiwa, walishindwa kuelewa nini kilichompata mtoto wao mpaka kufikia uamuzi wa kutoroka, walimfahamu vizuri Caroline, hakuwa mtu wa kuchukua maamuzi ya haraka haraka bila kufikiria! Waliamini haukuwa uamuzi wa Caroline, walichohisi wao ni kwamba alitekwa na kupelekwa mahali kusikojulikana. Walihofia maisha ya mtoto wao, walijua pengine alikuwa marehemu kwa wakati huo! Mama yake alilia mno siku alipoiona sura ya mwanae akitangazwa katika luninga kuwa alikuwa ametoroka.
Walikaa kwa wiki tatu wakisubiri Dk. Ian awapigie simu na kuwataarifu juu ya kilichotokea lakini hakufanya hivyo na walipopiga wao na kutaja majina yao waliambiwa Dk. Ian hakuwepo Canada wakati huo alikuwa safarini Miami kufuatilia ndege yake iliyopotea, kila siku walipopiga simu walijibiwa hivyo! Hilo ndilo lilizidisha wasiwasi zaidi ya maradufu, walishindwa kuelewa ni kwanini Dk. Ian hakufanya hivyo!
Baadae fikra zao zilianza kuwafanya wafikiri labda nae alikuwa pamoja na Caroline ndani ya ndege lakini kwa mujibu wa habari zilizoendelea kutangazwa katika vyombo vya habari Dk. Ian hakujajwa mahali popote, hilo walilifuta na uamuzi uliowaijia vichwani mwao ambao waliouona wa busara ulikuwa ni kusafiri hadi Canada kwenda kuujua ukweli kutoka mdomoni mwa mkwe wao Dk. Ian.
Hawakuhisi hata kidogo kuwa ni hasira ndiyo ilimfanya Dk Ian asiwapigie simu wala kuwatumia ujumbe wowote kuwataarifu juu ya yaliyompata mtoto wao! Dk. Ian alimchukia kila mtu kuanzia Caroline mpaka wazazi wake, alichokuwa amefanyiwa kilikuwa kitu kibaya sana, tayari kilishamrudisha kwenye kazi ya Mafia ambayo aliiacha muda mrefu, alikuwa tayari kumuua mtu yeyote au kufanya jambo lolote ili mradi ampate Caroline!
“Inabidi twende huko Canada, nafikiri mkwe wetu atakuwa na jibu zuri la maswali yetu!” Profesa Kadiri alimwambia mke wake.
“Unafikiri ni sawa tukisafiri wote?”
“Sioni ubaya wowote!”
“Gharama je?”
“Usijali tutatumia pesa tuliyonayo katika akaunti yetu, ni vyema tukasafiri wote wawili!”
“Sawa basi, hakuna tatizo nitaomba ruhusa kazini, nafikiri wataniruhusu maana hata wasiponiruhusu kazi hazifanyiki!”
“Utawezaje kufanya kazi wakati mwanao yupo wenye matatizo makubwa kiasi hicho?”
Maandalizi ya safari yalianza kufanyika, walichukua pesa katika akaunti yao na kukata tiketi mbili za ndege kwenda na kurudi Canada katika shirika la ndege la Uingereza, British Airways! Ndege za shirika hilo zilianzia safari yake Nairobi nchini Kenya, hivyo baada ya kukamilisha taratibu zote kwa sababu wao waliishi Arusha walisafiri moja kwa moja hadi Nairobi ambako walipanda ndege na kuondoka kwenda zao Canada, hawakuwa na furaha hata kidogo na safari hiyo! Tofauti na safari nyingine zote walizokwisha safiri pamoja kwenda nchi za nje, njia nzima Dk. Cynthia alilia akimlilia mwanae! Hakuwa na uhakika wa kumkuta nchini Canada na hakujua kama alikuwa hai au amekufa.
Walitua uwanja wa ndege wa Ottawa nchini Canada saa kumi na mbili jioni, walikuwa wamesafiri karibu masaa kumi na nane njiani sababu ndege waliyopanda ilikuwa na mizunguko mingi na ilitua katika nchi za Dubai, Sweden, Norway, Denmark ndiyo ikaingia Canada! Kila mtu alikuwa amechoka sana wakati wanatua katika uwanja huo, hapakuwa na mtu wa kuwapokea uwanjani na kila kitu kilikuwa kigeni kwao! Ilikuwa ni siku ya kwanza kwao kuingia katika nchi hiyo kwani kila mara Caroline alipowaalika kwenda kumtembelea walikataa!
Kwa taarifa walizokuwa nazo Dk. Ian alikuwa mtu maarufu sana katika nchi hiyo, hawakutegemea ingekuwa kazi ngumu kwao kumpata, walichokifanya kwa haraka baada ya kutoka nje ya uwanja ni kumwita dereva teksi aliyekuwa jirani akiita abiria na kumuuliza kama anamfahamu Dk. Ian.
“Yeah! I know him!” (Ndiyo namfahamu!)
“Can you take us to his resdential pallace?” (Unaweza kutupeleka nyumbani kwake?)
“That’s very easy to do!” (Hilo ni jambo rahisi sana kufanya!)
“How much are we going to pay you?” (Tutakulipa shilingi ngapi?)Mama yake Caroline aliuliza ili kujiepusha na migogoro ya abiria na madereva teksi kama ambay hutokea nchini Tanzania.
“We normally charge five dollars!” (Kwa kawaida tunatoza dola tano!)
“I think we can afford that!” (Nafikiri tunaweza kumudu!)
“Then let’s go!” (Basi twendeni!) Alisema dereva na kuwafungulia milango wote wakaingia.
Safari ilianza kutoka uwanja wa ndege wa Ottawa kuelekea nyumbani kwa Dk. Ian, giza lilikuwa bado halijaingia hivyo Profesa Kadiri aliweza kuiona vizuri mandhari ya jiji hilo maarufu duniani, alishangaa kuona majengo marefu kuliko hata aliyoyaona nchini Uingereza alikokwenda masomoni! Pamoja na giza kuanza kutanda bado watu walikuwa wengi mitaani na karibu watu wote aliowaona walikuwa ni wazungu, mara chache sana aliwaona watu weusi! Mke wake wala hakuangalia nje wakati wote gari likipita uso wake aliulaza kwenye miguu ya mumewe na kuendelea kulia kwa uchungu, alikuwa na mawazo mengi sana juu ya mwanae.
Gari liliuacha mji na kuanza kwenda nje katika maeneo yaliyokuwa na miti mingi, alishindwa kulifananisha jiji hilo na jiji la Dar es Salaam ambalo halikuwa na miti kabisa! Aliwasifu watu wa Canada kwa kutunza mazingira yao, kila sehemu aliyoiona ilikuwa kijani na ilivutia macho kuangalia.
“Where are you from?”(Nyinyi ni watu wa wapi?) Dereva aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu.
“We are from Tanzania!” (Tunatoka Tanzania!)
“Tanzania?” aliuliza dereva kwa mshangao.
“Yes, heard of it?” (Ndiyo, umewahi kuisikia?)
“Yeah! Yeah! Yeah! It is the most peaceful country in Africa, isn’t it? “( Ndiyo! Ndiyo! Ndiyo! Ni nchi yenye amani zaidi katika Afrika, au siyo?)
“You are right!” (Sawa sawa!)
“How are you related to Dk. Ian?” (Nyie mna uhusiano gani na Dk. Ian?)
“He is our son in law!” ( Amemuoa binti yetu!)
“So you mean the girl who escaped with his jet, you daughter?” (Kwa hiyo mna maana yule binti aliyetoroka na ndege yake ni binti yenu?) aliuliza dereva kwa mshangao, macho yake yalionyesha hofu kubwa.
“Ofcourse she is!” (Ndiyo ni binti yetu!)
“Are you not afraid of him? At the moment Dr. Ian is not a good person! He has killed more than ten workers within his pallace since his wife escaped! I’m sure you wont leave his home safely” (Hammuogopi? Kwa sasa hivi Dk. Ian siyo mzuri, ameua zaidi ya wafanyakazi kumi ndani ya makazi yake tangu mke wake atoroke, nina uhakika hamtaondoka salama!)
“No! We’re sure he wont do us any harm!” (Hapana, tuna uhakika hawezi kutudhuru sisi!) alijibu Profesa Kadiri kwa uhakika, haikuwa rahisi kwake kufikiria kuwa Dk. Ian angeweza kuwafanyia mambo aliyosema dereva huyo.
“Please take my words!” (Tafadhali aminini ninachokisema!) aliongeza dereva lakini hawakutaka kumuelewa walimwomba aongeze mwendo ili wafike upesi, dereva aliwatiii wateja wake na mbele kidogo gari lilikata kulia kuelekea kwenye lango kubwa ambalo mbele yake kulikuwa na bango lenye maandishi Dk. Ian Smith Resdential Pallace.
Dostları ilə paylaş: |